KINGAZI BLOG: 06/20/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Monday, June 20, 2016

MSANII JUX APATA MAJANGA HAYA


Juma Musa ‘Jux’ na mpenzi wake, Vanessa Mdee ‘V-Money’.

DAR ES SALAAM: Familia ya staa wa Bongo Fleva, Juma Musa ‘Jux’ imeingilia kati ishu ya mwanaume ‘tata’, mkazi wa Dar, James Delicious aliyetangaza kumtaka kimapenzi msanii huyo ambaye ni mpenzi wa Mwanamuziki Vanessa Mdee ‘V-Money’.

Akizungumza na Wikienda kwa niaba ya familia, dada wa Jux, Fatu-ma Juma alisema kuwa hakuna kitu kinachowaudhi kama kijana huyo kutwa kutangaza kumpenda na kumtaka mdogo wao huyo wakati wote ni wanaume na ni kinyume cha maadili ya kidini (familia ya Kiislam), Kitanzania na Kiafrika kwa jumla.

“Kiukweli familia inachukizwa sana na tabia ya huyo kijana ambaye haoni aibu, tunamtaka kuacha mara moja kusumbua watu akitaka namba ya Jux la sivyo tutachukua hatua za kisheria kwani anatukera sana,” alisema Fatuma.

Hivi karibuni kijana huyo alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa lazima ampindue Vanessa kwa Jux kwani anampenda jamaa huyo kupita kiasi.

Kurudiana na Diamond, Wema Aanika Ukweli


Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ enzi za penzi lao.

Stori: Imelda mtema, Wikienda
Dar es Salaam: Vunja ukimya! Tetesi zinazogonga vichwa vya mashabiki wa mastaa wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ zimepata ufumbuzi baada ya mlimbwende huyo kuanika ukweli wa ‘ubuyu’ huo, Wikienda limefanya naye mahojiano maalum (exclusive interview) yaliyochukua dakika 45.

KABLA YA MAHOJIANO
Kabla ya Wema kufunguka mambo mazito juu ya Diamond, uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba, sababu hasa za mashabiki wa wawili hao kuhisi penzi lao limefufuka chini kwa chini ni baada ya Wema kuanza kuwahimiza watu kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, wampigie kura Diamond ambaye anawania Tuzo za BET kwenye kipengele cha Best International Act: Africa, zitakazofanyika nchini Marekani hivi karibuni.

JIUNGE NA WEMA
Wikienda: Mashabiki wako wapo kwenye sintofahamu ya tetesi za wewe kurudiana na Diamond. Je, ukweli ni upi?
Wema: (kicheko cha kukata na shoka hadi machozi) hivi kwa nini kila ninapokutana na mtu lazima aniulize kuhusu mimi kurudiana na Nasibu (Diamond)?
Wikienda: Sasa hapo ndiyo ujue lisemwalo lipo na kama halipo laja, hebu eleza hili likoje?

Wema: Kwanza kabisa mimi sasa hivi nimekua. Utoto nimeuweka kando, sihitaji tena bifu zisizokuwa na maana na hata ukiangalia ni kitu gani tulichogombania, hakuna hivyo kuna wakati unafika lazima mtu ubadilike kabisa tena kwa kipindi kama hiki cha mwezi mtukufu.
Wikienda: Kuna mtu yeyote alikushauri kuanza kuposti watu wajitoe kumpigia kura Diamond?

Wema: Hakuna, mimi niliongozwa na hisia zangu kwa sababu hata hivyo sipendi kupelekeshwa na hisia za watu au watu wanasema nini, inatakiwa ifike kipindi nifanye vile moyo na akili yangu inavyotaka.
Wikienda: Unajua kuna kitu kinaitwa timu, yaani kati yako na Diamond. Vipi kwa upande wako hawajakujia juu kuhusu kuwataka mashabiki wampigie kura Diamond kwa sababu mara nyingi timu zenu huwa zinatukanana?

Wema: Kwanza hilo ndilo nataka kuliweka wazi, sasa hivi sitaki kuendesha maisha yangu kupitia timu kwa sababu mwisho wa siku mimi nina maisha yangu na wao wana maisha yao, yaani mpaka vitu vingine vinakera kwa sababu mtu unatakiwa kufanya kitu kinachotoka ndani ya moyo wako siyo kusikiliza watu wanataka nini.
Wikienda: Kwa hiyo unaona timu ndizo zinachochea ugomvi wenu?

Wema: Kabisa kwa sababu inatokea wakati anatukanwa Diamond, mtoto wake (Tiffah) na mkewe (Zari) kiukweli naomba kusema wazi mimi sipendi na mara nyingi naonekana kama mimi nimewatuma. Aisee sipendi kabisa hali hiyo na ninaomba timu zipunguze kutukana watu siyo vizuri.
Wikienda: Unafikiri timu imekusababishia matatizo?

