KINGAZI BLOG: 05/16/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, May 16, 2016

USAFIRI WA MABASI YAENDAYO HARAKA DAR ES SALAAM WAGUBIKWA NA CHANGAMOTO LUKUKI

Baadhi ya watu wanaotaka kusafiri na mabasi ya yaendayo haraka wakiwa katika kituo cha Posta ya Zamani (Baharini) wakipewa maelekezo kuwa katika kituo hicho mashine za kutolea tiketi zimeleta hitilafu kwa leo.

 Basi la mwendo wa haraka likitoka katika kituo cha Posta ya zamani bila kupakia abiria kutokana na kutokuwepo kwa tiketi kwa sababu ya mashine za kituo hicho kuleta hitilafu ya mtandao wa kutolea tiketi.
AULI za usafiri wa Mabasi yaendayo haraka zimeanza kutozwa leo katika jiji la Dar es Salaam huku kukiwa na changamoto nyingi katika vituo vya mabasi hayo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Afisa Uhusiano wa UDART, Deus Bugaywa amesema kuwa changamoto waliokutana nayo ni baadhi ya vituo kukosa mashine za kukatishia tiketi, mafuriko ya watu katika vituo pamoja na chenji kwa wasafiri wanaotumia huduma hiyo.

Amesema mfumo wa kadi ukianza utaondoa changamoto hiyo kwa wakazi wa Dar es Salaam na mfumo wa tiketi utatumika kwa wale ambao wanaingia katika jiji na kuondoka.

Aidha amesema mfumo huo unatakiwa fedha itakayotolewa lazima usome benki kuu kwa kuonyesha kodi katika tiketi, suala la chenji ni chagamoto kutokana na fedha ya chenji waliokuwa nayo ni milioni sita za sarafu lakini zimeweza kuisha.

Baadhi ya wananchi wanaotumia usafiri wamesema kuwa kuanza kwa usafiri huo umekuwa ni mapema kwa kushindwa kuona changamoto hizo.

Mmoja wa wananchi, Juma Said amesema kuwa wamekwenda kukata tiketi katika kituo na kuambiwa waende kituo kinachofuata hali hiyo ameona kuwa ni usumbufu.

Hata hivyo amesema kuwa mtu mmoja anapata tiketi ndani ya dakika 10 ambapo  ni vigumu kwenda na idadi ya watu kuweza kwenda kwa wakati.

HARMONIZE ATHIBITISHA UHUSIANO WAKE NA JACKLINE WOLPER,AANDIKA UJUMBE MZITO

Harmonize confirms that he is Dating Jackline wolper,its official now that Harmonize is dating Bongo Movie Actress Jackline wolper, and Harmonize have prove that after posting the image of Jackline wolper into his Instagram Account okay, let us pray for them and see where they end

Bunge Liliahirishwa Leo Asubuhi Kupisha Kamati ya Kanuni ipitie Hotuba ya Upinzani Iliyozuiliwa

Hotuba ya Godbless Lema, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilizuiliwa leo asubuhi  kusomwa Bungeni hadi ipitiwe  upya na kamati ya kanuni.

Bunge liliahirishwa  leo asubuhi hadi saa 10 jioni baada ya kuzuia kusomwa kwa hotuba hiyo kwa madai kwamba, ina maneno yanayohitajika kuondolewa ili ikidhi matakwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Kanuni.

Ndani ya Hotuba ya Lema  kipo kipengelea kinachoelezea sakata la makataba tata wa Kampuni ya Lugumi ambapo Kamati ya Mambo ya Ndani ilielezwa suala hilo kutojadiliwa bungeni kwa madai tayari lilikuwa limeanza kuchunguzwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Kipengele kinachohusu mkataba wa Kampuni ya Lugumu kipo kwenye sehemu ya tano inayoeleza Mikataba Tata ya Jeshi la Polisi.

Kwa muda mrefu mkataba huo uliotolewa na Jeshi la Polisi nchini kwa Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd wenye thamani ya Sh 37 bilioni umedaiwa kuwa na harufu ya ufisadi.

Mwaka 2011, kampuni hiyo ilipewa zabuni ya kufunga mashine za alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchini na kulipwa Sh 34 bilioni kati ya Sh 37 bilioni sawa na asilimia 99 ya malipo yote.

