KINGAZI BLOG: 09/10/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, September 10, 2016

Mtangazaji wa Clouds Tv ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya

Leo Septemba 10, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.

Miongoni mwa Wakurugenzi wa Halmashauri walioteuliwa, yumo pia mtangazaji wa kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv kinachorushwa kila siku kuanzia jumatatu hadi Ijumaa.

Hudson Stanley Kamoga ameteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.

Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuteua watangazaji kushika nyadhifa mbalimbali kwani alimteua aliyekuwa Mtangazaji wa ITV, Godwin Gondwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.

Wakurugenzi wengine walioteuliwa leo ni pamoja na;-

Mwailwa Smith Pangani – Halmashauri ya Wilaya ya NsimboGodfrey Sanga – Halmashauri ya Wilaya ya MkalamaYusuf Daudi Semuguruka – Halmashauri ya Wilaya ya UlangaBakari Kasinyo Mohamed – Halmashauri ya Wilaya ya NachingweaJuma Ally Mnwele – Halmashauri ya Wilaya ya KibondoButamo Nuru Ndalahwa – Halmashauri ya Wilaya ya MoshiWaziri Mourice – Halmashauri ya Wilaya ya KaratuFatma Omar Latu    – Halmashauri ya Wilaya ya BagamoyoGodwin Emmanuel Kunambi – Manispaa ya DodomaElias R. Ntiruhungwa – Mji wa TarimeMwantumu Dau – Halmashauri ya Wilaya ya BukobaFrank Bahati – Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe

Ruby aamua kumjibu Diva baada ya kudai kuwa hamfahamu....... "Ampa makavu live"

Muimbaji wa ‘Na Yule’ Ruby amefunguka baada ya mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Diva kudai kuwa hamfahamu msanii huyo.

Ruby ameiambia Bongo5 kuwa kauli aliyoitoa mtangazaji huyo anaiona ni kama utoto. “Naona ni ujinga, I don’t want to talk about it, naona ni utoto sidhani kama ninaweza kuliongelea hilo.”

“Everybody knows me, so nahisi huo ni utoto tu labda wa kukosa majibu kwenye maswali ya interview aliyohojiwa. I don’t to talk about her,” ameongeza.

Pia Ruby amedai kuwa licha ya kuzinguana na uongozi wa THT, bado mambo yanaenda mswano.

“Kutokuwa na mawasiliano mazuri na uongozi wangu wa zamani sijaathirika kwakweli, sitaki kuliongelea hilo kwa sababu mimi naona kwangu ni kitu ambacho kimeshapita nataka niongelee vitu ambavyo vinaendelea mbele. Sidhani kama nina tofauti na wao mimi sijui ila, I don’t talk about them, at all.”

Inawezekana Diva alitoa kauli hiyo kutokana na Ruby kutokuwa na mawasiliano mazuri na Clouds Media baada ya kushindwa kuhudhuria kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika Mwanza, August 20 ya mwaka huu.

Shilole adai ilikuwa si rahisi kufanya scene na raymond kwa "NATAFUTA KIKI".


Msanii wa muziki wa bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kusema ilikuwa ni jambo gumu kwake kufanya video ya ‘Natafuta kiki’ ya msanii Raymond.
Msanii Raymond akiwa na Shilole wakati wa utengenezaji wa video ya ‘Natafuta kiki’
Amesema ugumu huo ni kutokana na ukweli kwamba ‘scene’ ambazo alipaswa kucheza zilikuwa ngumu kwake jambo ambalo lilimfanya atumie kwanza kilevi kuondoa aibu.
Shilole alisema hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV na kudai alikuwa anashindwa kufanya mambo kwenye video hiyo kutokana na vile anavyomuheshimu Raymond kama mdogo wake.
“Mimi niliweka upendo na kuona nimsaidie mdogo wangu Raymond katika kazi yake ili iweze kutazamwa na watu wengi zaidi, ila kiukweli ilikuwa ni kazi mbaya sana kwangu na ngumu lakini nikaona maji nishayavulia nguo hivyo sina budi kuyaoga, nikamwambia Raymond wewe ni mdogo wangu sasa naanzaje kufanya haya mambo? Ilikuwa ni ngumu ikanibidi ninywe pombe kidogo ili niweze kuchangamka, kwani watu walikuwepo wengi nikawa naona aibu. Akaniambia hamna usijali hii kazi tu nisaidie tu, ikabidi nivae ile night dress na kuingia kazini” alisema Shilole.
Mbali na hilo Shilole alisema kuwa amekuwa akitumika kwenye baadhi ya video mbalimbali kutokana na wasanii hao kumuomba ashiriki kwenye video zao ili kuwasaidia video zao kuangaliwa na watu wengi zaidi.
“Nilifanya video ya Man Fongo haina ushemeji, video ya Darasa ‘Too much’ hii ya Raymond ‘Natafuta kiki’ na ile ya Dully Skyes na Harmonize ‘Inde’ wao wamekuwa wakiniomba na kusema uwepo wangu kwenye video zao unaleta ‘impact’ kwa watu kwani watu wanakuwa wanazitazama sana video zao hivyo mimi naamua kuwapa ‘support’.

 

Gallery

Popular Posts

About Us