KINGAZI BLOG: 04/20/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Wednesday, April 20, 2016

Hatimaye Mwili Uliozama na Gari Baharini Jijini Dar es Salaam Wapatikana



Mnamo majira ya saa 10 alfajiri, gari aina ya Hiace  iliteleza toka kwenye kivuko na kutumbukia katika bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam.

Gari hiyo ilikuwa na abiria wawili. Mpaka majira ya asubuhi, jeshi la zimamoto na uokoaji lilifanikiwa kuupata mwili mmoja na likaendelea kuutafuta mwili wa pili.

Mchana  huu  umepatikana mwili wa pili  wa Nice Karagwe  huku zoezi la kuitoa gari likiendelea

chanzo.Udaku special blog.
 
 
Wasiliana nasi;Kama una tangazo,habari,picha,maoni na ushauri n.k kupitia 0716528779/0755542721 na email.titoemmanuel@gmail.com

HATIMAYE Barakah Da Prince Amvisha Naj ‘Pete ya Uchumba'


Barakah Da Prince ambaye kwa sasa amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa kike, Naj, amedai kupiga hatua zaidi kuelekea kwenye uchumba.

Wamefunguka exclusively kwa Bongo5 kuhusu uhusiano wao:

“Yeah ni kweli mimi na Naj tuna uhusino na hadi kwetu nimeshamtambulisha na yeye kwao najulikana na pia nimemvisha pia pete, sio ya uchumba ila ni Promise Ring,” amesema Barakah.

“Ndio hivyo yaani kuna kazi pia ambazo tumefanya ila hazitatoka sasa hivi hadi kwanza kila mtu atoe single yake halafu ndio itakuja hiyo ngoma ya pamoja mimi na Naj,” ameongeza.

Kwa upande wake Naj amesema:

Ni kweli Barakah amenivisha pete kama alivyosema. Kwangu ni furaha sana maana nimeshakuwa na mahusiano yaliyopita lakini sikuwahi kufanya kitu kama hiki. Naona kabisa kuwa mahusino haya ni ya ukweli na naona kuna malengo kabisa, nafurahia kwakweli.”

“Bado hatujaanza kuishi wote ila muda mwingi tupo pamoja, nafurahia mahusiano yangu ya sasa. Ni kweli tumefanya ngoma ya pamoja lakini haitatoka sasa hivi mimi natakiwa niachie ngoma yangu na pia nishoot video, halafu pia nitarudi Uingereza mara moja, kuna vitu vyangu kule then nitarudi tena Bongo.”

Chanzo:Bongo5

 Kama una tangazo,habari,picha,maoni na ushauri,Wasiliana nasi kupitia namba zifuatazo;0716528779/0755542721 na

- EMAIL titoemmanuel93@gmail.com

Msomi avua nguo zote kwa kufungiwa ofisi


Stella Nyanzi alikuwa akimuunga mkono mgombea urais Kizza Besigye
Hatua ya mwanamke mmoja msomi ya kuvua nguo nchini Uganda imezua mjadala mkali nchini humo.

Chris Brown:Nilitaka kujiua kwa sababu ya Rihanna

Nilitaka kujiua kwa sababu ya Rihanna
Mwanamuziki Chris Brown amesema kuwa alitaka kujiua baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenziwe Rihanna kabla ya tuzo za Grammy mwaka 2009.

Gari Latumbukia Baharini Wakati likisubiri Kivuko cha Kigamboni leo Asubuhi..Lilikuwa na Watu Wawili Ndani

 
 Habari mbaya imetufikia kuwa leo asubuhi eneo kivukoni Kigamboni kuna gari ambalo lilikuwa linasuburia kivuko ili kuvuka limeingia baharini huku likiwa na watu wawili ndani yake mpaka sasa

Bunge Laanza Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lugumi




Hatimaye taarifa ya utekelezaji wa mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises, iliyoshinda zabuni mwaka 2011 ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37, umetua ndani ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na kuanza kujadiliwa.

Akizungumza jana bungeni, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hilaly alisema taarifa ya utekelezaji wa mkataba huo, ilifikishwa bungeni juzi na jana asubuhi wamepewa na wakaanza kuujadili papo hapo.