Wema: Siyo kwangu tu hata kwa Diamond. Hatuishi maisha ya kwetu, tunafuatisha timu. Labda niseme kwamba mimi ni shabiki namba moja wa nyimbo za Diamond lakini kiukweli hata ukitaka kuimba wimbo unajificha yaani maisha hayo sitaki tena kwa sababu hata nje ya uhusiano wa kimapenzi tuliokuwa nao huko nyuma  mimi ni shabiki mkubwa wa nyimbo zake, sasa kwa nini nibane hisia za kitu nikipendacho?

Wikienda: Kwa hiyo kinyongo ulichokuwa nacho nyuma sasa hivi huna tena?
Wema: Yaani mimi nimesafisha nia kabisa, sina tatizo na yeye kwa sababu najua inawezekana hata yeye anatamani kuniuliza kitu inashindikana au anahitaji kufanya kazi na mimi inakuwa ngumu kitu ambacho ni mambo ya kizamani kabisa.

Wikienda: Mara ya mwisho kuwasiliana na Diamond ni lini?
Wema: Niliwasiliana na Diamond tena kwa kumtumia meseji kipindi f’lani mama yake alikuwa anaumwa. Kiukweli kama mapenzi yalikwisha zamani sana. Yeye akaendelea na maisha mengine na mimi hivyohivyo.
Wikienda: Ukipata nafasi ya kukutana naye ili mfanye kitu kwa ajili ya mashabiki wenu inawezekana?

Wema: Kama nilivyosema awali, kwa upande wangu mimi sina tatizo lakini najua kabisa kuna vitu Diamond anavifanya vibaya kwangu ili kunizibia sehemu f’lanif’lakini sasa hiyo inanionesha nini kwa Diamond? Amekuwa kimuziki lakini siyo yeye mwenyewe, kuna kipindi namuonea huruma sana kwa mambo yake, natamani hata nimwite tukae chini na kumwambia kuwa yeye ni wa kimataifa hivyo mambo ya Kiswahili hayana nafasi tena kwake.
Wikienda: Kwa hiyo mtu akiwakutanisha mzungumze upo tayari?

Wema: Bila tatizo lolote, mambo ya matashititi hayahitajiki kwa sasa na hayana nafasi kwani imefika kipindi watu tumekua na maisha yanaendelea kwa sababu siwezi kumfikiria tena kimapenzi.
Katika mahojiano hayo, Wema alidai kwamba kuna mambo mengi ambayo Diamond amekuwa akimfanyia umafia hivyo tetesi kuwa amerudiana naye hazina ukweli wowote na kwamba haitatokea.

DIAMOND ATAFUTWA
Jitihada za kumpata Diamond ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa, kutumiwa ujumbe bila kujibu na kufuatwa ofisini ambako hakuwepo hivyo jitihada zinaendelea.

TUJIKUMBUSHE
Wema na Diamond ni wapenzi waliokuwa gumzo miaka miwili iliyopita kutokana na kuachana na kurudiana hivyo mashabiki wao wamekuwa wakiamini ipo siku watarudiana.

Njia rahisi 8 za kupata ajira popote ukiwa umemaliza chuo hizi hapa

Kutoka mwaka 2012 hadi 2015, kipindi cha miaka 3.. Nimeajiriwa na kampuni 7, full time, mshahara mzuri tu. Cha kushangaza hamna kampuni hata moja ambayo imewahi kusisitiza nioneshe cheti, baadhi huwa wanaulizia ila nikiiingia kwenye interview hua napita hadi wanasahau kuhusu cheti. Baada ya kuacha kazi yangu ya mwisho (sijawahi kufukuzwa, naacha mwenyewe) nime pata offer ya kazi zaidi ya sehemu 12, from August 2015 hadi June 2016 kipindi nnapoandika post hii, kwa sahivi nina kampuni 2 ambazo bado changa ila kwa pamoja zinaniingizia pesa kwa mwezi mara 5 kuliko kazi yoyote nliyowahi kufanya. 

So kwanini naandika hii post? Watu nliomaliza nao form 4, mwaka 2009. Ndio wamemaliza chuo wengi wao mwaka jana(2015). Wengi either hawana kazi na wanatafuta au wamekwama kwenye kazi inaowalipa mshahara mdogo sana. Waliofanikiwa kupata kazi ni wale ambao wazazi wao wana connections, ambao baada tu ya kumaliza wameweka kwenye kitengo ambacho hawapendi ila inabidi tu wawepo. Na marafiki wengine kibao wanalalamika kua kupata ajira ni vigumu.. kupata ajira ni vigumu... so kwa kifupi tu ntaandika point chache, ambazo mtu yeyote akizifanyia kazi utapata employment almost any company you apply for, utakua na offer za kazi nyingi unachagua tu, na kila mwaka ukipenda utakua mshahara wako unapanda tu. 

