Baada ya
ripoti ya CAG kutangazwa, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji
Francis Mutungi amevitaka vyama vya siasa nchini kuwasilisha hesabu za
Serikali (CAG) ya mwaka 2014/15 ndani ya siku 90 kabla havijachukuliwa
hatua za kisheria.
Pia
amevitaka vyama hivyo kuheshimu sheria za mashirika ya umma ambazo ni
Sheria ya Ukaguzi wa Fedha za Umma, Sheria ya Fedha za Umma na Sheria ya
Vyama vya Siasa
‘Tulishavikumbusha
vyama vya siasa kuwasilisha bajeti zao, baada ya kupata taarifa ya CAG
hatua inayofuata ni kuangalia taarifa hiyo na kuchukua hatua‘ –Jaji Francis Mutungi
‘Kama
kutakuwa na sintofahamu katika mahesabu ya vyama vinavyopata ruzuku
hatua ni pamoja na kukata kiwango kinachodaiwa, lakini tumewaambia
kwenye barua kuwa wana miezi mitatu ya kukamilisha suala hili‘ –Jaji Francis Mutungi
BOFYA HAPA KUONA VIDEO:ALICHOSEMA JAJI MUTUNGI KUHUSU RIPOTI YA CAG