KINGAZI BLOG: 07/21/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, July 21, 2016

BREAKING NEWS!!! Taarifa Kwa Umma Kutoka Wizara Ya Elimu




Rais wa Uturuki Atangaza Hali Ya Hatari kwa miezi mitatu

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan ametangaza hali ya hatari itakayodumu kwa miezi mitatu ili kutoa nafasi kwa mamlaka kuchukua hatua stahiki dhidi ya wanaoshukiwa kushiriki mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa juma lililopita.

Erdogan, ambaye alianzisha hatua ya kamata kamata katika taasisi mbalimbali tangu baada ya mapinduzi yaliyoshindwa, amesema hatua hiyo inazingatia katiba ya Uturuki na hajakiuka utawala wa sheria wala uhuru wa raia wa Uturuki.

Hali ya hatari, ambayo itaanza kutekelezwa mara tu baada ya kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali , itamruhusu Rais na Baraza kufanya kazi za bunge kupitisha sheria mpya na kuweka  mipaka au kusimamisha kwa muda baadhi ya haki na uhuru wa raia inapolazimika kufanya hivyo.

Erdogan alitoa tangazo hilo akiwa kwenye matangazo ya moja kwa moja kwa njia ya Televisheni mbele ya mawaziri wa Serikali baada ya mkutano wa baraza la usalama la Taifa.

Katika hatua nyingine, Majerali wa jeshi wameshtakiwa rasmi wakihusishwa na mapinduzi ya juma lililopita, pia imetangazwa kuwa majaji wa kijeshi na waendesha mashtaka wanafanyiwa uchunguzi.

Hata hivyo mamia ya shule na taasisi za kielimu zimefungwa.waalimu na wana taaluma ni sehemu ya maelfu ya wanajeshi, wafanya kazi wa umma na wengine wanaoshukiwa kuiangusha serikali, mpango unaodaiwa kuongozwa na Kiongozi wa Kidini aishie uhamishoni nchini Marekani, Fethullah Gulen.

Wanafunzi hawa wanaeleza hatua hii ina maana gani kwa mustakabali wa maisha yao.


Ali Kiba na Baraka Da Prince Wavamiwa na Majambazi Sauz

WANAMUZIKI wawili maarufu nchini Ali Kiba na Baraka Da Prince wanaosimamiwa na lebo ya Rockstar 4000 jana Julai 20, 2016 walivamiwa na majambazi saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki wakiwa safarini nchini Afrika Kusini.

Managementi inayowasimamia wasanii hao ya Rockstar 4000 imesema wasanii hao walivamiwa wakiwa kwenye kikao cha mikakati ya kuzungumzia safari yao nchini humo watakakokaa kwa muda wa siku saba.

Chanzo hicho kimesema majambazi hao walikuwa na silaha za moto (bunduki).

Miongoni mwa vitu walivyoibiwa ni pamoja na simu zao za mkononi ambapo majambazi hao wakati wote wa tukio waliwanyooshea bunduki kina Ali Kiba kuwatisha zaidi na bila kutaka kupoteza muda.

Baraka Da Prince na Ali Kiba wote ni wazima wa afya na hawakudhurika kwenye hilo tukio.

Pamoja na tukio hili kutokea, wasanii hao hawatorudi nchini bali wataendelea na mipango yao iliyowapeleka nchini humo.

Maaaaajabuu!!!!! Mbuzi azaa kichanga chenye sura ya binadamu



 

Nigeria

HAYA ni maajabu mengine kuwahi kutokea duniani! Mbuzi alyekuwa na mimba amejifungua kiumbe ambacho kina sura kama ya binadamu.

Tukio hilo lilitokea jana Jumatano katika mji wa Taraba nchini Nigeria na kuwaacha watu midomo wazi wakishangaa huku wasiamini kilichotokea.

Chombo cha habari cha Rariya cha nchini humo kiliripoti kuwa, kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio  hiyo, huenda mwenye mbuzi huyo alifanya naye mapenzi, ndiyo maana akazaa mbuzi mwenye sura ya binadamu.

Baada ya tukio hilo kutokea na taarifa kusambaa mjini na kwenye mitandao ya kijamii nchini humo, hakuna mtu yeyote mpaka sasa aliyejitokeza na kukiri kuwa mbuzi yule ni wake, na inadaiwa mara baada ya kujifungua kiumbe hicho kilipoteza uhai muda mfupi baadaye.