Toka nimeacha kazi nimepata offer za kazi kampuni kubwa kama clouds tv, star times, aggrey & clifford, na kampuni zingine ambazo siwezi kuzitaja maana walio ni offer wananifahamu vizuri. Na nikiwa na mda ntaandika zaidi kuhusu historia ya kazi zangu na kwanini niliacha kazi kote huko, actually kuna this one place i was employed (sija include kwenye hizo kampuni 7 nilizofanyia kazi) hii kampuni niliacha kazi baada ya siku 3, mwajiri akaniita mara tatu ofisini kwake kuniomba nibaki na ku offer kuniongezea mshahara mara 3 (kutoka laki 3, ikaongezeka hadi laki 5 na 50) lakini bado nikaacha hiyo kazi after 3 days (kumbuka hapa sina cheti hata kimoja, hata cha form 4 nilikua sijachukua kwa kua sikumalizia ada). 

Ukweli kuhusu cheti ni kwamba kuna sehemu na sehemu kinahitajika kama kuwa daktari, ama mwanasheria ila most of the jobs watu wanazotafuta na hawapati, vitu vinavyohitajika ni uwezo wako tu wa kufanya kazi, ntakuelezea jinsi ya kuonesha huo uwezo. 

Anyway enough chitchat... Below ni njia ambazo ukitumia utapata kazi unayotaka almost anywhere. 

1) How to battle the experience factor (Jinsi ya kupambana na wanaotaka uwe na experience kabla ya kazi) 

This is the easy one, hapa pa rahisi kinoma.. itakuchukua mda kama miezi sita or less (inategemea na ufanyaji kazi wako) lakini kupata experience kabla ya kuanza kazi ni muhimu, siri ya hapa' experience sio lazima uwe umeajiriwa before, wengi wanasema hivi, ila ukifuata hii njia ntayokutajia utapita na experience yako utayoipata. Ukimaliza chuo tu achana na watao ungua jua kutafuta kazi, tafuta experience kwanza. 

-Jitolee bure kabisa popote, usiombe ulipwe. hamna ataekataa wewe kujitolea, for example unafanya accounts, tafuta ndugu yeyote mwenye kampuni yoyote "iliyosajiliwa" 

jitolee bure, mueleze unatafuta experience so utafanya kazi bure yoyote siyo lazima iwe hata ya accounts we mwambie utafanya yoyote. Kama huna ndugu jipangie ratiba kuingia ofisi yoyote (chagua tatu kwa siku) na waambie the same. Ukiwa smart siku ya kwanza tu unapata (If needed ntaandika how to aproach any situation bila kukataliwa... someday). 

-So umeomba umepata, usikwame hapa fanya hii kazi maximum miezi miwili kwa nguvu zako zote. kama mda wa ofisi saa mbili, wewe saa moja upo pale, kama mda wa kutoka saa kumi na moja wewe upo hadi saa moja usiku. ila baada ya mwezi mmoja au miwili acha, wape sababu yoyote iwe nzuri lakini (nahama mkoani, narudi shule, ila usidanganye sana), what is important ni kuondoka in good faith na uwe na contacts za mmoja au wawili wa hiyo kampuni (ntaelezea kwanini baadae). Najua wengi watataka kukupa kazi wakiona ufanyaji wako wa kazi, ukitaka chukua ila ndo itakua mwisho wako huo, siku unaachishwa for any reason huna sehemu ya kwenda. i sudgest acha hiyo, move on to the next one. So Rudia hii process mara 3 hadi 6 for better results... 

-Siri ya hapa ni kuonekana kama umefanya mda mrefu, usianze mwanzo wa mwezi, nenda mwezi wa nne tarehe 15 hadi mwezi wa tano tarehe 15, hapa itaku aumefanya miezi miwili. au nenda mwezi wa nne tarehe 25 hadi mwezi wa sita tarehe 2, hapa umefanya miezi mitatu (kwenye CV, under experience unaandika intern from June -August). Kuna njia nyingi unaweza uka stretch kazi ya siku 90 kuwa una experience zaidi ya mwaka mmoja ambazo nikipata mda ntaelezea. 

{side note: usiombe hela yoyote ukiwa kwenye kipindi hiki, sijui utapataje hela ila figure it out, but most of the time kama percent 80 hivi ya sehemu utapoomba kujitolea utapewa hela za kula na nauli baada ya wiki tu ya kuona ufanyaji wako wa kazi} 

Ukimaliza kujitolea kampuni zako 3 –6.. Hii ni experience tosha, huhitaji yoyote nyingine. With this alone ukienda enterview 5 utapata kazi sehemu moja wapo guaranteed. Important sasa ni kuweka your contact kwenye kila kazi ulipofanya (namba za wahusika kila kampuni) na lazima uwe umeacha kwa good terms incase wakipiga utasifiwa sana, hawajawahi kupiga in my case ila mtu mmoja nilimpa hii njia wakapiga simu. 

