KINGAZI BLOG: 08/11/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, August 11, 2016

Mtoto wa OBAMA arekodiwa Akivuta Bangi

Mtoto mkubwa wa Rais Barack Obama – Malia Obama – anahisiwa siku kadhaa nyuma alikuwa amepewa kipisi cha bangi kuvuta na akavuta na kujikuta akirekodiwa na video za mapaparazi wa Marekani. Tukio hilo limekuja siku chache tu baada ya video nyingine kumuonesha binti huyo akikata viuno kwenye moja ya matamasha ya muziki huko Marekani.

Inasadikiwa Malia alivuta sigara hiyo ‘haramu’ kwenye tamasha la lollapalooza kwenye Jiji la Chicago, jimbo la Illinois ambalo ni jimbo la nyumbani kwa Rais Obama. Mmoja wa wahudhuriaji wa tamasha hilo Jerrdin Selwyn mwenye umri wa miaka 18 alidai kuwa alimkuta Malia akiwa anavuta ganja na marafiki zake na hakukuwa na shaka ya hilo kwani harufu ya bangi ilikuwa wazi
“Kulikuwa na kijana mmoja pale ambaye alikuwa anavuta na akampasia Malia ambaye alishikilia kama kwa dakika moja kisha akampatia mtu mwingine” alidai binti huyo. Na alidai pia kuwa alikuwa na picha zinazoonesha mtoto huyo wa Rais wa Marekani akivuta bangi hiyo

SNURA:WANAUME WANANISUMBUA SANA.

Msanii wa muziki Snura Mushi alimaarufu kama Snura Majanga amefunguka na kusema kuwa amekuwa akipata shida sana na wanaume mbalimbali wenye matamanio kutokana na vile anavyoweza kutumia mwili wake kwenye uchezaji wake akiwa stejini.

Snura alizungumza haya kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kuwa licha ya kupata usumbufu huo kwa wanaume hao lakini amekuwa akijitunza na kujiheshimu kwani anafanya hivyo kulinda kazi yake na heshima yake kama mwanamke.

"Unajua watu wakisikia Snura Chura huwa wanatokea wengi sana, na kweli huwa napata shida sana kwa wanaume wengi wenye matamanio, na inawezekana kweli kati yao wapo wenye mapenzi ya kweli na mimi lakini ndiyo hivyo, kitu nachozingatia sana ni kuilinda kazi yangu, hivyo wanapotokea wanaume wa namna hii mimi nachokifanya siku zote ni kuwa mbali nao kabisa ndiyo maana nashinda vishawishi hivyo kila siku" alisema Snura

KESI YA MTUHUMIWA ALIYEKUWA AKIIBIA SERIKALI MILIONI 7 KWA DAKIKA YAAHIRISHWA


Washtakiwa, Mohamed Yusufali “Choma” na Samwel Lema wakizungumza na wakili wao mara baada ya kesi hiyo kuhiishwa.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeahirisha kesi inayomkabili mfanyabiashaa Mohamed Mustapha na mwenzake wanaodaiwa kuiibia serikali shilingi milioni saba kwa kila dakika, kesi hiyo imetajwa kusikilizwa tena Agosti 18, 2016 huku watuhumiwa wakirudishwa rumande.


Hakimu aliyekuwa akisoma shauri la kesi hiyo, Wilbard Mashauri amesema watuhumiwa hawawezi kupewa dhamana na mahakama hiyo kwa kuwa haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa watuhumiwa wa kesi hiyo.



Wafanyabiashara Mohamed Yusufali “Choma”, na mwenzake Samwel Lema ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Northern Engineering Works Limited wakikabiliwa na mashitaka 222 ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 14.


Baadhi ya ndugu, jamaa, marafiki na wanahabari waliofika kuhudhuria kesi hiyo.

Washtakiwa wanadaiwa kujipatia pesa hizo kwa njia ya udanganyifu katika mapato ya serikali, , Samwel Lema, ambao wanadaiwa kusababisha hasara kwa kughushi na kukwepa kulipa kodi.

Watuhumiwa wakitoka kotini.

Donald Trump alaumu wanahabari kufuatia utata kuhusu bunduki

Donald Trump amewalaumu waandishi wa habari baada yake kushutumiwa kwa matamshi yake ambapo alidaiwa kuwahimiza wafuasi wake wamuue mpinzani wake Hillary Clinton wa chama cha Democratic.

Alikuwa amewaambia wafuasi wake kuwa wanaweza kumzuia hasimu wake Bi Clinton kwa kutekeleza haki zao za silaha.

Alisema Bi Clinton anaweza kupeleka haki zake huria za kisheria mbele ya Mahakama ya Juu kama atashinda urais mwezi Novemba, na kufuta haki ya raia kumiliki silaha.

Akihutubia mkutano wa kisiasa katika jimbo la North Carolina, Bw Trump alidokeza kuwa haki za umiliki wa silaha zinaweza kusaidia kumzuia Bi Clinton kuchukua mamlaka.

Kauli yake hiyo imezua hasira kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakimshutumu kwa kuchochea ghasia.

Lakini muda mfupi baadaye alijitetea na kusema kuwa alikuwa tu anawataka wanaounga mkono haki za umiliki wa silaha kupiga kura kwa wingi.