Nafasi ya kazi Tanzania Norplan Tanzania Ltd mwisho wa maombi ni tarehe 3 august 2016



SUPERVISOR ( MEDIUM AND LOW VOLTAGE LINE CONSTRUCTION)

POSITION DESCRIPTION:

From Mwananchi, 13th July 2016

NORPLAN Tanzania Ltd (NORPLAN) is a multidisciplinary Consultancy firm registered with Engineers Registration Board as a Local Consulting Company under Registration Number LCF 092. NORPLAN is a member of Association of Consulting Engineers Tanzania (ACET) hence directly affiliated with FIDIC. The firm is therefore an independent operation, with no interests in any manufacturing or contracting organizations. Our impartiality guarantees an objective level of professional advice. NORPLAN Tanzania Limited is currently looking for candidates to fill up vacant positions as described below:

Supervisors – Medium and low Voltage Line Construction (8 Posts)

Qualifications and Skills:
Detailed knowledge of Medium and Low Voltage Line construction and supervision
Thorough knowledge of applicable work practices and procedures, and safety requirements
Must have good written and oral communications ability in English.
A minimum of five (5) years of experience in line construction.
Experience in Rural Electrification Projects and working with TANESCO projects
, Holder of Diploma/FTC in electrical engineering from any recognized Institution.
Possession of computer knowledge is an added advantage.
Must possess a high degree of diligence and professional credibility

Key Duties and Responsibilities:

The successful candidate is expected to work in Mbeya, Iringa, Pwani, Tanga, Arusha or Mara regions. The role
of the supervisor shall be to oversee the supervision of MV/LV line and substations construction.
She/he will oversee each phase of the installation, materials, equipment inspection and approval of
contractors’ works for compliance with design and specifications.

APPLICATION INSTRUCTIONS:

Qualified Candidates should send applications by hand delivery or postage (not by emails) including the
following:
• Curriculum Vitae with two referees
• Copies of relevant certificates and awards
• One passport size photograph attached to application letter

The deadline for ‘receiving applications shall be three weeks from the date of this advertisement.
Only Shortlisted Candidates will be contacted.
Apply to:
The Managing Director
NORPLAN Tanzania Limited
P.O B.O.X 2820,Dar es Salam

Njia 3 Asili za Kuondoa Weusi katika Makwapa na Mapaja

Inner thighs/mapaja ya ndani na makwapa hutokea weusi kutokana na msuguano wa ngozi kwasababu ya mapaja kugusana, hata ngozi iliyokauka pia inaleta weusi katika ngozi.
Hivyo nimekuletea njia natural ya kuondoa weusi huo bila kutumia madawa makali.

1.TUMIA MAFUTA YA NAZI NA NDIMU.

Mafuta ya nazi yanatumikakulainisha ngozi lakini unaweza kutumia pia katika kuondoa weusi ukichanyanya na ndimu..

Fata step hizi::

Chukua vijiko 3 vya mafuta ya nazi changanya na ndimu nusu
Paka sehemu yenye weusi katika mapaja huku ukisugua kama unafanya massage kwa dakika 15.
Kisha osha na maji ya uvuguvugu na kausha kwa kitambaa kilaini na kisafi.

2.TUMIA MCHANGANYIKO WA SUKARI ASALI NA NDIMU.

Mchanganyiko huu pia unaweza ukaondoa weusi katika mapaja na makwapa, fuata step hizi::

Changanya kijiko kimoja cha asali, ndimu nusu na kijiko kimoja cha sukari.
Paka sehemu yenye weusi na sugua kawaida hadi sukari ipotee.
Acha ikae kama dakika 10 kisha osha na maji ya uvuguvugu.

3.GANDA LA CHUNGWA NA ASALI

Kama mnavyojua machungwa yana vitamin C, na hivyo ukichukua ganda la chungwa pamoja na asali, mchanganyiko wake pia unaondoa weusi.

 Fuata step hizi::

Chukua ganda la chungwa na kijiko kimoja cha asali.
Kamua hilo ganda maji yake yangie kwenye asali.
Kausha nakusaga hilo ganda kisha poda yake ichanganye na asali
Paka mchanganyiko huo katika sehemu yenye weusi, kaa kwa muda wa dakika 15
Osha na maji ya kawaida hadi kugandaganda kupotee.

