KINGAZI BLOG: 07/16/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, July 16, 2016

PICHA HII YA ZARI AKIWA NA MAMA YAKE YAZUA ZOGO KUBWA MITANDAONI,MAMA DIAMOND AHUSISHWA


Zari Hassani au Zari the Boss Lady amezidi kumake headline leo hii ambapo kupitia picha aliyoweka ya kumtakia heri mapya yameibuka.

Pamoja na watu kumpongeza katika picha hiyo ,lakiwatu mbali mabli waliokomenti katika picha hiyo walibainisha wazi kumtaka Zari kuachana na maisha ya Bongo,hukuw engine wakidai kuwa Heri ya Mama huyo kuliko mkwe wake ambaye ni mama Diamond .wengine pia walidai kushangazwa na ukimya wa mama zari katika maiha ya mwanae,ili hali mam mkwe wake amekuwa akijihusisha na maisha ya mwanae

Wengine walidiriki kumwita mama huyo Malkia kama ambavyo Zari amemtambulisha kwa mashabiki zake kuwa ni malkia wake,zaidi tiririka na comment za mashabiki haoa hapo chini

Fundi adondoka toka ghorofa ya sita mtaa wa Pemba jijini Dar es Salaam

Mfanyakazi ya ujenzi kwenye nyumba inayojengwa mtaa wa Pemba eneo la Kariakoo jijini Dar es salaam mchana wa leo amekimbizwa hospitali baada ya kudondoka kutoka ghorofa ya sita ya jengo hilo.
Haijajulikana bado sababu za kudondoka kwake nasi tunamwombea apate nafuu haraka.

MUONEKANO MPYA WA MWANADADA KAJALA MASANJA

Picha:Baadhi ya mitindo ya mavazi ya zamani

Baadhi ya vijana wamejarbu kuonesha baadhi ya mitindo ya avazi ya zamani atia picha hii

+18 WAKUBWAAA!!!GIGY MONEY NI BALAAA!!!HEBU ONA HAYA MAPOZI HAYA HATARI

Gigy Money share her rude photos throw social medias 



BAADA YA BASATA KUUFUNGIA WIMBO WA NEY WA MITEGO,DIVA WA CLOUDS FM ATOKWA NA 'POVU' HILI..!!!


Katika kile kinachoonekana kuchukizwa na maamuzi ya BASATA ya kuufungia wimbo mpya wa Ney wa Mitego,Diva wa kipindi cha Ala za Roho kinachoruka hewani na kituo cha Clouds Fm,Loveness Love ameibuka na kunena mazito juu ya BASATA.

BASATA ambao wanahusika na kusimamaia kazi za sanaa nchini wameufungia wimbo wa mpya wa Ney wa Mitego kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukiuka maadili ya kitanzania.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter,Diva amesema kuwa BASATA inafaa ifumuliwe ili wawekwe vijana ambao wanapenda mziki wa Bongo Fleva na io wazee ambao wao waapenda nyimbo za MSONGO NGOMA.

Wanafunzi elimu ya juu watoa saa 72 kwa bodi ya mikopo


Kamati ya mawaziri wa mikopo ya serikali za wanafunzi wa Elimu ya juu nchini Tanzania inayoundwa na mawaziri, Manaibu waziri na makatibu wa wizara ya mikopo kutoka vyuo vyote nchini leo July 16 2016 wamkutana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.  
Akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo, Mwenyekiti wa kamati Taifa, Shitindi Venance amesema kipindi cha mwisho wa mwezi huu wanafunzi wa elimu ya juu watatakiwa kufika katika vituo vyao vya kazi vilivyosambaa nchi nzima ili kuendelea kupata mafunzo kwa vitendo ila wamesikitishwa kwamba wakati wakijiandaa na hilo  hakuna mchakato wowote unaoendelea kupelekea kupata fedha hizo, Shitindi amesema…….
>>>Mpaka sasa hivi tukiwa tumebakiwa na takribani siku tano kabla ya kufunga chuo hakuna hata karatasi za kusaini zilizotumwa vyuoni ili kukamilisha zoezi hilo na mchakato wa kusaini hukuchukua muda wa siku tatu mpaka tano
>>>Kutokana na ucheleweshaji huo tunatoa muda wa saa 72 kuanzia leo Jumamosi, mpaka Jumanne ya wiki ijayo kwa bodi ya mikopo kufikisha fedha za kujikimu wakati wa mafunzo kwa vitendo katika vyuo vyote hapa nchini ili wanafunzi waweze kusaini na kupokea malipo yao:-Shitindi
millard ayo.com

