
Mamia ya watu wamekongamana nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa kuupokea
mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan
Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa
kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya
mwili huo kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za
mwisho.
Maafisa...