KINGAZI BLOG: 05/29/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, May 29, 2016

JWTZ Washusha Abiria Kwenye Magari yao na Bodaboda ili Washiriki Zoezi la Usafi


KATIKA hali isiyo ya kawaida, askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Mkoani Mtwara jana walisimamisha vyombo vya usafiri barabarani asubuhi na kushusha abiria waliokuwemo, ili washiriki kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi.

Mwandishi alishuhudia abiria wakishushwa katika magari, pikipiki katika maeneo mbalimbali ya mji wa Mtwara na kutakiwa kushiriki zoezi la usafi.
 
Ufanyaji usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi umekosa mwamko mjini Mtwara tangu kuzinduliwa na Rais Desemba 9, mwaka jana.
 
Bila kujali itikadi za vyama wala cheo cha mtu, JWTZ waliwataka wananchi kupaki vyombo vya usafiri na kufanya usafi ili kukabiliana na milipuko ya magonjwa.
 
Baadhi ya wananchi walioshiriki usafi huo, walipongeza jitihada za JWTZ katika kutilia mkazo zoezi la usafi mkoani humo.
 
Zoezi hilo la usafi liliongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego ambaye alisema litakuwa endelevu mkoni hapo.

Magazeti ya Leo Jumapili ya May 29 kwenye habari za kitaifa kimataifa michezo na stori nyingine kali

Jumapili ya leo  Mei 29 naanza kwa kukuletea habari zilizopo kwenye magazeti ya tanzania kama zilivyopewa uzito wa juu kwenye habari za kitaifa kimataifa na mchezo,usisahau kulike page yetu facebook.com/tanzaniampyasasablog na twitter@tanzaniampyasasa



Wanafunzi 7000 UDOM watimuliwa

Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kimewasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi maalumu ya ualimu wa sayansi kwa ngazi ya stashahada na kuwataka waondoke chuoni hapo mara moja.

Jana, lilitolewa tangazo chuoni hapo likiwataka wanafunzi hao kuondoka kati ya jana hadi leo saa 12 jioni. Tangazo hilo lilieleza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo katika ufundishaji wa stashahada hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imeamua wanafunzi hao kurejea majumbani na wataelezwa mustakabali wao “mapema iwezekanavyo”.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula alipotakiwa kufafanua suala hilo, alisema kwa ufupi kuwa suala hilo lipo lakini akaelekeza apigiwe simu Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Beatrice Baltazal kwa maelezo zaidi.

Baltazal alipotafutwa alisema kusimamishwa kwa wanafunzi hao kulitokana na agizo la Serikali na wametakiwa kulitekeleza.

Kuhusu lini na nini hatima ya wanafunzi hao, alisema bado hawajui hadi hapo watakapoelekezwa vinginevyo.

Hata hivyo, kulikuwa na malalamiko kwa wanafunzi hao juu ya namna walivyopewa taarifa za kusimamishwa masomo yao kwa ghafla na kutakiwa kuondoka.

Kozi ya stashahada ya ualimu wa sayansi, ilianzishwa maalumu kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete kwa lengo la kuziba pengo la walimu wa sayansi na ilikuwa inatolewa UDOM pekee.

Waliokuwa na sifa za kujiunga na kupewa mikopo ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kufaulu vizuri masomo ya sayansi. 

Wanafunzi hao waliokuwa wamekopeshwa na Serikali wamesimamishwa siku mbili baada ya wenzao zaidi ya 480 wa Chuo Kikuu cha St. Joseph kusimamishwa baada ya kubainika hawakuwa na sifa za kudahiliwa.

 

Gallery

Popular Posts

About Us