“Wametuletea taarifa ya utekelezaji wa mkataba huo leo asubuhi (jana), ila taarifa hiyo ilifika bungeni jana (juzi), na sisi kamati tumekaa asubuhi kuijadili kama tulivyokubaliana wakati wa vikao vya kamati mjini Dar es Salaam na tutatoa taarifa ya maamuzi ya kamati,” alisema Aeshi ambaye ni Mbunge wa Sumbawanga Mjini.

Akizungumza baada ya kuahirisha kikao cha kamati hiyo jana jioni, Aeshi alisema hawajafikia maamuzi na kwamba leo wataendelea kujadili taarifa hiyo na mchana watatoa maazimio ya kamati.

“Tumeahirisha kikao hadi kesho (leo) na bado tunapitia taarifa hiyo na kama kamati itaona haja ya kuwaita tena jeshi hilo kutoa maelezo, tutajua baada ya kufikia maamuzi,” alisema Aeshi na kuongeza kuwa kwa sasa wanachambua taarifa hiyo na iwapo wataona kuna haja pia ya kuutaka mkataba huo watatoa maelekezo.

Awali, Aprili 5, mwaka huu mjini Dar es Salaam, kamati hiyo ilitoa siku saba kuanzia siku hiyo kwa Jeshi la Polisi nchini, kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi iliyopewa zabuni ya kufunga mashine 108 katika vituo tajwa nchini, ila hadi sasa ni vituo 14 tu ndivyo vilivyofungwa mashine hizo.

Hatua hiyo ilikuja baada ya kamati hiyo kukutana na jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu za jeshi hilo za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kubainika kuwa na ukiukwaji wa utekelezaji wa mkataba huo.

Ukiukwaji wa utekelezaji wa mkataba huo mwingine ni pamoja na kampuni hiyo kulipwa asilimia 99 ya fedha zote za mkataba huo wenye thamani ya Sh bilioni 37, huku kazi iliyofanywa ni chini ya robo.

“Ukiangalia kazi iliyofanywa tangu mwaka 2011 hadi leo ni kidogo na pesa hawa kampuni wameshachukua asilimia 99, sasa tumewaagiza watuletee huo mkataba ndani ya wiki moja walioingia na kampuni hiyo ili tuupitie,” alisema Aeshi wakati wa vikao vya Dar es Salaam.

Hata hivyo, baada ya maagizo hayo, taarifa hiyo ya utekelezaji haikuwasilishwa kwenye kamati hiyo ndani ya muda uliokubaliwa na Aeshi alisema siku zote wamekuwa wakitoa maagizo kwa mdomo na taasisi nyingi zimekuwa zikitekeleza.

Aliongeza ila hilo la mkataba wa Lugumi lilikuwa tabu kutekelezwa hadi kamati hiyo, ilipochukua hatua za kukumbushia kwa kuandika maelezo.

Hata hivyo, baada ya taarifa za mkataba huo,zilisambaa habari kwenye vyombo vya habari kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (CCM), Said Lugumi na vigogo wengine.

Kutokana na sakata hilo, mbunge huyo alikanusha kuhusika kwake na kusema ni kweli kwamba ana urafiki wa kawaida na Said Lugumi na kusisitiza kwamba hahusiki kwa njia yoyote na kampuni hiyo.

“Kwanza kabisa mimi si mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo, hilo ni jambo la msingi kabisa watu waelewe na sijawahi kufanya biashara yoyote na Lugumi. Said Lugumi ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo tunafahamiana naye na ni rafiki yangu,” alisema Ridhiwani.

Baada ya kutumbuliwa jipu na Rais Magufuli jana Mkurugenzi wa jiji la dar WILSON KABWE asema haya.

Baada ya kusimamishwa kazi na Rais Magufuli jana aliyekuwa mkurugenzi wa jiji la dar ndugu Wilson Kabwe ameibuka na kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake
akiongea mna mwandishi wetu aliyemhoji  bwana Kabwe alikuwa na haya ya kuzungumza..