Also hizi kampuni utaziandika under experience kwenye CV yako, kwenye format ifuatayo 

[​IMG] 

(n.b these are samples) 

2) Kampuni inapenda "the multitasker" (mtu anaeweza kufanya vyote) 

Again this is very easy hata sijui kwanini watu hawa apply. Kwenye CV yako always have a section ya "other skills" or kitu kingine kama hiki kinachoweza onyesha skills zako zingine. Kwa mimi other skills nikikuonyesha CV yangu imejaa page nzima moja... Ukiulizwa kwanini, wewe sema unapenda sana kujifunza, na kuwa haulali siku bila kujifunza kitu kipya (hii inabidi iwe kweli kwa ushauri wangu, jifunze kitu kipya kila siku, but for the purpose of this post achana na hilo). 

Unapataje other skills? Well tupo kwenye ulimwengu ambao ni rahisi sana kujifunza chochote. Best source nnayotumi ni youtube. YouTube ni mtandao wa video wenye kila kitu utachoweza kufikiria wewe... as long as its legal kipo humu ndani, wewe jifunze chochote then andika kwenye other skills. Vitu kama photo editing kwenye photoshop' unaweza ukajifunza ndani ya siku mbili, basic za ku edit picha kwenye photoshop, alafu kwenye CV andika "Basic skills in photoshop editing". Ndo rahisi kihivyo, believe me kama hau apply kwa ajili ya graphics hutotumia hiyo photoshop skill, 98% ya other skills huto kuja kuzitumia hata mara moja. 

Mfumo wa kuandika kipengele cha other skills ni as follows 

[​IMG] 

(n.b always know the basic of the skill unayoandika, na uandike kweli unavyoweza hiyo skill, kama ni basic tu andika beginner, also nikipata mda ntaandika skills rahisi ambazo unaweza kujifunza na wapi unaweza jifunza fast) 

3) Cha kufanya kabla ya interview (Muhimu) 

Hapa sasa umetuma CV yako na umeitwa kwenye interview, kwa mimi sijawahi kwenda kwenye interview na nikakosa kazi niliyoitwa, kuna mda nikawa nafanya kama test tu niende alafu nione kama ntapata, alafu napata. kuna mtu nlimpa hizi njia akatumia sehemu tatu, sehemu mbili akaitwa aanze, akaishia kuchagua tu wapi atalipwa zaidi. 

I) Fanya Research ya hiyo kampuni unayo apply.. Chukua siku nzima kufanya research ya hiyo kampuni siku moja kabla ya kwenda kwenye enterview, ujue ni nini inahitaji, kwanini wanataka ajiri, nini kimekosekana. Kampuni inaajiri ili either kuziba pengo au wanaona kuna upungufu flani kwenye kitengo husika. So hawatoi ajira ili kukusaidia wewe upate kipato, THIS IS VERY IMPORTANT . Narudia, kampuni hai ajiri ili kukusaidia wewe upate kipato au usolve matatizo yako, ina kuajiri ili ku solve matatizo yao. 

So kamwe usiende kwenye interview ili kujielezea wewe, DO NOT DO THIS. Kosa ndo hapa kubwa, hii ndo sababu kwanini haupati kazi kama una tafuta, mtu anaenda enterview ili kujielezea sijui "mimi ni mchapakazi, mimi naweza ABC...... achana na hayo.... 

Inabidi useme vitu kama "naona kuna ukosefu kwenye sector ya customer care kwa kipindi cha miezi sita, na kampuni ikitoa customer service nzuri ndo wateja wanaiamini, so mi naweza nikasaidia kampuni yako kwa kufanya ABC" This is the right way. This alone will get you the job kama ukiweza fanya research vizuri na kuona nini kimekosekana. 

kuna siku kulikua na kazi ya social media marketing, nilitafuta hadi mtu ambae anafanya kazi kwenye kampuni husika na kumuuliza kampuni inahitaji nini, akaniambia "ni kweli wamesema wanatafuta mtu wa ku manage social media, ila ukweli wanahangaika sector nzima ya marketing"… long story short nilifanya kazi hapo kwa miezi minne kama marketing manager. 

4) Fanya kazi unayo apply kabla ya kuajiriwa 

Hii na prefer kufanya baada ya interview, kama wewe ni project manager (mfano) na ndio una apply for kazi ya u manager, tafuta njia ya kuonyesha uwezo wako kabla haujaanza kazi, kitu kama andaa report then mtumie boss. Au kama wewe ni marketing, ukitoka tu kwenye enterview nenda katafute mteja kwa ku market hiyo kampuni, au andaa marketing plan. Hii step ndio ngumu kwenye baadhi ya sector. Lakini hii ndio wazungu wanaiita "nail in the coffin". 