Mambo mengine yaliyosababisha hotuba hiyo izuiliwe ni  Uuzwaji wa nyumba uliomtaja Rais John Magufuli moja kwa moja, Rushwa na bunge kutumika kuwalinda watuhumiwa , tabia ya Rais na usalama wa nchi na mwisho ni kuwataja viongozi wa juu wa serikali kwa maneno ya dhihaka.
 

WAZIRI ATAKA WATUHUMIWA WANAOONEKANA KATIKA VIDEO INAYOSAMBAA MITANDAONI WAKIMBAKA MWANAMKE WAFIKISHWE MAHAKAMAN

I

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametaka watuhumiwa waliombaka mwanamke eneo la Dakawa mkoani Morogoro na video yake kusambazwa wafikishwe mahakamani haraka.

Haya ndio maneno ya Waziri Ummy Mwalimu katika Akaunti yake ya Facebook:

Ndugu zangu! Nimeiona dakika chache zilizopita video ya mwanamke akidhalilishwa na wanaume wawili (mashuka yanaonyesha eneo la Tiff Lodge Wami - Dakawa). Nakemea kwa nguvu zangu zote waliofanya kitendo hiki. Ni unyama uliopitiliza. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu. Hatuwezi kuuvumilia.

Nimeshamuomba Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP wachukue hatua stahiki haraka.

Pia nawaomba sana ndugu zangu msisambaze hizo video. Hiyo ni kuendelea kumdhalilisha huyo dada. Amebakwa na pia wamerekodi hilo tukio! Hii haistahimiliki na haivumiliki. Wanawake wote na wanaume wapenda haki na maendeleo ya wanawake tukemee kwa nguvu zetu zote unyama huu.

SOMA MAELEZO YA MDADA ALIYELETEWA VIDEO HIYO
 Jana usiku kaka yangu mmoja kaniletea video iliyonifanya nisipate usingizi. Ni clip mbili za dada mmoja aliyetekwa na kuwekwa chumbani na wanaume wawili. Wamempiga picha za uchi na kumtendea tukio baya kabisa.
Yule dada analia na anajaribu kuficha sura lakini anapigwa na kuingiliwa kwa nguvu. Wanazungumza kiswahili. Wanaonesha ubakaji kwa kurekodi. Shuka la nyumba linasomeka Teth Lodge, ya BOX 63. Mahali ilipo hapaonekani vema lakini ni kama vile Wami Dakawa.
Sidhani kama huyu dada ataendelea kuishi kama binadamu wa kawaida maana kisaikolojia lazima atakuwa kaumia sana hata akibaini hii clip inasambazwa tayari. Nimeshindwa kuiweka hapa kwa kuwa inasikitisha sana. Naandika nikilengwa machozi.
Sihukumu, Mungu anisamehe lakini nadhani hawa wabakaji wanastahili adhabu kali kuliko zote tuzijuazo. Mungu ampe nguvu huyu binti

CHANZO: JAMII FORUM

Waziri Nape Alivyofafanua Suala La Kurusha Live Bunge Mjini Dodoma


Sehemu ya Majumuisho ya Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitolea ufafanuzi suala la Bunge  kurushwa Live na studio za Bunge.


Serikali Yasema Kusitishwa kwa Baadhi ya Misaada ya Wahisani Hakujaathiri Sekta ya Nishati



Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo ameliambia Bunge Mjini Dodoma kwamba miradi ya umeme vijijini (REA) haijaathirika chochote kwa Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) kuondoa misada yake Tanzania.

Muhongo ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyetaka kujua serikali imepata hasara kiasi gani kwa MCC kuondoa fedha zake katika miradi ya umeme nchini.

Akijibu swali hilo Prof Muhongo amesema fedha za MCC zilikuwa haziendi kwenye miradi ya maendeleo ya umeme vijijini hivyo miradi hiyo itaendelea kama ilivyopangwa.

''Hakuna dola hata moja ya MCC iliyokuwa inaenda kwenye umeme vijijini fedha zilikuwa zikienda kwenye miradi ya maji, barabara na nishati lakini siyo umeme wa vijijini na fedha za kwenye nishati zilikuwa hazivuki theluthi moja hivyo kama umejiandaa kulima hekari 8 akakuongezea mtu 2 ili zifike 10 siku akiondoa za kwake utandelea na zako 8 kama kawaida''-Amesisitiza Prof. Muhongo.

Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) ilisema Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea msaada wa awamu ya pili ambao ulikuwa wa jumla ya Dola 472.8 milioni ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja za Tanzania.