SAKATA LA DK MWAKA KUFUNGIWA WAZIRI WA AFYA ATOA KAULI HII 


SEREKALI imemtaka Dk Mwaka kwenda kwenye sheria kama hajaridhika na uamuzi wa serikali wa kukifungia kituo chake cha tiba za asili.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na wadau wa afya katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera.Ummy alisema kuwa uamuzi uliofanywa na serekali wa kukifunga kituo cha afya cha dk Mwaka ni sahihi kwani hajaonewa kwasababu matangazo na huduma alizokuwa akitoa zilikuwa haziendani na maadili na taratibu za udaktari.
“Dk Mwaka asichonganishe wananchi na serekali yao kwamba tumewafungia huduma walizokuwa wakipata kwake wakati huduma alizokuwa akitoa hazikuwa na sifa”alisema Ummy
Alisema kuwa kama anaona ameonewa aende mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake.”Kama anaona tumemuonea aende mahakamani tutakutana huko”alisema
Waziri ummy Mwalimu yupo Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo amezindua jengo la wodi ya wazazi iliyojengwa na shirikala jhpiego lenye thamani ya shilingi milioni 150

V

TCU YATANGAZA VIGEZO VYA KUJIUNGA NA ELIMU YA JUU/CHUO KIKUU MWAKA 2016/17 SOMA HAPA

tcu banner
BAADA YA KUTOKA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA JANA TAREHE 15,BODI YA VYO VIKUU IMETANGAZA VIGEZO VYA KUJIUNGA NA ELIMU YA CHUO KIKUU
KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 KUJUA ZAIDI BOFYA HAPA CHINI





Ukiiangalia hii video unaweza kuacha kwenda kwenye makanisa ya "kiroho"...

Kinachonisikitisha zaidi sio utapeli wa huyu nabii, bali ni kuwa hadi sasa kuna watu wanaenda kwenye kanisa lake...

Kweli binadamu tu wajinga!!!
Las

Magazeti ya Leo Jumamosi ya July 16, Ikiwemo Habar Shule ya Kata Yafanya Kweli Matokeo Kidato cha Sita



SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya July 16, Ikiwemo Shule ya Kata Yafanya Kweli Matokeo Kidato cha Sita

Wanajeshi 104 Waliotaka Kumpindua Raisi wa Uturuki Wauwa Katika Jaribio la Mapinduzi

Naibu mkuu wa jeshi la Uturuki ametangaza kwa njia ya runinga kuwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi limeshindwa.

Jenerali Umit Dundar alisema kuwa wapanga mapinduzi 104 wameuauwa. Pia amesema kuwa watu wengine 90 wakiwemo polisi na raia wameuawa.

Usiku kucha miji ya Ankara na Istanbul ilikumbwa na milio ya risasi na milipuko baada ya wanajeshi waasi kufanya mashambulizi wakitumia vifaru na helikopta.

Maafisa wanasema kuwa zaidi ya wanajeshi 1500 wamekamatwa huku wale wa vyeo vya juu wakiwemo majerali wakipokonywa nyadhifa zao.

Mhe. Rais, Hivi Ndiyo Julius Nyerere International Airport Inavyowatesa Wageni na Kuwakimbiza

Mheshimiwa Rais, labda hili litakuwa gumu kidogo kwa wewe kuligundua maana viongozi wote wanapopita pale uwanjani huwa hawatumii njia na process hii ambayo sisi watu wa kawaida na wageni wanaotoka nje huwa wanaitumia katika kupata viza (tourist visa) ya kuingia nchini.