CHECK PICHA MASTAA WA BONGO WALIOACHIWA WATOTO LAKINI HAKUNA NDOA


Rose Ndauka

Mwandishi wetu, Risasi Jumamosi

MPANGO au matarajio ya kila mwanadamu ni kuishi katika uchumba, kuolewa kisha kupata watoto! Wapo ambao wamefanikiwa hilo, wapo ambao wamepata kwanza mimba baadaye wakaolewa lakini wapo pia waliopata mimba kabla ya ndoa kisha wakatofautiana na waliowapa, kila mmoja anaishi kivyake.

Katika ulimwengu wa mastaa wa kike Bongo, leo nakuletea baadhi ya mastaa ambao wamepata watoto lakini kwa namna moja au nyingine safari yao na waliowapa ujauzito haikufika mbali, ikavunjika. Wapo ambao walipata kabla na wengine baada ya ndoa.

Wengi wao huwanadi watoto hao mitandaoni kwa maneno mazuri wakionesha kwamba ndiyo faraja yao baada ya kuachana na wapenzi au waume wao;

ROSE NDAUKA

Aliingia katika uchumba na Malick Bandawe. Wakafanikiwa kupata mtoto mmoja, uchumba ukayeyuka wakati wawili hao wakiwa katika mchakato wa kuelekea kwenye ndoa.

SNURA MUSHI

Amefanikiwa kupata watoto wawili; wa kike na wa kiume kwa baba tofauti. Wote wameingia mitini. Akapata mchumba mpya, naye wakamwagana kabla ya kufanikiwa kuolewa wala kuzaa.

ZUWENA MOHAMMED ‘SHILOLE’

Ana watoto wawili wa kike ambao alizaa na wanaume wawili tofauti kwa nyakati tofauti. Kwa sasa wamemuachia chata ya watoto hao wa kike ambao anawadi mitandaoni.

KAJALA MASANJA

Aliingia kwenye ndoa na Faraji Agustino akiwa tayari ameachiwa chata moja ya kike na Prodyuza, Paul Matthysse  ‘P Funk’. Bahati mbaya mumewe hakufanikiwa kuzaa naye, akafungwa kwa msala wa kutakatisha fedha haramu. Hadi sasa ana furaha kuwa na binti yake huyo.

HAMISA MOBETO

Alikuwa kwenye uchumba na bosi wa redio moja maarufu, akafanikiwa kupata mtoto mmoja na uchumba ukaishia hapo. Kila mtu yupo kivyake kwa sasa Mobeto anajifariji na chata yake ya kike aliyoachiwa.

JENIFFER KYAKA ‘ODAMA’

Inasemekana amezaa na kigogo mmoja ambaye ana familia yake. Inadaiwa kuwa kigogo huyo ameelekeza nguvu zake kwa mkewe hivyo Odama kubaki na chata yake ambayo anainadi kwenye mitandao ya kijamii mara kwa mara.

IRENE UWOYA

Aliingia kwenye ndoa na mshambuliaji wa zamani wa Rayon Sports ya Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’. Akafanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume (Krish) kisha ndoa ikasambaratika na sasa anafarijika kwa kuachiwa kopi yake.

WENGINE

Masta wengine ambao kwa namna moja au nyingine wamezalishwa na kuachiwa watoto ni pamoja na Shamsa Ford, Faiza Ally aliyezaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Siwema Edson (aliyekuwa demu wa Nay wa Mitego) na Riyama Ally ambaye ameachiwa chata ya kike.

MASTAA WA BONGO MOVIE WALIOKUMBWA NA MAKUBWA,UREMBO WOTE KWISHINE,

AUNT EZEKIEL.
Na Gladness Mallya
Kuna watu wamekuwa wakisema kuwa, duniani hakuna mtu aliyeumbwa mwembamba! Kwamba unayemuona leo akiwa mwembamba usije ukashangaa kesho ukakutana naye akiwa bonge kiasi cha kuchukiza.
Hilo limekuwa likitokea sana kwa wanaume na wanawake. Mifano ya watu hao ipo na tunapoiangalia fani ya uigizaji Bongo, wapo mastaa wa kike ambao huko nyuma walikuwa potabo, lakini leo hii wamekuwa mabonge kiasi cha baadhi yao kujichukia.
Wanajichukia kwa sababu wanajua kwa ubonge wao umepunguza na urembo wao pia. Wamejiachia kwa kula mapochopocho, kunywa pombe sana huku wakitumia muda mwingi kulala na kusahau mazoezi.
Mazingira yamewafanya wakose madili ya kuigiza kwenye filamu ambazo zinawahitaji wasichana warembo. Yaani kuna ‘scene’ ambazo zamani walikuwa wakizicheza vizuri lakini leo hii hawawezi kupewa shavu kwa sababu ya unene unaowakosesha mvuto na hivyo kuingia grupu la wamama.

BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’.

Wanakosa sifa ya ku-maintain muonekano wao kutokana na kushindwa kufuata ratiba ya vyakula kwa mujibu wa fani yao. Katika makala haya, mwandishi wetu anakuletea baadhi ya mastaa ambao maumbo yao kwa sasa yapo tofauti na zamani.

AUNT EZEKIEL
Amejaliwa kuwa na mtoto mmoja wa kike aitwaye Cookie. Kwa sasa amekuwa bonge kupita kiasi kwani muonekano wake wa zamani, ule wa Ki- Miss, uliowahi kumfanya wakati f’lani kuwa mshindi wa shindano la urembo mkoani Mwanza, limepotea kabisa. Amepoteza sifa zake za urembo.

WEMA SEPETU
Mwanadada huyu ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2006 na mcheza filamu za Kibongo, amebadilisha kabisa muonekano wa mwili wake, kwani hivi sasa amenenepa tofauti na enzi zake.

BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’
Staa huyu mkongwe kwenye gemu la filamu wakati anaigiza filamu ya kwanza kabisa ya Johari, alikuwa na umbo f’lani ‘amaizing’ lakini kwa sasa amefutuka na kuwa mnene.

JACK PENTZEL ‘JACK CHUZ’
Msanii huyu ambaye ni mama wa mtoto mmoja, zamani alikuwa mwembamba kiasi lakini kwa sasa amekuwa mama, kwani amejiachia na kunenepa sana hali iliyopoteza kabisa ule muonekano wake wa zamani.


LULU SEMAGONGO ‘AUNTY LULU’.

LULU SEMAGONGO ‘AUNTY LULU’
Dada huyu asiyeishiwa matukio, aliyepata umaarufu tangu akiwa mtoto, pale alipokuwa mtangazaji wa Kipindi cha Watoto Show cha Radio One, muonekano wa mwili wake umebadilika kwa kiwango kikubwa sana.

Licha ya kuwa ni mtangazaji, pia ni muigizaji wa filamu za Kibongo, zamani alikuwa mwembamba sana lakini kwa sasa amekuwa bonge na kila anakopita wanaume wakware lazima wakate shingo zao kumtazama.

TIKO HASSAN
Ni mama wa mtoto mmoja, kwa sasa amejazia tofauti na zamani kwani alikuwa mwembamba jambo ambalo linawafanya watu wamshangae kutokana na ubonge wake uliokuja ghafla,

MKE WA REGNARD MENGI, JACKLINE, ATANGAZA AJIRA HIZI, CHANGAMKIA SASA.

MKE wa Bilionea mkubwa TZ,Regnald Mengi,Jackline Mengi leo hii ametangaza tenda kubwa kwa wasuka KATANI wote nchini ambao wanaweza kutengeneza zulia la katani.
Jackline ambaye umaarufu wake umekuwa zaidi mara baada ya kuolewa na mmiliki huyo wa kituo cha Luninga cha ITV,ameandika kuwa yupo tayari kukutana na fundi wa kutengeneza mazulia hayo ili wakafanya biashara.

V

 Follow


Bado natafuta mtengenezaji wa mazulia ya katani kama haya nchini.Naomba anayefahamu anitumie contacts


Diamond platinumz azidi kung'ara ....!!!! Ateuliwa kuwania Tuzo zingine tena.

The African Muzik Magazine Awards AFRIMMA has today unveiled the nominees list for the 3rd edition of the biggest African music awards in Diaspora. Following the outstanding success of the 1st and 2nd editions, AFRIMMA 2014 and AFRIMMA 2015 respectively; anticipation and expectations have hit the roof for this year’s edition set to hold in Dallas on October 15th, 2016.