Mwandishi;Umezipokeaje hizi taarifa za wewe kusimamishwa kazi na Rais baada ya tuhuma zilizotolewa juzi na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndugu Paul makonda?

Kabwe;Mimi sina lolote la kuzungumza kwa sababu maamuzi yamekwishatolewa, ninachosubiri ni uchunguzi ufanywe ili ukweli ubainike.

Mwandishi;Ninachotaka kujua ni wewe unazungumziaje suala hili?

Kabwe;Nimekwishakwambia kwamba sina la kuongea kuhusu hilo na pia sina tatizo lolote na uamuzi huo uchunguzi ufanyike na nina hakika kwamba ukweli utajulikana tu,Kama itabainika nimeonewa je, kuna fidia yoyote ntapewa?

Rais Magufuli: Shinyanga Ina Watumishi Hewa 226.

BOFYA  KUPATA APP YA TANZANIAMPYASASA..BOFYA HAPA

Idadi ya wafanyakazi hewa katika mkoa wa Shinyanga ambao awali ulidaiwa kutokuwa na wafanyakazi hao kabisa, imeongezeka na kufikia 226.

Hayo yamebainishwa leo na Rais John Magufuli katika uzinduzi wa Daraja la Kigamboni, ambapo alisisitiza kuwa serikali yake haitawafumbia macho viongozi ambao kwa namna moja au nyingine wataruhusu mianya ya ubadhirifu wa fedha katika maeneo yao.
 
"Mkoa wa Shinyanga kwa taarifa nilizonazo hadi sasa wameshapatikana wafanyakazi hewa 226 kutoka ‘zero’ hivyo ni lazima tuwajibike kwa watanzania wanyonge” ,amesema Rais Magufuli.

Wakati wa kuwasilisha ripoti ya Mikoa Serikalini aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela alisema mkoa wake hauna mtumishi hewa hata mmoja ,jambo lililosababisha rais Magufuli kuunda tume iliyobaini watumishi hewa 45 katika awamu ya kwanza.

Baada ya kubainika uwepo wa watumishi hao, Rais alitangaza kutengua uteuzi wa Mkuu huyo wa Mkoa kwa kutokuwa makini na taarifa anazopewa na wasaidizi wake. 

Je, una tangazo,habari,picha,makala,Maoni na ushauri wasiliana nasi kupitia,Simu namba 0716528779/0755542721
na Email.titoemmanuel93@gmail.com 

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo April 20 2016 kwenye,Habari zaUdaku, Kitaifa,kimataifa na michezo.

Baraka da prince:Huwa sigongei magari ya wenzangu.

Msanii anayefanya vizuri katika game la bongo fleva Baraka da prince ameweka wazi na kukanusha taarifa zilizovuma kwamba huwa anaazima magari na kutamba nayo mjini.

Lady Jaydee kwenda South Africa kushoot Video ya #Ndi ndi ndi.

Baada ya miaka 10 ya kufanyakazi na muongozaji wa video Justin Campos, Komando Jide au Lady Jaydee amerudi tena kwake kufanyanaye kazi, kutengeneza video ya wimbo wake wa #NdiNdiNdi

Taarifa hiyo ya kufanyakazi na Justin Campos ameitoa Lady Jaydee mwenyewe kwenye ukurasa wake wa Instagram, baada ya kupost video ikimuonyesha Justin Campos akisema ni heshima kwake kufanyakazi na Jaydee ingawa si mara ya kwanza.

“Nilikutana na Justin Campos kwa mara ya kwanza 2006 wakati tunafanya video ya 'Njalo' nilioshirikiana na kundi la Afrika Kusini linalojulikana kama 'Mina Nawe', Justin ndio alikuwa Director wa video hiyo baada ya miaka 10 tumefanyanae kazi tena 2016,” aliandika Jaydee.

Pia Lady Jaydee ameanza kupost picha za video hiyo huku akiandika “#NdiNdiNdi loading Kikomandooooooo #NguvuYaUmma #WananchiWameipokea #NdiNdiNdiMusicVideo”
 

Gallery

Popular Posts

About Us