Pale kuna uozo mkubwa sana na si hilo tu basi upoteaji mkubwa wa fedha za serikali ambazo nadhani huwa zinaingia mifukoni mwa baadhi ya wafanyakazi na viongozi wao, ni mtandao ambao upo kwa muda mrefu tu. Ni usumbufu kwelikweli usiokuwa na sababu yoyote.

Sasa ninaelezea kwa kirefu:
Wageni wengi wanaokuja Tanzania na kuchukulia visa zao pale aiport huwa wanatozwa dola za kimarekani 50 ($50.00 Usd) na huwa hawakubali aina nyingine yoyote ya pesa isipokuwa dola za kimarekani tu. (hilo ni tatizo namba 1).

Wageni wanapofika basi kuna mtu (sijui ni nani na anatoka department gani) husimama pale na kukusanya passport zote na hizo dola 50 (kila passport huwekwa dola 50 ndani yake) huyo mtu huzikusanya bila hata ya kutoa risiti yoyote,(na kuwaambia msubiri) na kuenda nazo kusikojulikana (labda ni ofisini kwao) kwa ajili ya kuweka hizo viza, hapo sasa ndiyo kuna tatizo kubwa sana, Mtasubiri si chini ya saa moja ndipo mtarudishiwa passport zenu na viza tayari zimo ndani, akifika huyu mtu anaanza kuita majina na kukukabidhi passport zenu ili sasa muelekee uhamiaji kwa ajili ya kupata entry ya kuingia, wakati huo sasa wale wenzenu wote mliokuja nao wameshamaliza kupita kwa watu wa forodha na wako nje tayari.

Nimesikia kwa sasa hivi huyo mtu wa kukusanya hizo passport hayupo ila walichofanya ni kuweka kijiofisi kidogo ambacho hufanya hivyo hivyo, unafika pale kwenye hicho kijiofisi na kumpa passport na dola 50 (hawataki aina nyingine yoyote ya fedha) na HUPEWI risiti yoyote, halafu unaambiwa usubiri, baadaye anakuja mtu kuzikusanya passport zote hizo anaenda nazo ndani huko, hapo bado tena mtasubiri siyo chini ya saa moja au mawili ndiyo mrudishiwe hizo passport. Mimi nilishuhudia wageni wenye asili ya kizungu wakilalamika sana pale airport kuhusu huo usumbufu.

Sasa mimi maswali yangu ni kwa nini wanapenda kuwafanyia watu huu usumbufu? na hapo ni dhahiri kuwa kuna pesa nyingi tu ambayo badala ya kwenda serikalini basi huingia mifukono mwa watu.

Sasa Mheshimiwa Rais kama tuko kwenye kuitengeneza Tanzania hii kuwa nzuri, bora na ya uwajibikaji, kwa nini basi usisafishe na kulitatua tatizo hili? Mimi naamini kabisa kuwa wageni wengi wanaokuja TZ wakishapata usumbufu huu basi huwa hawarudi tena na badala yake wanakwenda nchi jirani.

Nini cha kufanya:
Nimetembelea nchi nyingi ambazo hutoa viza palepale airport (visa on arrival) na hukuti matatizo kama haya kwa sababu hakuna wizi.

Nchi 1: Hapa ukifika tu utakuta kuna ofisi, unaenda dirishani unampa passport yako na pesa au bank card (pesa ya kigeni yoyote inayotambulika, zote zimeorodheshwa pale), palepale anakubandikia visa (sticker) na unaelekea kwa uhamiaji. Kitendo hicho hakichukui hata dakika 5.

Nchi 2: Hawa hawataki fedha taslimu kabisa, ni bank card tu, ukifika tu unaenda kwa uhamiaji moja kwa moja, pale unafanya malipo kwa bank card yako, unapata risiti na anakugongea viza (mtu huyohuyo mmoja), kwa hiyo yeye hakamati fedha taslimu kabisa. Hapa sasa tunaweza kusema kwa wale wasio na card je? Jibu ni hivi, kwanza watu wengi wanaoomba viza hapo airport ni wageni na ndiyo maana wanaomba hizo viza, kwa asilimia kubwa ya hao watu wanazo kadi, na pili unaweza kununua Prepaid visa/mastercard, kwa wale wanaoishi ughaibuni watanielewa, kupata bank card huko ughaibunu siyo big issue.