Ukiweza fanya kazi kabla ya kuajiriwa muajiri kama amekwama kwenye kuchagua watu watano na wewe mmoja wao, lazima atakuchagua wewe kwa sababu ameona uwezo wako, wengine wote walipo hapo hajui uwezo wao, lazima atakupa hata mwezi mmoja wa trial. Mwezi mmoja unatosha kabisa kumfanya akupe mkataba wa mwaka au zaidi. 

Ukiweza kwenda na kazi ambayo unataka kupewa, uwe umeshaifanya then interview ikiisha tu unamuonesha, unaweza ukapewa kazi hapohapo. Especially kama umefuata maelezo yaliyopita ya hapo juu. imenitokea more than once, kuna watu nje wanasubiri kufanyiwa enterview ila muajiri ananiuliza mimi naweza anza lini. 

-------------------------------------------------------------------------------------

Okay... nmechoka kuandika.... this post imekua ndefu kuliko nilivyotegemea.. Na mda unaenda I have a lot to do. So naishia nusu kwa sasa.. Kwa ataehitaji niendelee tafadhali nijulishe kwa kuacha comment hapo chini, na kama una swali lolote pia uliza ntajitahidi kujibu. Kuna mambo mengi sana, kama ya kupata mshahara mwingi zaidi ya wanaotaka wakupe bila kuwaomba, na pia njia za kufanya kazi kampuni zaidi ya moja kwa wakati mmoja, promotions na mengine for next time. 

Nimeshasaidia watu wachache kupata kazi, I hope hii itamfikia mtu husika na kumsaidia yeye pia kupata kazi yake anayo ihitaji. Sijawahi kutumia cheti hata mara moja kupata kazi na wala nikitafutwa kupewa kazi sijawahi ulizwa kuhusu cheti natafutwa kisa I am the most qualified person ya hiyo sector wanaemjua (ukweli ni kwamba kuna wengi zaidi who are more qualified) ukitumia hizi njia vizuri utapata kazi yoyote unayoitaka mostly kwenye private sector, ila I was offered kazi hadi serikalini for 900,000 (laki tisa) + gari la kutembelea na sehemu ya kuishi, nikakataa. This too ni maongezi ya siku nyingine. 

Kwa ataekua ana wonder mi nipo kwenye sector ya I.T, ila nmesaidia watu wa accounts, project management, H.R, presenter pamoja na marketing executive kupata kazi in a very short time, ukitumia hizi njia vizuri hautokosa ajira, this is a fact. 



source JAMII FORUM

Wastara Aamua Kuachana na Uigizaji

Dar es Salaam: Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amejipanga kuachana na uigizaji na kufanya ishu nyingine ikiwa ni pamoja na biashara ambazo ameanza kuzifanya.

Akizoza na Wikienda, Wastara alisema kuwa anamalizia kazi ya uigizaji mwaka huu na mwaka unaokuja atakuwa mwingine kabisa kwani baada ya kufika nchini Msumbiji (aliko kwa sasa) amepata dili lingine zuri ambalo ataliweka wazi baada ya mipango yake  kukamilika.

“Kinacho niachisha uigizaji si biashara tu bali ni pamoja na dili nililolipata huku Msumbiji, kama litakwenda nilivyopanga, nitaliweka wazi inshallah,” alisema Wastara.

Hivi karibuni, Wastara aliripotiwa kuwa na ujauzito ambapo alikimbilia nchini Msumbiji.

GIGY MONEY AELEZA JINSI MWARABU WAKE ALIVYOMSITIRI

IKIWA imepita wiki moja tangu ‘muuza nyago’ kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kugundulika kuwa ameangukia katika penzi la mwanaume wa Kiarabu aishiye Dubai, Aziz, staa huyo amefunguka kuwa amemsitiri vitu vingi.
Akizungumza na mwandishi Gigy ambaye pia ni Mtangazaji wa Choice FM katika Kipindi cha Admin alisema kuwa kila binadamu anapangiwa mtu sahihi wa kuishi naye na kwamba kuangukia kwenye penzi na Mwarabu huyo kumemfanya kuachana na mambo mengi aliyokuwa akiyafanya kama kujianika kihasara katika mitandao ya kijamii na kutoa lugha chafu hovyo.
“Kiukweli kabisa, Aziz (Mwarabu) amenisitiri sana, zamani ulikuwa hunikuti hivi, japokuwa yupo mbali (Dubai) lakini kila siku nachati naye, ananipigia simu na anahakikisha sifanyi mambo ya kijinga,” Alisema Gigy.
Gigy anayedaiwa kutoka na msururu wa wasanii wa Bongo Fleva wakiwemo Ommy Dimpoz, Rich Mavoko, Alikiba na Hemed PHD alimnasa Mwarabu huyo miezi sita iliyopita kupitia Instagram ambapo walianza kwa kutumiana picha kisha namba za simu.