Baadaye alisema wanahabari wa shirika la habari la Fox News walipinda matamshi yake na kuyafanya yaonekane kana kwamba alikuwa anawahimiza wafuasi wake wenye silaha wazitumie kumuangamiza Bi Clinton.

Hii si mara ya kwanza kwa Bw Trump kulazimika kukosoa kauli zake.

1. Kumbeza mlemavu
Aliwahi kukanusha kumbeza mwandishi wa habari mlemavu wa gazeti la New York Times Bw Trump alilegeza mikono yake alipokua akielezea makala kuhusu mashambulizi ya 9/11 iliyoandikwa na Serge Kovaleski, ambae ana ulemavu wa mikono. Hata hivyo mwanasiasa huyo alisistiza kuwa hakujua ripota huyo anafanana vipi na kwamba anawaheshimu watu wenye ulemavu.

2. Iran kulipwa pesa
Donald Trump aliwahi kufafanua baada ya awali kudai kuwa aliona mkanda wa video wa malipo ya pesa ya Marekani kwa Iran. Alitoa madai hayo kwenye mkutano wa kisiasa. Trump alisema malipo yalikua na uhusiano na Iran kukubali mapatano ya nyuklia

3. Wanawake kutoa mimba
Donald Trump alifuta kauli yake ya awali ambapo alisema wanawake waliotoa mimba waadhibiwe saa chache tu baada ya kutoa pendekezo hilo. Alipendekeza kuwa "aina fulani ya adhabu " itolewe kwa wanawake waliotoa mimba kama zitakuwa kinyume cha sheria. Lakini baada ya ukosoaji mkubwa , Bw Trump akarejelea msimamo wa chama cha Republican kwamba mtu anaefanya kitendo cha utoaji mimba anapaswa kuadhibiwa, si mwanamke pekee.

4. Kudukuliwa kwa Clinton
Donald Trump alisema alitumia tu lugha ya mzaha alipokowaalika warusi wadukue jumbe za Bi Hillary Clinton zilizopotea. Aliikiambia kituo cha televisheni cha Fox News kwamba chama cha Democrat kilikua tu kinatumia mzozo huo kukwepa masuala makuu. Kauli zake zilikua kuhusu jumbe 30,000 za barua pepe za Bi Clinton ambazo hakuziwasilisha kama sehemu ya uchunguzi kuhusu jumbe za siri. "nilikua najaribu kuwa mzushi tu," Bw Trump alikiambia kituo cha Fox News.

Mwenyekiti wa kijiji auawa kwa, kuchinjwa kama kuku MVOMERO.


Imetokea Morogoro Wilaya ya MVOMERO kijiji cha MAFURU kitongoji cha KIDIWA mwenyekiti wa kitongoji kwa jina GODFREY MPEKA  ameuawa kikatili na watu wanao sadikika kuwa ni wajamii ya wafugaji Mpaka mchana wa Tarehe 9 Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi na Afisa usalama wa Wilaya walikuwa katika eneo la tukio wakiwatafuta wauaji hao.

Mauaji hayo yametokea Mara Tu baada ya mwenyekiti kuwakamata ngombe walio kuwa wame ingizwa kwenye shamba la wanakijiji ndipo wafugaji walipo mkamata mwenye kiti na kumchinja kama kuku.

Angalia Video kisha usisahau Kubofya Subscribers hapo chini ya YouTube..





MSANII DIAMOND PLATNUMZ ATOA MSAADA WA TSH. MIL 20 KWA TAASISI YA UPASUAJI/MATIBABU YA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA.

Msanii wa muziki Diamond Platnumz ametoa msaada wa tsh 20 Milioni kwa ‘GSM Foundation’ kwa ajili ya kusaidia jitihada za taasisi hiyo ya kutoa huduma ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Timu ya Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikishirikiana na GSM Foundation imekuwa ikizunguka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma hiyo bila gharama yoyote.

Raisi huyo wa label ya ‘WCB’ ameonyesha kughuswa na jitihada za taasisi hiyo na kuamua kuchangili kiasi hicho.

“Moyo wangu unaniambia nisingeshikwa mkono ama kusaidiwa na watu basi nami nisingeweza leo hii kufikia hatua hii ndogo niliofikia na ndio maana kidogo nikipatacho huwa napenda kusaidia wenzangu,” aliandika Diamond Istagram. “Leo Mapema nilitembelea ofisi za GSM foundation kuwasilisha kidogo tulichobarikiwa kwa niaba ya WCB. kwajili ya kusaidia watoto wenye matatizo ya Vichwa vikubwa (Bobble Head Syndrome) na Mgongo wazi,”

Kwa upande wa GSM Foundation, ameandika:Leo tumepokea hundi ya shilingi milioni ishirini (20,000,000/=) kutoka kwa @diamondplatnumz kama mchango wake kwa #GSMFoundation. Tunamshukuru kwa kuja kututembelea ofisini kwetu na kwa msaada aliotupatia. Mwenyezi Mungu amuongezee pale alipopunguza.

ZITTO KABWE AMVAA TUNDU LISSU.... AIBUA MADUDU YAKE


*BY ZITTO KABWE*
"Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini. Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa. Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?
Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda.
Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.
They must know I am not a push over. Chacha died, I won't.
Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili."

Habari kubwa kwenye Magazeti ya Leo Alhamisi ya Agosti 11 kwenye headlines za kitaifa kimataifa michezo na udaku



 

Gallery

Popular Posts

About Us