Kwa awamu ya kwanza Tanzania ilipokea Dola 698 milioni na moja kati ya mambo yaliyosababisha MCC kuondoa fedha zao ni pamoja na kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.

Majaliwa asema serikali inataka watu wake wafanye kazi ndiyo maana wamezuia matangazo ya bunge live


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa serikali kuzuia matangazo ya live ya bunge ni kuwafanya wananchi wake wafanye kazi kwa bidii na kuacha kushinda kwenye runinga wakiangalia bunge.

Tayari Bunge limeshaelezwa sababu mbili tofauti za kukatisha matangazo hayo ambazo ni gharama ambazo Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) linalipia na hivyo kulazimika kupunguza matangazo hayo.

Awali, Waziri wa Habari, Nape Nnauye ambaye alitoa tamko hilo bungeni, pia alisema vyombo binafsi vinaruhusiwa kurusha matangazo hayo moja kwa moja, lakini navyo vimepigwa marufuku.

Sababu nyingine iliyotolewa na Nape ni kuwa uamuzi wa kuzuia matangazo hayo ulifanywa na Bunge la Kumi wakati likipitisha uamuzi wa chombo hicho wa kuanzisha studio yake.

Lakini juzi, akiwa nchini Uingereza Majaliwa alikuwa na sababu nyingine ya kuzuia matangazo hayo kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni.

Akijibu swali kuhusu sakata hilo wakati akizungumza na Watanzania waishio London, Majaliwa, alisema kurusha moja kwa moja matangazo ya shughuli za Bunge ni kwenda kinyume na “Hapa Kazi Tu”, kaulimbiu ya Rais John Magufuli aliyoianzisha wakati wa kampeni.

“(Kurusha shughuli za Bunge moja kwa moja) Maana yake ni kuwa katika kipindi cha Bunge la Bajeti ambalo linaendeshwa kila siku, Watanzania wangekuwa wanaangalia Bunge kwa miezi hiyo mitatu bila ya kufanya kazi,” alisema mtendaji huyo mkuu wa Serikali.

“Tulilazimika kujifunza kutoka kwenye mabunge mengine. Hivi hapa Uingereza mnaangalia Bunge live kila siku?” alihoji Waziri Mkuu na kujibiwa kuwa linarushwa moja kwa moja kwa kipindi kisichozidi dakika 15 wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu.

Majaliwa alisema Bunge la Tanzania lilikuwa pekee katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na duniani ambalo lilikuwa likirushwa moja kwa moja kuanzia asubuhi hadi usiku.

Waziri Mkuu aliendelea kufafanua kwamba Bunge la Tanzania linarusha moja kwa moja kila siku asubuhi wakati wa maswali ya kawaida na Alhamisi asubuhi wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu.

Alisema mijadala yote hurekodiwa na kuhaririwa, kisha hurushwa kati ya saa 8:00 mchana na 9:00 alasiri na kati ya saa 3:00 na 4:00 usiku.

“Kwa Watanzania wanaopenda kufanya kazi na wanaopenda kufuatilia mambo ya bungeni, walikuwa hawaoni ‘live coverage’ kwa sababu walikuwa kazini, lakini sasa hivi wanaweza kufuatilia masuala ya Bunge,” alisema Majaliwa na kuongeza kuwa muda wa jioni uliopangwa, mtu anakuwa ametoka kazini na anaweza kuangalia televisheni akiwa nyumbani.

Source: Mwananchi

Aibu, Fedheha ya Mabasi ya Mwendo Kasi, Jiji, Manispaa Dar


IKIWA ni siku tano kupita baada ya mabasi ya mwendo kasi kuanza kusafirisha abiria katika Jiji la Dar es Salaam, hali ya vituo vyake inatisha, anaandika Happiness Lidwino.

Baadhi ya vituo hivyo vinatoa harufu kali, vimeenea mikojo, kinyesi na takataka ngumu ambapo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na manispaa husika vimedai kutohusika na usafi wake.
Miongoni mwa vituo alivyotembelea mwandishi wa habari hii ni pamoja na Moroco (Kinondoni), Kinondoni B, Manyanya na Kimara Baruti ambapo vituo hivyo vimekuwa na hali inayotia shaka usalama wa abiria wanaotumia vituo hivyo kusubiri usafiri.

Gatson Makwembe, Msemaji wa Jiji alipoulizwa kuhusu ufuatiliaji wa usafi kwenye vituo hivyo baada ya hali kuwa mbaya, amedai jiji halihusiki.
“Mimi siwezi kuzungumzia suala hilo kwani sisi halituhusu labda uwatafute Dart au Msemaji wa Manispaa ya Kinondoni,” amesema Makwembe.