Breaking News: Basi la NBS latapa ajali mbaya Gairo

Basi la NBS linalotoka DAR kwenda TABORA limepata ajali mbaya maeneo ya Gairo, inasemekana kunawatu wamelaliwa na Basi hilo na mpaka sasa haijajulikana watu wangapi wamefariki Dunia na waliojeruliwa..

Tunaendelea kufatilia tukio hili kwa ukaribu zaidi na tutakujuza mdua sio mrefu kila kitakacho jili..






source :Muungwana blog

Kim Kardashian kumnusuru auza makalio kwenye ‘gift paper’


Kim Kardashian.

NEW YORK, MAREKANI

KISTAAJABU ya Musa! Mwanamitindo na Mtangazaji wa Kipindi cha Keeping Up With The Kardashians, Kim Kardashian ameamua kujikita kwenye ujasiriamali ambapo hivi karibuni aliibuka na biashara ya kuuza makalio yake kwenye karatasi za zawadi ‘gift paper’.


Makalio yake kwenye karatasi za zawadi ‘gift paper’.

Kim (32) ambaye ni mama wa watoto wawili, North na Saint aliozaa na rapa Kanye West, alianzia ujasiriamali kwa kutengeneza gift paper zikiwa na picha mbalimbali za sura zake, mumewe na mtoto wake, North.

Inaelezwa kuna kipindi alitengeneza gift paper zenye jina la Bae ambazo zilitumika kwa wingi kwenye harusi ya mwanamitindo, Lorraine Shwartz ambazo huziuza kwa Sh. 76,300.

 

Breaking News: Wabunge wa Upinzani Waziba Midomo yao Kwa Karatasi na Plasta na Kisha Kutoka Nje


Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni leo wametumia mtindo mpya kueleza hisia zao baada ya kuamua kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakiwa wamejifunika midomo kwa karatasi.

Hii ni wiki ya pili mfululizo wabunge hao wamekuwa wakitoka bungeni baada ya kutangaza kutohudhuria kikao cha bunge kinachoongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema wameamua kutumia mtindo huo mpya kwa sababu Bunge limekataa kuwasikiliza hoja zao.

Askofu Gwajima atoa Tamko


Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, jana walisali bila kuwapo kwa Askofu wao, Josephat Gwajima ambaye anatafutwa na Jeshi la Polisi. 

Mara nyingi Jumapili, Gwajima ndiye amekuwa akiongoza ibada katika kanisa hilo lililopo Ubungo Kibo, lakini jana iliongozwa na mchungaji Edward Adriano ambaye hata hivyo, hakueleza chochote kuhusu alipo askofu huyo.

Gwajima anatafutwa na polisi baada ya kusambaa kwa sauti inayosikika kama yake akitaka Rais mstaafu, Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake.

Jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema suala la Askofu Gwajima atalizungumza leo.

Alhamisi iliyopita Polisi walizingira nyumbani kwa Gwajima kwa saa saba, wakitaka kumkamata bila mafanikio.

Kamanda Sirro alisema wanamtafuta askofu huyo ili athibitishe kama maneno yenye uchochezi, yanayosambaa kwenye mitandao ni ya kwake.

Ulinzi kanisani 
Ulinzi katika kanisa hilo jana uliimarishwa na vijana waliovaa vizibao vya njano, vilivyoandikwa polisi jamii tii sheria bila shuruti. Idadi ya vijana hao wanaokadiriwa kufika 40, walikuwa wengi kuliko Jumapili nyingine zilizopita.

Licha ya kutokuwapo kwa askofu huyo kanisani hapo, waumini walijaa na wengine kukosa viti huku wengine wakionekana kusimama nje ya kanisa hilo.

Kauli ya  Msaidizi wa Gwajima

Msaidizi wa Askofu Gwajima, Yekonia Bihagaze, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, alisema juzi kuwa taratibu, sheria na kanuni zinapaswa kufuatwa kumkamata kiongozi wao.

"Kanisa la Ufufuo Na Uzima ni makini, tulivu na halikurupuki kwenye maamuzi yake. Na nchi haiongozwi mitandaoni, kama serikali inamtaka mtu ziko taratibu, sheria kanuni za kuzifuata," sehemu ya taarifa ya Mchungaji Bihagaze ilisomeka.

"Kwa sasa kila mmoja anaona nchi inapiga hatua kimaendeleo, ni vema wananchi sasa tukaachana na propaganda kama hizi, ni vema tukaweka shabaha yetu moja kushirikiana na Rais tulijenge taifa Letu. Taifa hili si mali ya mtu mmoja, ni mali yetu sote kwa manufaa yetu na vizazi vingine vitavyokuja.

