KINGAZI BLOG: 06/02/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, June 02, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA MAKTABA MPYA YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandala, Balozi wa China hapa nchini lu you Qing, maafisa wa kampuni ya Kutoka China ya Jiangsu Jiangdu wakiweka mchanga kama ishara ya kuweka jiwe la msingi katika Maktaba Mpya ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam UD mara baada ya kuwasili chuoni hapo. Maktaba hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandala, Balozi wa China hapa nchini lu you Qing, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na makamu wa Rais katika serikali ya awamu ya nne Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Spika Mstaafu Pius Msekwa mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maktaba hiyo ya kisasa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini katika Kitabu maalum cha Kampuni ya Jiangsu Jiangdu construction group inayojenga Maktaba Mpya ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam UD mara baada ya kuwasili chuoni hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Balozi wa China hapa nchini lu youQing kabla ya kwenda kuzungumza na jamii ya  wanachuo kikuu cha Dar es Salaam.

Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala akitoa maelezo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   kuhusu ujenzi wa Maktaba hiyo ya kisasa itakayochukua wanafunzi zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja. Wengine katika picha ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Wziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akipita kwenye mabango ya picha za mfano wa majengo ya Maktaba mpya itakayojengwa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya jamii ya  wanachuo na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maktaba mpya itakayochukua zaidi ya wanafunzi 2000 kwa wakati mmoja.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli machapisho ya tafiti mbalimbali za madini na mambo mbalimbali ya kimaendeleo zilizofanywa na wahadhiri wa chuo hicho mara baada ya kuwahutubia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha machapisho hayo. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya Wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kumaliza kuwahutubia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba mara baada ya kumaliza mkutano huo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Mlimani jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Nikki Wa Pili Ft. ChinBees - Role Model(AUDIO)



QUICK ROCKA,G-NACKO & JUX - HAPO(AUDIO)


VIDEO: Rich Mavoko rasmi WCB, kasainishwa rasmi leo June 2 2016


June 2, 2016 label ya Wasafi inayomilikiwa na staa Diamond Platnumz inaingia kwenye headlines za Bongo Fleva baada ya kumtambulisha rasmi  msanii  wao mpya  Rich Mavoko ambaye anakuwa ni msanii wa nne atakayesimamiwa kazi zake katika label hiyo.
Kwa mujibu wa Diamond Platnumz amesema…Kwasasa Label yangu inakuwa na jumla ya wasanii wanne ukiachana na Rich Mavoko kuna Dada yangu Queen Darling ambaye sijawahi kumtambulisha lakini anakuwa ni msichana wa kwanza katika label yangu kwahiyo tutakuwa na Raymond, Harmonize, Rich Mavoko na Queen Darling
Unaweza kuangalia video hii hapa chini

PICHA ZA WOLPER WA HARMONIZE ANAVYOJIACHIA UKWENI


Leo ni siku ya tatu kuanzia Harmonize na mpenzi wake Wolper waanze kuposti picha wakiwa  mtwara kwa wazazi wa harmonize.

I am having the best time of my life.. Nikiwa na Mama angu... Kabla hamjatoka lazima mpige story, akuchekeshe... Mjipikilishe.. Akushauri 

Hapa nimepata rafiki kwa kweli...

I love my mama Mkwe.. Mama Raj wangu

kupitia ukurasa wake wa IG  Wolper amepost picha akiwa anafurahia kuwa karibu na mama mkwe na kushare nae mambo tofauti katika maisha ya mtwara, nimekuwekea hizi picha pamoja na maneno yaliyoambatana na picha hizo kutoka mtwara life.

Nalipenda jiko nanaliweza #ukweni👌

Mtu na wifi yake my Amina

Jiko bila umbea aliivishi wifi & I Mood

Mkwe kwa mbali👌

Bibi kanifanya nacheka kwanzia mwanzo wa pishi paka mwisho jamani Nina Amani moyoni syo kwa mahaba haya yenye mizizi sugu ukizingatia huyu ndo yule Bibi aliyemfundisha Raj mapenzi nakumsisitizia mwanamke apigwi nangumi ila niupande wakanga basi mwezenu taabani syo makosa yangu nimakosa ya unyago wakimakonde

WAFAHAMU MASTAA 12 AMBAO WANAONGOZA KWA KUMWAGANA NA WAPENZI WAO!