Sebastian Mhowera, Ofisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni alipoulizwa, alidai kazi ya Manispaa ya Kinondoni ni kusimamia usafi wa barabarani pekee.

“Sisi kazi yetu ni kusimamia usafi barabarani ndani ya manspaa hii na sio uchafu uliopo ndani ya vituo vya mabasi ya UDA. Siwezi kuzungumzia uchafu uliopo kwenye nyumba ya jirani,” amesema.
Alipotafutwa William Gatambi, Msemaji wa Kampuni ya Dart inayosimamia UDA hakupatikana kujibu aliye na dhamana ya kufanya usafi kwenye vituo hivyo.

Hali ya wasiwasi inaendelea kutawala kwa wananchi kutokana na vituo hivyo kuwa na hali mbaya, kukosa ulinzi na hata kugeuka kuwa maeneo ya vibaka, mateja na watoto wa mitaani kupata hifadhi ya usingizi.

Kituo cha Kimara Baruti kimekuwa na mlundikano mkubwa wa watu, harufu mbaya inayotokana na kinyesi, mkojo huku mwingine ukiwa umefungwa kwenye chupa za maji na kutupwa hovyo. Uchafu wa kituo hicho unafanana na vituo vingine.

John Mgonja, mmoja wa abiria aliyekuwa akisubiri usafiri katika Kituo cha Moroco ameeleza kushangazwa na huduma mbovu za vituo hivyo.
“Kwanini vituo havina ulinzi, hakuna maji, sakafu chafu, taka ngumu kila mahali na harufu mbaya mpaka imekuwa kero.

“Sijui sisi tuna tatizo gani, hivi haya mambo yote hayakuwa kwenye mpango wao. Wao wanachojua ni kukusanya fedha kwa ajili ya nauli tu?” amehoji Mgonja.

Amesema, watu wanalazimika kufanya hivyo kwa kuwa, kama amebanwa na haja na vyoo vipo kwake anaona ni bora kikudhi haja yake kwanza mengine mbele kwa mbele.
“Sasa kama umefika hapa na umebanwa kwanini usijisaidie, lakini hata kama utaacha vyoo vichafu nani atakukamata? Hakuna mlinzi na hakuna usalama wowote,” amesema.

PENZI LA ALI KIBA ,DIAMOND PLATINUMS LAMTESA JOKATE KIDOTI


Mlimbwende Jokate Mwegelo ‘Kidoti’. 
Siri imevuja kuwa penzi la vinara wawili wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond PlanumZ’ na Ali Saleh Kiba ‘King’ linadaiwa kumtesa mlimbwende Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye amekuwa akijutia kujiingiza kwenye uhusiano na wasanii hao. TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Jokate, hivi karibuni alitupia mashairi ya Wimbo wa Ndi Ndi Ndi wa Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo baadhi ya mashabiki wake walimtaka kuwaahidi kuwa hatarudia kujiingiza kwenye penzi la mastaa hao (yaani Diamond na Kiba) kwani ishu hiyo ilimfanya atafsiriwe vinginevyo tofauti na ilivyokuwa awali. Ilisemekana kuwa kauli hizo za mashabiki hao zilikuwa kama kugongelea msumari wa moto kwenye kidonda kwani ishu hiyo imekuwa ikimsumbua na kumsababishia maumivu yanatokana na kujutia uamuzi wake huo kwa kuwa hakudumu nao. 

Jokate akiwa na Ali Kiba.
“Unajua Jokate alijijengea na ana heshima sana kwenye jamii yetu kwa uwezo na upeo wake (IQ) na hata kujitambua, sasa anapokuwa na uhusiano na msanii kisha baada ya muda mfupi akaachana naye kama 
ilivyokuwa kwa Diamond na sasa Kiba, inaweza kumshusha hadhi, na hiyo ndiyo inamfanya Jokate ajute kujiingiza kwenye mapenzi na mastaa hao,” kilifunguka chanzo hicho. 
ALIPASWA KUWA BUNGENI?
Hata hivyo, baadhi ya watu wake wa karibu walikwenda mbele zaidi na kusema kwa muonekano wake alipaswa kuwa mjengoni (bungeni) akitema madini, kwani hawana hofu na elimu yake ila tatizo ni hilo tu la ‘kurukaruka’ na wasanii. “Kiukweli Jojo (Jokate) anastahili kuwa bungeni akitafuta njia mbadala ya kutatua matatizo ya wananchi wake wa jimbo lake f’lani hivi. “Au kama anataka kuendelea na mapenzi kwa kuwa ameachana na Kiba basi atafute mtu wake na kutulia naye kwani kuna baadhi ya warembo wenye majina wana watu wao na wametulia wanafanya mambo ya kujenga taifa,” alisema mmoja wa watu hao. 