Some of Africa’s big hitters and the most impressive names on the African music scene in the past calendar year earned a mention in highly competitive categories. Wizkid, Flavour, Davido, Sarkodie, Aka are joined by fresh faces like Falz, Mr. Eazi, Locko and Bisa Kdei on the AFRIMMA 2016 Nominees list. Also for the first time in the history of AFRIMMA, North African music and Caribbean music have been recognized with categories.
Celebrating African music and heritage , the 3rd edition of the annual African Muzik Magazine Awards AFRIMMA promises to be another festival of African music and the nominees list has set off the massive countdown to 10/15/16. Start Voting atwww.afrimma.com and Get your tickets athttp://www.afrimma.com/

Best Male West Africa
Wizkid – Nigeria
Bisa Kdei – Ghana
Serge Beynaud – Ivory Coast
Olamide – Nigeria
Flavour – Nigeria
Carlou D – Senegal
Davido – Nigeria
Sarkodie – Ghana

Best Female West Africa
Tiwa Savage – Nigeria
Yemi Alade – Nigeria
Efya – Ghana
Vivian Chidid – Senegal
Mz Vee – Ghana
Dobet Gnahore – Ivory Coast
Adiouza – Senegal
Almok – Togo

Best Male East Africa
Eddy Kenzo – Uganda
Diamond Platnumz – Tanzania
Jacky Gosee – Ethiopia
Ali Kiba – Tanzania
Jose Chameleon – Uganda
Bebe Cool – Uganda
Sauti Sol – Kenya
Dynamq – South Sudan

Best Female East Africa

Victoria Kimani – Kenya
Vanessa Mdee – Tanzania
Ester Aweke – Ethiopia
Tsedenia Gebremarkos (Ethiopia)
Linah (Tanzania)
Knowles Butera – Rwanda
Sheebah Karungi – Uganda
Akothee – Kenya

Best Male Central Africa

Fally Ipupa – Congo
Magasco – Cameroon
Ferre Golla – DRC
C4 Pedro – Angola
Stanley Enow – Cameroon
Kyaku Kadaff – Angola
Franko – Cameroon
Fabregas – Republic of Congo

Best Female Central Africa

Anna Joyce – Angola
Laurette La Perle – Congo
Betty Akna – Equitorial Guinea
Charlotte Dipanda – Cameroon
Chikune – Namibia
Daphne – Cameroon
Rennis – Cameroon
Arielle T – Gabon

Best Male Southern Africa

Aka – South Africa
Black Coffee – South Africa
The Dogg – Namibia
Vee Mampeezy – Botswana
Dj Bongz – South Africa
Emtee – South Africa
Roberto – Zambia
Casper Nyomvest- South Africa

Best Female Southern Africa

Zonke – South Africa
Miss Lira – South Africa
Ice Queen Cleo – Zambia
Lizha James – Mozambique
Pah Chihera – Zimbabwe
Nnunu Ramo Gotsy – Botswana
Busiswa – South Africa

Best Male North Africa

Amr Diab – Egypt
Tamer Hosny – Egypt
Chawki – Morocco
Mohammed Hamaki – Egypt
Douzi – Morocco
Saad Lamjareed – Morocco
Khaled -Algeria
Saber Rebai – Tunisia

Best Female North Africa

Samira Said – Morrocco
Ibtissam Tiskat – Morocco
Angham – Egypt
Sandy – Egypt
Amal Maher – Egypt
Latifa – Tunisia
Amani Swissi – Tunisia
Jannat Mahid – Morocco

Best African Group

Sauti Sol – Kenya
Radio & Weasel – Uganda
Os Moikanos – Angola
Bracket – Nigeria
Mi Casa – South Africa
R2bee’s – Ghana
Bana C4 – Congo
Yamoto Band – Tanzania

Crossing Boundaries With Music Award


C4 Pedro (Angola)
Wizkid (Nigeria)
Maitre Gims – (Congo)
Tinie Tempah – Nigeria
MHD – Senegal
Ayo Jay – Nigeria
STL – (Kenya)
Rotimi (Nigeria )

Best Gospel

Frank Edwards – Nigeria
Uche Agu – Nigeria
Willy Paul – Kenya
SP Koffi Sarpong – Ghana
Icha Kavons – Congo
Ntokozo Mbambo – South Africa
Sinach- Nigeria
Sonnie Badu – Ghana