Wema Sepetu na Diamond
KATI ya kundi la watu wanaoongoza kwa kumwagana katika uhusiano wa mapenzi ni mastaa, lakini kwa nyakati tofauti baadhi ya mastaa waliotengana huishia kuingia kwenye uhusiano thabiti na wapenzi wengine hadi kuoana huku zilipendwa wao wakiishia kuyumba kimapenzi au kutokuwa na mpenzi wa kudumu kiasi kwamba unaweza kuitafsiri hali iyo kwa kutumia usemi wa huku sawa, kule majanga.
Wafuatao ni baadhi ya mastaa waliopitia kasumba hiyo:Katika historia ya wapendanao kwa mastaa, hawa wanaweza wakawa ndiyo kapo pekee iliyojizolea mashabiki lukuki Bongo kabla ya kumwagana kwao, lakini kwa sasa kila mtu akiwa na zake, ambapo Diamond ametulizwa na penzi la mwanamama Zarinah Hassan, ‘Zari’ na tayari uhusiano wao umejibu kwa kuzaa mtoto huku zilipendwa wake, Wema Sepetu akiwa ni majanga kwa kuwa tangu amwagane na Diamond hajatulia katika uhusiano rasmi. 

Kanye West na Amber Rose
Enzi za mapenzi yao wawili hawa walitengeneza vichwa vya habari na kuwavutia watu wengi waliowafuatilia, lakini kama uhusiano mwingine mapenzi yao yaliishia ukingoni na kila mtu akachukua zake ambapo Kanye alinasa kwa Kim Kardashian na kuishia kuoana na kuzaa mtoto huku mapenzi yao yakizidi kushamiri kila siku tofauti na upande wa Amber Rose ambaye alijaribu kutulia na ‘mbishi’ Wizy Khalifa lakini mwishowe akaambulia kibuti na kubaki akitangatanga. 

Janet Jackson na Jermaine Dupri
Umaarufu wa mapenzi ya wawili hawa ulikuwa gumzo nchini, Marekani kutokana na mwanadada huyo kutokea kwenye familia maarufu ya muziki iliyotambulishwa na bendi ya Jackson Five ambayo Michael Jackson alitokea huku Jermaine Dupri kwa upande wake akiwa prodyuza mkali wa muziki enzi hizo.
Baada ya kumwagana, Janet ameolewa na bilionea wa Kiarabu kutoka Qatar, Wissam Al Mana huku majanga yakiwa kwa Jermaine ambaye mpaka sasa haeleweki anatoka na nani. 

Ben Affleck na J.Lo
Mapenzi kati ya diva wa muziki Jennifer Lopez na mwigizaji Ben Affleck yalikuwa yenye mvuto wa kipekee nchini Marekani, lakini kama wengine nao walimwagana kiroho mbaya huku Ben Affleck akimuoa mwanadada Jeniffer Garner na kuzaa naye watoto huku J.Lo akiwa haeleweki baada ya awali kudhaniwa atatulizwa na mkali wa muziki wa hisia, Mark Antony, lakini ilishindikana kwa mwanadada huyo kutoka na bitozi Casper Smart kabla ya kumwagana. 

IYOBO NA MWENGI
Huyu ni dansa maarufu wa nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye aliwahi kutoka na mdada wa mjini, Mwengi na kuzaa naye mtoto, lakini mwishoni wakatengana kwa ugomvi baada ya Mose kuangukia kwa msanii wa muvi, Aunt Ezekiel na hatimaye kupata mtoto. Wakati huo hadi sasa Mwengi hajaweka wazi uhusiano wake jambo linaloonesha kuwa bado majanga kwa upande wake.

JACK PATRICK NA JUX 
Mwanzoni walificha mapenzi yao, lakini baadaye wenyewe wakayaweka wazi mapenzi yao kabla ya kutengana baada ya Jack kuswekwa jela nchini China. Jux ameangukia kwenye penzi la diva wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee huku mambo kwa Jack ambaye bado yupo gerezani yakiwa magumu baada ya awali kutwangwa talaka akiwa gerezani na aliyekuwa mumewe, Fundikira. Hadi sasa hana mpenzi anayejulikana wazi kiasi cha kuonekana kama mkiwa

JK: Nchi za Afrika Haziwezi Kukwepa Misaada ya Wazungu


Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema nchi za Afrika haziwezi kukwepa misaada kutoka nchi za Ulaya kwa kuwa misaada hiyo ni jukumu lao la kihistoria.

Kikwete alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaojadili malengo mapya 17 ya Umoja wa Mataifa yanayohusu ‘Maendeleo Endelevu kwa mwaka 2030’.

Mkutano huo umejikita kujadili lengo namba 16 linalohimiza haki, amani na jamii shirikishi, hasa katika masuala ya utawala wa sheria kama chachu ya maendeleo endelevu.