HUYU HAPA JOKATE 
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Wikienda lilimtafuta mlimbwende huyo na kumfikishia madai hayo kisha kumweleza mabadiliko wanayotaka mashabiki na watu wake wa karibu ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Siku zote ninavyojua mimi mapenzi hayachagui, suala la kumpenda nani kwa maana ya staa, kiongozi, fukara, mwenye elimu au asiyekuwa nayo na wengineo ni matakwa ya moyo wangu kutokana na ulipodondokea. “Kama ni ishu ya kuwa bungeni ni suala la muda, wakati ukiwadia basi kila kitu kitakuwa sawa. Kama ni mchumba wasubiri watamuona siku ya ndoa lakini hao wengine wala sijatoka nao!”

KABLA YA DIAMOND, KIBA 
Ukiachilia mbali Diamond na Kiba, pia Jokate aliwahi kukiri na kuripotiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mbongo anayekipiga kwenye Ligi ya Kikapu ya Marekani, NBA, Hasheem Thabeet.
CHANZO: IJUMAA WIKIENDA

VIDEO YA WEMA SEPETU YAMUWEKA PABAYA,NI ILE ILIYOMUONYESHA AKIDENDEKA


Kipande cha video kilichosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii ya Instagram, Facebook na WhatsApp kikimuonesha staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘akidendeka’ chumbani na mwanaume kimemuweka pabaya baada ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo kusema kuwa kama ni sehemu ya filamu haina maadili ya Kitanzania. 
Akizungumza na Wikienda kwa njia ya simu akiwa nje ya nchi wikiendi iliyopita, Fisoo alisema kuwa kama ni filamu mpya ya mwanadada huyo, ikiingizwa sokoni ikiwa haina maadili yanayotakiwa kamwe hawawezi kuruhusu kusambazwa popote na wala hawawezi kuipitisha. 
Kipande hicho cha filamu hiyo kinamuonesha Wema akiwa anadendeka kikwelikweli na jamaa huyo jambo ambalo bodi hiyo imeliangalia kwa upande wa pili na kwamba haitaingia sokoni ikiwa hivyo. Baadhi ya mashabiki wa Wema waliokiona kipande hicho walikuwa na maswali lukuki kichwani kutokana na kile walichokuwa wakikiona kwenye kipande hicho cha filamu hiyo. 
“Jamani hata kama ni filamu, hapana, imezidi, kwa kweli ni hatari sana maana kama Wema angekuwa mwanamke wangu hata hiyo filamu angeacha kuicheza kabisa,” alisema mmoja wa mashabiki hao. Kwa upande wake mpenzi wa Wema ambaye ni Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan alisema kuwa na yeye anatamani kupata nafasi ya kucheza filamu, tena apewe vipande kama hivyo hata kama ishirini, atacheza kwa uangalifu.
“Yaani na mimi napenda sana nicheze filamu vipande kama hivyo ishirini hivi tena nitacheza vizuri sana maana najua kila mtu anaweza kuigiza kama hivyo,” alisema Idris. Kwa upande wake Wema hakutaka kusema chochote juu ya kipande hicho.
CHANZO: IJUMAA WIKIENDA

Makonda: Wanawake Ndiyo Chanzo Cha Ufisadi Nchini





MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanawake wamekuwa ni chanzo cha ufisadi nchini kutokana na kupokea zawadi zitokanazo na fedha za kifisadi.

Makonda aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani Vingunguti Dar es Salaam jana katika mkutano wa kujadili namna ya kupata mikopo mbalimbali kutoka Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

” Ninyi wakina mama mmekuwa chanzo cha ufisadi kwa vile mmekuwa mkipokea fedha na zawadi mbalimbali kutoka kwa watoto wenu lakini mmekuwa hamuwahoji wanako zitoa fedha hizo kwani zingine zinakuwa za kifisadi” aliseama Makonda.