"Adui wa Rais wetu awe adui yetu sote. Siasa zitakuja tu baadaye ila kwa sasa nchi itulie, watu tuchape kazi, tulipe kodi kwa sababu kuna Rais mwenye nia ya kuipeleka mbele.

"Hakuna duniani Taifa linaloweza kuendelea pasipo wananchi kushirikiana bega kwa bega na kiongozi wao."

Serikali yaamua kusitisha Ajira Zote Kwa Muda



SERIKALI imesitisha ajira zote, kama njia ya kukabiliana na wimbi la watumishi hewa.

Kutokana na uamuzi huo hivi sasa hakuna nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa Serikali na wakala zake pamoja na utoaji wa vibali wa likizo ya bila malipo.

Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro,  jana alisema kuwa Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa ajira, ili kupitia upya muundo wa Serikali na taasisi zake.

Alisema utekelezaji wa mkakati huo utakwenda sambamba na kusitisha kwa muda utoaji wa vibali vya ajira zote mbadala pamoja na uidhinishaji wa ajira hizo zilizopo Sekreterieti ya Ajira katika utumishi wa umma na kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi.

“Ni kweli tumesitisha kwa muda ili kupitia mfumo wa Serikali na hata kuangalia ulipaji wa mishahara kama upo katika malipo stahiki.

“…na hili litakwenda sambamba na hata kusitishwa malipo ya mishahara yanayotokana na upandishwaji wa vyeo kwa watumishi. Tukimaliza zoezi hili ndipo tunaweza kuanza kutoa ajira za Serikali,” alisema Dk. Ndumbaro.

Alisema muundo mpya wa utumishi wa Serikali unakwenda sambamba na uhakiki wa malipo ya mishahara, hivyo ni lazima ujue ni nani unayemlipa kuliko ilivyo sasa.

Kwa mujibu wa maelekezo hayo uhamisho na uidhinishaji katika mfumo wa watumishi ambao wamehamishwa kutoka kwa mwajiri mmoja kwenda kwa mwajiri mwingine ambao atalipwa mshahara mkubwa kuliko ule wa sasa pia utaangaliwa kwa lengo la kupata taarifa sahihi za mtumishi husika.

“Baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki watumishi pamoja na tathmini ya muundo wa Serikali na taasisi zake, wote wataarifiwa ni lini utekelezaji utaendelea,” alisema.

Taarifa kutoka maeneo mbalimbali nchini, zinaarifu kuwa maelekezo hayo yalitolewa Juni 13, mwaka huu na kusambazwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa makatibu wakuu wote, makatibu tawala wa mikoa, kwa wakuu wa idara za Serikali zinazojitegemea.

Waliotakiwa kutekeleza maelekeo hayo ya Serikali ni wakurugenzi wote wa majiji, manispaa na miji, wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya, watendaji wa taasisi za umma na watendaji wa wakala za Serikali kwa upande wa Tanzania Bara.

Kamatakamata

Wiki iliyopita vyombo vya dola vilianza kuwatia mbaroni watumishi hewa kwa kuwafuata na pingu majumbani.

Hatua hiyo imetajwa kuwa ni mkakati wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli, kuanza kupambana na watendaji ambao wamekuwa wakiisababishia hasara Serikali ya kulipa mamilioni ya shilingi kwa watumishi hewa.

Kutokana na uamuzi huo  ambapo mtumishi mmoja wa moja  za Mkoa wa Kigoma, alifuatwa na askari wa polisi na kutiwa mbaroni nyumbani kwao Ubungo Kibangu jijini Dar e Salaam.

Tukio hilo la aina yake lilitokea mchana wa juzi na kuibua hisia miongoni mwa majirani ambao waalisema kuwa, askari hao walifika nyumbani kwao na mtumishi huyo na kumfunga pingu mikono na miguuni na kuondoka naye.

Kutokana na hekaheka hiyo ya watumishi hewa, taarifa kutoka wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, zilidai kuwa walimu watano wastaafu nao walikamatwa na polisi kwa madai ya kupokea mishara hewa.Mbali na walimu hao pia alikuwepo muuguzi mmoja.

Hivi karibuni akizungumza Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki, alisema Serikali imewaondoa jumla ya watumishi 12,246 kwenye mfumo wa malipo ya mishahara kwa sababu mbalimbali, ikiwemo umri wa kustaafu kwa lazima, kufukuzwa kazi, vifo na kumalizika kwa mikataba.

Waziri Kairuki alisema kuondolewa kwa watumishi hao kumeokoa Sh bilioni 25 ambazo zingelipwa kwa watumishi hao.

Alisema kuwa fedha hizo zingepotea endapo watumishi wasingeondolewa kwenye mfumo, ikilinganishwa na watumishi 10, 295 walioondolewa kwenye mfumo kuanzia Machi 15 hadi Aprili 30 mwaka huu.