Nchi 3: Hawa sasa ukifika unaenda dirishani kulipa kwa bank card au fedha taslimu, halafu anakupa risiti unaenda nayo kwa uhamiaji na passport yako na uhamiaji anakupigia entry visa kwenye passport yako na kwenye ile risiti, hapo huchukui hata dakika kumi.

Sasa mimi sisemi tuige hayo hapo juu (lakini kama ni mazuri kwa nini tusiige?) lakini tukichukua yote hayo na kuyachanganua vizuri basi tunaweza kutengeneza mfumo wetu wenyewe ambao hautampa mgeni usumbufu hapo airport. Pili ningependa pia kuiomba serikali hizi balozi zake ziwe zinajaribu kutoa visa kwa waombaji wake kwa haraka kidogo ili kuondoa nenda rudi nyingi.

Mimi naamani kabisa kuwa hilo tatizo linaweza kutatulika na mtiririko wa wageni unaweza kuongezeka, maana wenzetu wageni huwa hawapendi usumbufu, kwanza huwa wanakuja kutembea na hivyo huwa hawapendi kupata bugudha kama hizo hasa ukizingatia kuwa Airport ndiyo kioo cha nchi, maana ya kwamba mgeni akiona mwenendo wa pale airport (airport yoyote duniani) basi tayari inampa taswira ya nchi hiyo ilivyo.

Kwa hiyo Naomba Mheshimiwa Rais na waziri husika mlifumbulie macho suala hili, Fedha za serikali pale airport bado zinaliwa na wajanja.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki JPM

By Pepe17/JF

GIGY MONEY ASEMA BILA PESA HATOI PENZI,AELEZA HAYA


Stori: Boniphace Ngumije
Muuza sura kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amefunguka kuwa kutokana na wanaume wengi wakware kupenda kuwatumia mastaa kisha kuwaumiza, anawatangazia kuwa hana mapenzi ya dhati, mwenye fedha ndiye atakayemfaidi.
Akipiga stori na gazeti hili, mwanadada huyo aliongeza kuwa amejionea na kujifunza hilo kutoka kwa mastaa wenzake.
“Mimi mwanaume akinihitaji namuuliza kama ana fedha, kama hana natupa kule,” alisema

GPL

Basata Waufungia Wimbo wa "Pale Kati Patamu" was Ney wa Mitego

KUFUNGIWA NA KUPIGWA MARUFUKU KWA WIMBO WA ‘PALE KATI PATAMU’ WA MSANII EMMANUEL ELIBARIKI ‘AKA’ NEY WA MITEGO 
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘pale kati patamu’ ulioimbwa na Msanii Ney wa Mitengo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili.

Msanii huyu amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua Sekta ya Sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonesho yenye kukiuka maadili. Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.

Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kuhakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya sanaa.

ikumbukwe kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine. Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa Pale Kati patamu ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama. 
Kwa mantiki hii BASATA halitavumilia wasanii wachache ambao wanataka kuigeuza tasnia ya sanaa na wasanii genge la wahuni wasio na staha na wanaojipanga kuibomoa jamii. BASATA linapenda kueleza ya kufuatayo · BASATA linatamka kuwa limeufungia wimbo huu rasmi kutumika kwa namna yoyote ile. · Aidha pamoja na adhabu ya kufungia wimbo huu hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. 
Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapotengeneza kazi zao. 
SANAA NI KAZI, TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI 
Godfrey Mngereza 
KATIBU MTENDAJI

RAIS MAGUFULI ATIMIZA AHADI YAKE AMPA KAZI MREMA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Mhe. Augustino Lyatonga Mrema.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.Katika uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Mwenyekiti wa Chama cha TLP Taifa, Mhe. Augustino Lyatonga Mrema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole. Miezi kadha iliyopita Mrema alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akimuomba Rais Magufuli ampe kazi yeyote kwenye serikali yake ili amsaidie kutumbua majipu.