Makonda aliwaambia wanawake hao kuwa hata katika suala zima la usafi linaanzia na malezi ya usafi ya wakina mama kwa watoto wao tangu wakiwa wadogo jambo ambalo lingesaidia kipindi hiki ambapo kunachangamoto kubwa ya kusafisha miji yetu.

Katika hatua nyingine Makonda alitoa pongezi kwa Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto kwa kuwa jirani na wananchi wa kata yake kwa kufanya maendeleo bila ya kujali itikadi za vyama hasa katika kujipatia mikopo kutoka katika Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

“Nimefurahishwa na diwani wenu Kumbilamoto kwa kushirikiana nanyi ili  kujiletea maendeleo ni jambo zuri na wakati huu ni wa kukutana kubuni na kuangalia jambo gani litawakwamua kiuchumi badala ya kuwaza maandamano yasiyo na tija” alisema Makonda.

Auawa Kwa Kuchomwa Visu Akituhumiwa Kutoka Kimapenzi na Mtalaka Wake




Mkazi wa Kijiji cha Chala B, Tarafa ya Chala wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa, Moses Nambasita (48) ameuawa kwa kuchomwa visu kutokana na kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Akisimulia mkasa huo mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Vincent Mwanambuu alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni baada ya kuvamiwa na kijana mmoja alipokuwa akitoka nyumbani kwake kwenda nyumba jirani, alishambuliwa kwa kuchomwa visu.

Mwanambuu alisema baada ya kupata taarifa hizo alitoa taarifa Kituo kidogo cha Polisi Chala, askari walifika na kuchukua mwili kwa ajili ya uchunguzi na kuanza msako dhidi ya mtuhumiwa.

Akielezea chanzo cha mauaji hayo, Mwanambuu alisema mtuhumiwa alipata taarifa kuwa Nambasita ana uhusiano na mtalaka wake, ambaye walikuwa wameachana kipindi kirefu.

Alidai kuwa kutokana na taarifa hizo, mtuhumiwa alipeleka shauri la ugoni katika Mahakama ya Mwanzo Chala.

“Lakini kabla hata shauri hilo halijamalizika, tunashangaa kuona mtuhumiwa ameamua kujichukulia sheria mikononi, baada ya kutekeleza unyama huo alikimbia na kutokomea kusikojulikana,” alisema.

Mtendaji wa Kijiji cha Chala, Godfrey Mwanakatwe alisema kutokana na mazingira hayo polisi wanawashikilia watu wanne kwa kosa la kushiriki mauaji hayo.

Hatua hiyo inatokana na baada ya wao kutoa taarifa kwa muuaji kuwa Nambasita ana uhusiano wa kimapenzi na mtalaka wake, ambaye mpaka sasa haijulikani alipo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, baada ya uchunguzi wa polisi ndugu wa marehemu waliruhusiwa kuuzika mwili huo.

Mwaruanda alisema chanzo cha kifo hicho ni wivu wa mapenzi na kuongeza kuwa mtuhumiwa alianza vizuri kwa kufuata sheria, lakini haijulikani kilichosababisha kuchukua uamuzi huo wa kinyama.

Alisema wanawashikilia watu watatu wakituhumiwa kushiriki mauaji hayo, kwa kutoa taarifa kwa mtuhumiwa kwamba Nambasita alikuwa na uhusiano na mtalaka wake.

Kamanda Mwaruanda aliwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi, hivyo wafuate taratibu kupata haki zao.

Jionee video:Mbunge ataka ichongwe sanamu ya Diamond platnumz iwekwe posta na ile ya askari itolewe.


 Ulanga Goodluck MlingaMay 13 2016 ilikuwa ni zamu ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017. Katika kipindi cha kupokea michango ya maoni kutoka kwa Wabunge, Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga akaguswa na harakati za staa wa Bongo flava Diamond Platnumz…

’Ingekuwa amri yangu tungechonga sanamu la Diamond tukaliweka kwenye mnara wa Askari, ule mnara tumeuchoka. Ametufikisha mbali naameitangaza nchi yetu huko mbele‘

‘Serikali hatuna mpango wowote wa kuwasaidia wanamuziki, wanapenya wenyewe tunaenda kukutana nao mbele na sisi tunajifanya kuwasaidia. Yuko wapi Mr. Nice?,hatujawawekea mfumo mzuri, ninaongea haya nikiyamaanisha’

Unaweza kumcheki kwenye hii video hapa chini…


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu MEI 16 kwenye habari za kitaifa kimataifa udaku na, michezo.


 

Gallery

Popular Posts

About Us