Kikwete alisema jukumu hilo linapaswa kuendelezwa kwa kuwa maendeleo ya nchi za Ulaya yalitokana na rasilimali walizozitoa Afrika kipindi cha ukoloni.

Alisema nchi za Afrika zina rasilimali za kutosha hivyo, ili zifanye kazi bado kunahitajika uwekezaji ambao utaweza kuinua viwanda na kukuza uchumi wa nchi za Afrika, kwani bila hivyo itachukua muda mrefu kufika mbali kiuchumi.

Hata hivyo, alisema nchi za Afrika lazima zijiwekee utaratibu wa namna ya kupokea misaada hiyo, lakini lengo liwe ni kunufaisha wazawa na kwa kufuata sheria za nchi husika na zile za kimataifa.

“Misaada tunayoizungumzia siyo lazima iwe fedha, bali tunahitaji wawekeze zaidi kwetu kwa mikataba ya kisheria inayolinda wazawa, kwa mfano Tanzania tuna rasilimali za kutosha kama gesi, madini na vinginevyo, lakini hivi vyote vinahitaji kuibuliwa na kutayarishwa. Lazima tuwape nafasi ili kufanikisha lakini kwa sheria zitakazowalinda Watanzania,”alisema Kikwete.

Kauli hiyo ya Kikwete imekuja wakati Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli amekwisha kuweka msimamo katika hotuba zake kadhaa akitaka Tanzania ijitegemee kwa asilimia kubwa badala ya kutegemea misaada ya nje.

Wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kwanza ya juu (flyover) katika makutano ya Barabara za Mandela na Nyerere eneo la Tazara, Rais Magufuli aliita misaada ya wahisani ‘mkate wa masimango’ na kusema kuliko kula mkate huo ni bora kushindia muhogo.

Ingawa hakufafanua wala kuzungumza kwa undani juu ya kauli hiyo, lakini aliitoa ikiwa zimepita siku chache tangu Shirika la Maendeleo la Milenia (MCC) la Mareka ni kusitisha msaada wa Dola za Marekani milioni 472.8 karibu Sh1 trilioni kwa madai kuwa Tanzania ilikiuka misingi ya kidemokrasia kwa kurudia uchaguzi wa Zanzibar na kushindwa kusimamia She ria ya Makosa ya Mtandao.

Pia, Rais Magufuli Machi 29, akiwa katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato mkoani Geita alisema jukumu kubwa lililo mbele ya Watanzania kwa sasa ni kushikamana na kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja ahakikishe anaongeza uzalishaji na utendaji kazi mahali pake pa kazi.

“Kwa hiyo ni lazima tujisimamie sisi wenyewe, na tukijisimama sisi wenyewe kwa kila mmoja kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi afanye kazi kwelikweli, kama ni mkulima afanye ukulima wake kwelikweli, kama ni mfanyabiashara afanye biashara kwelikweli, kama ni mfugaji afuge kwelikweli, kama ni mvuvi avue kwelikweli, Tanzania hii tutavuka,”alisema.

Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Sheria (IDLO) yenye makao makuu yake nchini Italia, ambayo kwa Tanzania mlezi wake ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkapa alisema katika nchi yeyote ili kupata maendeleo ni lazima kuwe na Katiba ya wananchi ambayo haitalenga kundi moja.

“Awali nchi nyingi za Afrika hazikuwa na Katiba ya wananchi, bali kulikuwa na Katiba ya chama ambayo kwa sasa ni nchi za kidikteta pekee zimebaki na mfumo huo, kwa sasa tulilenga kuweka sera, mikakati thabiti ili tuweze kutekeleza malengo mapya ya dunia chini ya dira mpya ya Umoja wa mataifa ya maendeleo ya dunia,” alisema Mkapa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki alisema kama ilivyo ajenda ya nchi za Afrika, nchi haiwezi kuwa na utawala wa sheria kama hakuna upatikanaji mzuri wa sheria.

“Lazima uweke mifumo mizuri ya kutatua migogoro pia, utoaji wa vibali bila kutoa rushwa, hata katika uwekezaji utakapokuwa huna sheria nzuri inayolinda upande huo ni vigumu wawekezaji kuwepo,” alisema Kairuki.

Mkurugenzi Mkuu wa IDLO, Irene Khan alisema mkutano huo umejikita katika kujadili haki, amani na jamii shirikishi.

“Lengo ni kuwa na dira mpya ya maendeleo ya dunia inayolenga kutokomeza umaskini, kulinda mazingira, kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kushirikisha makundi yote kwenye jamii katika masuala ya maendeleo,” alisema Khan.