Best Newcomer

Adekunle Gold – Nigeria
Reekado Banks- Nigeria
Harmonize – Tanzania
Falz – Nigeria
Locko- Cameroon
Nathi – South Africa
Kofi Kinaata – Ghana
Humblesmith – Nigeria

Best Video Director

Justin Campos – South Africa
Godfather – (South Africa)
Clarence Peters – Nigeria
Patrick Elis- Nigeria
Mysta Adrenalyne -Cameroon
Enos Olik – Kenya
Phamous Films – Ghana
Savy Filmz – Uganda

Best Dj Africa

Dj Spinall – Nigeria
Dj Joe MFalme – Kenya
Dj Cndo – South Africa
Dj Neptune – Nigeria
Dj Malvado Jnr – Angola
Dj Shiru – Uganda
Dj D-Ommy – Tanzania
Dj Labastille – Cameroon

Best African Dj USA

Dj Tunes – Nigeria
Dj Amin – Ethiopia
Dozzy Ross – Nigeria
Dj Deemoney – Nigeria
Dj Silent Killa – Carribeans
Dj Akua – Ghana
Dj Fully Focus -Kenya
Dj Rell – Sierra Leone


AFRIMMA Video of The Year

Flavour – Champion (Nigeria)
Emma Nyra ft Patoranking – For My Matter (Remix)
Sauti Sol ft Ali Kiba – Unconditional Bae (Kenya/Tanzania)
Bisa Kdei – Brother Brother (Ghana)
Akothee ft Diamond – My Sweet Love Kenya /Tanzania
Stanley Enow ft Aka and Locko – Bounce (Cameroon/South Africa)
Phyno ft Olamide – Fada Fada
Korede Bello ft Tiwa Savage – Romantic ( Nigeria )

Music Producer of The Year

Young John – Nigeria
Masterkraft – Nigeria
Dr Fizol – Uganda
Kaywa – Ghana
Visita – Kenya
Tweezy – South Africa
Tud Thomas – Tanzania
Dj Coublon – Nigeria

Best African Dancer

Kaffy Dancequeen – Nigeria
Ezinne CEO – Nigeria
Brenda Derry – Cameroon
Sherri Silver – Rwanda
La Petite Zota – Ivory Coast
Eddy Wizzy – Uganda
Moses Iyobo – Tanzania
Roxy Roberts –

Best Rap Act

Phyno – Nigeria
Olamide – Nigeria
Aka – South Africa
Sarkodie – Ghana
Casper Nyovest – South Africa
King Kaka Sungura – Kenya
Octopizzo – Kenya
Prodigio – Angola

Best Collaboration

Reggea Blues – Harrysong , Kcee , Iyanya, Olamide and Orezi
Finally by MasterKraft , Flavour and Sarkodie
Mr. Eazi ft Efya – Skin Tight – Ghana
Diamond Platnumz ft Aka – Make Me Sing
Wizkid X Dj Maphorisa – Soweto Baby
Kiff No Beat ft Dj Arafat – Approchez Regardez
Lil Kesh ft Patoranking – Is it Because I love You
J Martins ft Youssour Ndour – Time is Now

Song of The Year

Sauti Sol ft Ali Kiba – Unconditional Bae
Franko – Coller La Petite
Reggea Blues – Kcee, Harrysong, Orezi, Iyanya and Olamide
Bisa Kdei – Mansa
Tekno – Duro
Kiss Daniel – Mama
Phyno ft Olamide – Fada Fada
Diamond Platnumz ft Aka – Make Me Sing

Artist of The Year

Flavour (Nigeria)
Diamond Platnumz ( Tanzania)
Sarkodie (Ghana)
Wizkid (Nigeria)
Aka (South Africa)
Tiwa Savage (Nigeria)
Sauti Sol – Kenya
C4 Pedro – Angola

Dancehall Act of the Year

Timaya – Nigeria
Stonebwoy – Ghana
Buffola Soldier – Zimbabwe
Burna Boy – Nigeria
Mc Norman Ganja -Uganda
Samini – Ghana
Patoranking – Nigeria
Shatta Wale – Ghana

AFRIMMA Caribbean Artist of The Year

Morgan Heritage
Alaine
Machel Montano
Sean Paul
Konshens
Busy Signal
Tarrus Riley
Olatunji

Wema: Licha ya Kuniacha, Nitazaa na Idris

LICHA ya madai kuwa wapenzi wawili, Idris Sultan na Wema Sepetu wamemwagana, muigizaji huyo nyota na Miss Tanzania 2006, amesema anataka kuzaa na mshindi huyo wa Big Brother Hotshots 2014 kutokana na jinsi anavyojali na mwenye huruma nyingi.