UFAFANUZI KUHUSU SIFA/MAKSI KULINGANA NA MATOKEO YAKO YA FOMR 6 ZA KUINGIA CHUO KIKUU 2016/2017


Habari yako,
Kama ambavyo ahadi yetu kukufanya wewe mdau wetu upate kitu roho inapenda.Jana matokeo ya kidato cha sita yalitangazwa.

Hongereni sana kwa mliofaulu na mliofeli msikate tamaa,jaribuni kutafuta altenative mapema kabla mda haujakupita.

MASWAYETU BLOG imepokea maswali mengi sana,kutoka kwa wadau wa blog hii hasa form 6 wanaotarajia kwenda chuo kikuu.
swali lililoulizwa sana:JE DIV III WANAENDA CHUO KIKUU?
JIBU: siku zote kuchguliwa chuo kikuu hawaangalii divison ya mtu,ila wanaangalia minimum entry qualifcation za kuingia chuo.Minimum entry qualifiction hapo nyuma ilikuwa ni lazima upate E mbili kwenye combination yako.
Lakini juzi TCU walibadilisha Vigezo na kupandisha hadi D mbili.
Hii inamaana kwamba Endapo kama umepata D D F-DIV 3 Pts 15 chuo utapata kwa sababu una minimum entry qualification za kujiunga chuo kikuu.
ila kama una A E E DIV 2 pts 11 chuo huwezi kupata kwa sababu hauna minimum entry qualification.

Kutokana na maelezo hapo juu ni kwamba ,umeona mtu alie na D mbili ana DIV 3 pts 15 lakini sifa za kwenda chuo kikuu
anazo.lakini mwenye DIV 2 pts 11 hana sifa za kwenda chuo.


swali jingine:Je,mwenye DIV III Atapata mkopo mwaka huu?  

jibu:Wengi mmekuwa mkichanganya kati ya GRANT na MKOPO ,kutokana na guidelines za bodi ya mikopo ni kwamba ,
GRANT ni kama schoralship utolewa kwa wanafunzi waliofaulu sana yaani DIV 1 & 2 ,pia lazima uwe umechaguliwa kusoma kozi za MEDICINE,MIFUGO au LABORATORY.

LOAN utolewa kwa wanafunzi wote waliofaulu kwa kiwngo cha kuanzia DIV 1 hadi 3 ,ila kigezo kikubwa uwe umechaguliwa kusoma kozi zenye priority na mkopo.

bonyeza hapo kuona kozi zenye priority>>>>KOZI PRIORITY 2016/2017


bonyeza hapo kuona matokeo form 6 na ualimu 2016>>>>ACSEE,GATCE AND DSEE NECTA RESULTS 2016



Conclusion: 
Kuanzia leo naomba ujue na umwambie rafiki yako kwamba chuo kikuu huwa hawaangalii DIVISON katika kuchagua wanafunzi ,bali wanaangalia MINIMUM ENTRY QUALIFICATIONS ambazo ni lazima uwe na principle passes mbili ambazo ni D D ktk combination yako uliyosomea.mfano kama ni PCM lazima uwe na  atleast kuanzia D D katika masomo yako ili uwe na sifa za kwenda chuo kikuu 2016/2017.

thanks.

HAYA HAPA MATOKEO YOTE YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2016



THE NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

Baraza  za mitihani la tanzania jana limetangaza matokeo ya kidato cha Sita pamoja na Vyuo vya ualimu kwa mwaka 2016, na kama kawaida yetu KINGAZI BLOG hatuko nyuma kukuletea list nzima ya majina ya matokeo yoooote!!  hebu bofya hapo chini.

 >>>BOFYA HAPA KUONA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2016.<<<<<<
>>>>BOFYA HAPA PIA KUONA MAJINA MENGINE.<<<<
 

Gallery

Popular Posts

About Us