Wapinzani Wawasilisha Hoja ya Kumwondoa Madarakani Naibu Spika, Dr Tulia Ackson

Wabunge wa upinzani wamewasilisha kwa Spika wa Bunge hoja ya kumwondoa madarakani Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa kutokuwa na imani naye.

Hatua hiyo imefikiwa na wabunge hao kufuatia kutoridhishwa na mwenendo wa uongozi wa Dk Tulia anapokalia kiti cha Spika.

Tangu Jumanne wiki hii, wabunge hao wamekuwa wakisusa vikao vinavyoongozwa na kiongozi huyo kwa madai anaminya demokrasia.

Walifikia uamuzi huo baada ya Dk Tulia kuzuia kujadiliwa hoja ya kufukuzwa kwa wanafunzi zaidi ya 7,000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) iliyowasilishwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na kukatisha mjadala wa bajeti ya maji.

Kitendo hicho kiliwafanya wabunge wote wa upinzani kupingana na maamuzi ya Dk Tulia, jambo lililosababisha watolewe bungeni.

Kutokana na hali hiyo wabunge hao kupitia Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya akisindikizwa na Mbunge wa Kibamba, John Myika wa Chadema na Mbunge wa Konde wa CUF, Khatibu Said Haji waliwasilisha hoja hiyo kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah baada ya Spika, Job Ndugai kutokuwapo bungeni.

Hoja hiyo iliwasilishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 138 (1) ambayo inaeleza utaratibu wa jinsi ya kumwondoa Naibu Spika.

Kanuni hiyo inasema, “Utaratibu wa kumwondoa Naibu Spika madarakani chini ya Ibara ya 85(4)(c) ya Katiba utakuwa kama ule wa kumwondoa Spika, isipokuwa tu taarifa ya kusudio la kumwondoa Naibu Spika madarakani inayoeleza sababu kamili za kuleta hoja hiyo, itapelekwa kwa Spika ambaye ataiwasilisha kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kuijadili.”

Fasili ya pili ya Kanuni hiyo inasema: “Endapo Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itaridhika kuwa zipo tuhuma mahususi dhidi ya Naibu Spika zinazohusu uvunjaji wa Katiba, Sheria au Kanuni zinazoongoza Shughuli za Bunge, basi Kamati hiyo itaidhinisha kuwa hoja hiyo ipelekwe bungeni ili iamuliwe.”

Kwa mujibu wa Ibara ya 85(4)(c), Naibu Spika atakoma kuwa Naibu Spika na ataacha kiti cha Naibu Spika endapo ataondolewa kwenye madaraka ya Naibu Spika kwa azimio la Bunge.

Akizungumzia uwasilishwaji wa hoja hiyo, Millya alisema taarifa zaidi watatoa leo kuhusu msimamo wao huo.

Dk Tulia aliwataka wabunge wenye malalamiko juu ya utaratibu wa uendeshaji wa shughuli za Bunge kukata rufaa kwa kufuata Kanuni za Bunge.

Alisema kanuni ndogo ya 5(2) inasema Spika atawajibika kutilia nguvu kanuni zote za Bunge na 5(3) inasema Spika anaweza kumtaka mbunge yeyote anayekiuka kanuni hizi kujirekebisha mara moja.

Alisema kwa hiyo mbunge yoyote asiyeridhika, kanuni za Bunge zinamruhusu kukata rufaa na zinamweleza nini cha kufanya.

Serikali Kuendelea kukosa mabilioni ya msaada toka USAID


Serikali itakosa mchango wa dawa zenye thamani ya Dola 375 milioni za Marekani (Sh787 bilioni), ambazo zimekuwa zikichangwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

USAID ilitoa mchango huo chini ya mradi wa kutunza na kugawanya dawa hasa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV) kwa kipindi cha miaka 10 nchini.

Mradi huo ambao pia umeisaidia Serikali kujenga maghala ya kuhifadhia dawa umefikia mwisho.

Hata hivyo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya alisema licha ya mradi huo kufikia ukomo na kuwa na msaada, wizara imejipanga kuhakikisha kuna uhakika wa upatikanaji wa dawa nchini.

Dk Ulisubisya alisema hata bajeti ya mwaka 2016/17 ya Wizara ya Afya imetoa kipaumbele kwenye dawa.

“Tunataka kuhakikisha Watanzania wanafikiwa na huduma ya dawa kote nchini,” alisema.

Dk Ulisubisya alisema kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, USAID ilitekeleza mradi huo na wananchi zaidi ya 8,000 wamefikiwa na kupata huduma ya dawa.

Alisema wakati mradi huo unaanza watu waliokuwa wanatapa dawa hasa za ARV walikuwa wachache.

