KINGAZI BLOG: 06/03/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Friday, June 03, 2016

Magufuli: Wanaopita Kwenye Barabara za Mwendokasi Chomoeni Tairi za Magari Yao Muuze.

Rais John Pombe Magufuli achukizwa na uharibifu na matumizi mabaya ya miundombinu ya mabasi ya mwendo kasi na kuagiza mamlaka zinazohusika ziwachukulie hatua kwa wasiofuata sheria. Amewataka wachukue magari yao na wapeleke kituoni kisha wachomoe matairi ya watuhumiwa wauze na watakuwa wamepata biashara Msikilize Hapa ...

Nay wa Mitego Anaimba Hip Hop Kama Taarab, Abadilike – Gigy Money

Video vixen machachari, Gigy Money amedai ni muda wa rapper Nay wa Mitego kubadilika kwasababu anachokisikia kwenye nyimbo zake ni taarab na sio hip hop ya ukweli. image Gigy ambaye hapo awali amewahi kuzinguana na hitmaker huyo wa ‘Nasaka Pesa’ baada ya kutumika kwenye video ya Shika Adabu Yako ya rapper huyo na kutolipwa ujira wake, amemuambia mtangazaji wa Jembe FM ya Mwanza, JJ kuwa hip hop...

Wabunge wa CCM wamepinga shinikizo la wapinzani kutaka kumuondoa naibu spika Dk.Tulia

Baada ya June 2 2016  kambi rasmi ya upinzania bungeni kutoa tamko la kutaka Naibu spika wa Tanzania Dr. Tulia Ackson aondolewe madarakani kwa azimio la kuvunja sheria inayoendesha bunge, leo June 3 2016 Wabunge wa CCM wamepinga shinikizo hilo. Wakiongea mbele ya Waandishi wa habari Dodoma, Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu), Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Abdallah Possi ambaye...

MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO.

Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi bungeni mjini Dodoma Juni 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama (kulia)  na Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye wakiteta na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah Bungeni mjini Dodoma Juni...

Basi la mwendo kasi Lagongana na Pikipiki Shekilango Dar es Salaam

Ajali zimeendelea kutokea katika barabara za mabasi yaendayo haraka ambazo zimekuwa zikisababishwa na madereva wasiotaka kufuata sheria za barabarani ambapo leo katika mataa ya kuongozea magari Shekilango basi moja liendalo haraka limegongana na pikipiki. Ajali hiyo ambayo haikusababisha vifo wala majeruhi imetokea majira ya saa sita ambapo kwa mujibu wa mashududa dereva wa boda boda akiwa na abiria...

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA TPDC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Prof. Sufian Hemed BUKURURA kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanzia tarehe 30 Mei, 2016. Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb.), amewateua wafuatao kuwa  Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC kuanzia tarehe...

Profesa Tibaijuka: Wapo Waliochota Fedha za Escrow Lakini Wamenyamaziwa

Jinamizi la kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow bado linamsumbua mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka baada ya kuliibua kwenye semina ya mapambano dhidi ya ufisadi, akichongea wabunge ambao hawajaguswa. Profesa Tibaijuka alipoteza uwaziri wa nyumba, ardhi na makazi kwenye sakata hilo baada ya kubainika kuwa aliingiziwa fedha zinazoonekana zilitoka kwenye akaunti...

Hiki ndicho alichojibu Wema kuhusiana na katuni hii aliyochorwa na mastaa wengine wenye uhusiano na mastaa wanaowazidi umri

Hivi karibuni gazeti moja la udaku liliwachora mastaa wa kike wenye uhusiano na mastaa wa Bongo wanaowazidi umri. Mastaa hao ni pamoja na Jacqueline Wolper aliyechorwa akimnywesha uji mpenzi wa Harmonize anayeonekana akiwa amebeba mdoli. Wengine ni Wema Sepetu akiwa amempakata Idris Sultan, Zari the Bosslady akimweka Diamond kwenye kitolori cha kuwafundishia watoto kucheza na Aunty Ezekiel akiwa...

Aliyewalisha watu nyama ya mbwa azua taharuki!

Akiwa ameshika upaja wa nyama ya mbwa. TANGA: Kitendo cha kijana aliyefahamika kwa jina la Zakaria Swaki, mkazi wa Kijiji cha Mlalo, wilayani Lushoto mkoani Tanga kukutwa na hatia ya kuwalisha watu nyama ya mbwa kimezua taharuki huku wengi wakidai kuwa, kwa hali ilivyo watakuwa hawawaamini wauza nyama. Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, wananchi hao wa Mlalo na viunga vyake walisema...
 

Gallery

Popular Posts

About Us