Alisema pia kuwa watumishi hewa 1,951 wameongezeka ikiwa ni pamoja na Sh bilioni 1.8.

Alifafanua kuwa ofisi hiyo ilitoa maelekezo kwa Makatibu Wakuu, Wakuu wa taasisi za umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuwasilisha taarifa ya watumishi hewa ifikapo Juni 10, mwaka huu. 

Chanzo: Mtanzania

HAYA HAPA MAGAZETI YA TANZANIA YALICHOANDIKA LEO TAR 20 JUNE 2016 KWENYE HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO.

Karibu ,tunakuletea kilichoandikwa kwenye magazeti ya Tanzania leo June 20 kwenye habari za kitaifa kimataifa michezo na stori nyingine kali usiache kukaa na si kupitia facebook kwa kulike Page yetu na pia kutufollow kupitia twitter@tanzaniampyasasa.

Albamu ya Beyonce 'Lemonade' yashtakiwa


Image copyrightREX
Image captionBeyonce
Albamu mpya ya Lemonade iliotolewa na Beyonce Knowles imeorodheshwa miongoni mwa albamu zilizopendwa sana baada ya kutolewa mwaka huu,lakini ,kipande cha albamu hiyo kilichotolewa wiki moja kabla ya uwepo wa albamu hiyo kufichwa hadi wakati wa toleo la filamu fupi lililoandamana na albamu hiyo kimezua utata.
Kipande hicho cha albamu hiyo kilishirikisha msururu wa vipande vifupi vifupi vya albamu hiyo bila maelezo ,vingi vikimuonyesha Beyonce na kumalizika kwa maelezo yaliosema :Lemonade A world Permier event.
Na sasa mtengezaji huru wa filamu kwa jina Matthew Fulks anadai kuwa kipande hicho kilinakili mojawapo ya kazi zake kwa jina Palinoia.
Fulks anadai kwamba kampuni ya muziki ya Sony ile ya Columbia Recordings pamoja na ile ya Beyonce Parkwood Entertainment zilijua kuhusu kazi yake kabla ya utengezaji wa Lemonade ulipoanza na kwamba walishawishiwa na kazi yake.
Anasema kuwa kipande hicho cha albamu ya Lemonade kinafanana na kile cha Palinoia ambayo ni kazi yake.
Anaongezea kuwa baadhi ya vitu vinavyofanana kati ya filamu hizo mbili ni pamoja na michoro katika ukuta,watu wenye macho mekundu na picha zilizopigwa katika ngazi pamoja na eneo la kuegesha magri chini ya nyumba.

Wasiohudhuria vikao vya bunge TZ hawatalipwa


Image captionBunge la Tanzania
Wabunge wa upinzani nchini Tanzania ambao wamekuwa wakikosa kuhudhuria vikoa vya bunge kwa karibu wiki ya pili mfululizo, hawatalipwa marupuupu yao wakati wa kipindi hicho, hadi pake watakapoanza kuhuduria vikao.
Naibu spika Dr Tulia Ackson alitoa tangazo hilo kaumbatanana uamuzi wa awali ulitolewa na spika wa bunge mwaka 2008 wakati wabunge kutoka chama cha CUF walichukua hatua ya kususia vikao vya bunge.
"Kama waakilishi wa watu, tunahitaka kuhudhuria shughuli za bunge badala ya kujisajili na kuondoka kufanya mambo ambayo hayana mahusiano na bunge". Alisema Dr. Tulia wakati akitoa tangazo hilo.
Wabunge kutoka upinzani wakiwemo wale kutoka vyama vya Chadema,CUF na NCCR, wamekuwa wakisusia vikao vya bunge tangu tarehe 30 mwezi Mei mwaka huu, wakati naibu spika aliwaamrisa waondoke bungeni baada ya kukiuka amri zake.


Vyakula 7 vizuri kwa kuongeza nguvu za kiume kikamilifu



Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.
Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster". Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.

Sababu za kukosa nguvu za kiume

 Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema, utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani?
Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:
  • Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
  • Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
  • Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume

Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda mahusiano na ndoa.

1. Blueberry


Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume. Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.
Soma piaNjia 7 za kuongeza uzito

2. Mtini (Figs)


Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.

3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)


Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.
Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.

4. Karanga

 
Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.

5. Vitunguu saumu


Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.
Soma pia: Jinsi afya ilivyo muhimu kwako

6. Ndizi


Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).

7. Chocolate


Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.
Soma piaJinsi mihogo ilivyo hatari kwa afya yako

Vyakula ni bora kuliko madawa makali

Mie binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako yote ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.
Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko, lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri uangalie jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa kupanda mtungi, ruksa kuangalia njia mbadala.
Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi, kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa makini.
Kama ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni vizuri ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa mara ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni hapo chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua tatizo la nguvu za kiume.
 

Gallery

Popular Posts

About Us