
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameomba boti za kivita kutoka nchini China ili kusaidia ulinzi katika ukanda wa bahari ya Hindi.
Aliomba boti hizo Dar es Salaam jana wakati alipotembelea boti ya Jeshi la Wanamaji kutoka China waliokuja nchini kwa ziara ya kirafiki wakiwa wametoka kutekeleza jukumu la kushiriki katika ulinzi katika Ghuba ya Aden.
Alisema upatikanaji wa boti hizo utasaidia...