Dk Ulisubisya alisema shirika hilo pia lilisaidia kuweka mfumo wa kisasa wa kielektroniki wa kufuatilia matumizi na mahali dawa zinapopatikana.

Kaimu Mkurugenzi Afya wa USAID nchini, Janeane Dauis alisema mradi huo umekuwa na mafanikio nchini.

Dauis alisema shirika hilo litaendeleza ushirikiano wake na Serikali ya Tanzania ili kuweka msukumo zaidi wa kuboresha sekta ya afya nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu alisema mbali na kupata msaada wa kujengewa maghala na USAID, wako kwenye mkakati wa kujenga maghala yao ya kuhifadhi dawa.

Bwanakunu alisema shirika hilo lilitoa Dola 14.2 milioni za Marekani (Sh29.8 bilioni) kwa ajili ya ujenzi wa maghala.

Mkurugenzi huyo alisema MSD inatarajia kujenga maghala yake.Alitaja maeneo wanayotarajia kujenga maghala hayo kuwa ni Dar es Salaam eneo la Buguruni, Mtwara na Moshi.

Pia, alisema MSD inaendelea kupanua wigo wake katika mikoa mbalimbali ukiwamo Iringa.

Haya hapa Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 2 kwenye habari za kitaifa kimataifa,na michezo





Wabunge 7 wa Upinzani Waliosimamishwa Kuhudhuria Bungeni Waongezewa Adhabu nyingine

Wabunge saba wa upinzani waliosimamishwa bungeni, watakumbana na kibano kingine cha kukatwa mshahara na posho kwa kipindi chote cha kutumikia adhabu.

Wabunge hao ambao Jumatatu walisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda tofauti kwa madai ya kukiuka kanuni ni Zitto Kabwe (Kigoma Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Godbless Lema (Arusha Mjini).

Adhabu hiyo ilitolewa  kama azimio la Bunge baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kupendekeza wabunge hao waadhibiwe kutokana na kuomba mwongozo wa kiti cha Spika kwa jambo ambalo tayari lilishatolewa uamuzi.

Habari zilizopatikana bungeni zilieleza kuwa wabunge hao watakumbana na Kanuni ya Bunge ya 75, ambayo inahusika na masharti ya mbunge aliyesimamishwa kazi.

Naibu Katibu wa Bunge (Shughuli za Bunge), John Joel alithibitisha kuwa utekelezwaji wa kanuni hiyo utafuatwa kwa wabunge wote ambao wamefukuzwa.

Akizungumzia hatua hiyo, Heche alisema hadi sasa hajapata barua ya kusimamishwa Bunge, hivyo hata kama watakata posho au mshahara haimsumbui kwa kuwa hawezi kusikitikia kitu hicho wakati haki inaminywa.

Zitto alisema hajasikia taarifa hizo za kukatwa mshahara kwa kuwa hajapewa barua inayoeleza mambo hayo wala ya kusimamishwa Bunge.

Serikali Yazidiwa Mzigo wa Vijana Wanaotakiwa Kujiunga JKT ......Waziri Asema ni Vigumu Kuwachukua Vijana Wote Kutokana na Uhaba wa Fedha


VIJANA wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa mujibu wa sheria wamekuwa wengi kiasi cha kuifanya Serikali kushindwa kuwachukua wote, Bunge limeelezwa.

Hivyo, kutokana na sababu hiyo, Serikali imeamua kuongeza idadi ya kambi za mafunzo ili wachukuliwe wote. Hayo yalisemwa bungeni jana mjini hapa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Munira Mustafa Khatib (CCM) aliyetaka kufahamu ni kwa nini Serikali isianzishe mpango maalumu wa kuwapeleka JKT vijana wanaomaliza kidato cha nne.

Akijibu swali hilo, Waziri Mwinyi alisema, “Uwezo wa JKT kwa sasa kuchukua vijana wa kujitolea ni kati ya vijana 5,000 hadi 7,000 kwa mwaka kutokana na bajeti inayotolewa. 

Alisema, utaratibu wa sasa wa vijana kujiunga na JKT ni ule wa kujitolea kwa vijana wenye elimu ya kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu na ule wa mujibu wa sheria unaowahusu waliomaliza kidato cha sita.

“Kuwachukua vijana wote wanaomaliza kidato cha nne kama anavyoshauri mbunge hautowezekana kutokana na uwezo mdogo kifedha,” alisema. 

Hata hivyo, alisema ushauri huo ni mzuri na serikali itafanya maandalizi ya kambi nyingi zaidi na kutenga bajeti kubwa zaidi kwa ajili ya uendeshaji kwa kadri uwezo wa kifedha utakavyoruhusu.

 

Gallery

Popular Posts

About Us