Akiteta na Amani hivi karibuni, Wema alisema atajisikia fahari sana endapo mtoto wake wa kwanza angezaa na Idris kwa kuwa amemuonesha dhahiri kuwa ni baba bora.

“Kiukweli namuomba sana Mungu kila kukicha, baba wa mtoto wangu awe ni Idris kwa kuwa ni mwanaume pekee ambaye naona ni mwenye mapenzi ya dhati kwangu,” alisema Wema.

Chanzo: Amani

Kinana atoa Masharti Endapo Rais Magufuli Atamhitaji Aendelee Kuwa Katibu Mkuu wa CCM

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ametoa neno endapo Rais John Magufuli atamhitaji kuendelea na wadhifa huo, huku akibainisha kuwa amekutana na changamoto nyingi katika nafasi hiyo kiasi kwamba wakati mwingine alikata tamaa.

Mwanasiasa huyo maarufu ndani ya CCM na nchini, anatarajiwa kuhitimisha uongozi wake wiki hii wakati Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa, Rais John Magufuli atakapokabidhiwa uenyekiti huo na kuunda Sekretarieti yake mpya ambayo haijulikani kama itaongozwa tena na Kanali huyo wa zamani wa Jeshi.

Akizungumza jana na waandishi wa habari baada ya kukagua Ukumbi wa Mkutano Maalumu wa CCM utakaofanyika keshokutwa Jumamosi, Kinana ambaye amekuwa katika nafasi hiyo kwa miaka mitatu na nusu, alisema aliombwa katika nafasi hiyo baada ya kuwa aliamua kustaafu, lakini akakumbana na changamoto mbalimbali.

CCM kuwa mbali na wananchi 

Alisema kuna wakati aliona kama vile chama kiliacha kwenda kwa wananchi na kwamba hakikuwa karibu sana nao.

“Ninyi ni mashahidi, ikabidi kubuni utaratibu mzuri wa kwenda kwa wananchi ili chama kiwe karibu na wananchi, kiwasikilize na kuwa sauti ya wananchi kifuatilie matatizo yao kisimamie utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi,” alisema Kinana na kuongeza kuwa katika kufanya hivyo amekuwa akiwasiliana na Rais na Waziri Mkuu kwa ajili ya matatizo kutatuliwa.

“Changamoto ya pili ya kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya chama, hapo nyuma kulikuwa na misukosuko kidogo ya umoja na mshikamano, kushutumiana na kulaumiana,” alisema na kuongeza kuwa kazi nyingine aliyofanya ni kuimarisha umoja ndani ya chama, kushirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha chama kinajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kurejea katika misingi yake ya awali katika maeneo ya uadilifu, uwajibikaji na utendaji kazi kwa ufanisi.

Azuiwa ziarani

Kinana alisema amekwenda wilaya zote, majimbo, mikoa na nusu ya kata za nchi na amesafiri zaidi ya kilometa 192,000, kufanya mikutano zaidi ya 3,700 ya aina mbalimbali ya ndani na nje na haikuwa kazi rahisi

 “Changamoto nilizokutana nazo ambazo lazima nikiri ni pale nilipotaka wakati mwingine kufanya ziara kwenye maeneo fulani fulani niliambiwa ni hatarishi siwezi kwenda kwa hiyo ilibidi nibishane na viongozi na watendaji wakuu wa serikali…nikasema hapana nimeamua kwenda lazima niende,” alisema Kinana.

Katibu huyo akitoa mfano alisema kuna wakati aliamua kutoka kwa boti kutoka Nyamisati wilayani Rufiji kwenda Mafia, viongozi wa Mkoa wa Pwani walifikiri si njia salama ya kusafiri na kumpelekea ujumbe asisafiri kwa boti, bali asafiri kwa ndege, lakini alisema hapana ataondoka kwa boti.

“Walichofanya wakakaa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na wakaniandikia barua rasmi kwamba tunakushauri usisafiri kwa boti safiri kwa ndege kwa maana nyingine walikuwa wanajivua lawama kwa yatakayotokea, lakini vile vile kunitisha kidogo kwamba si salama zaidi nikawasisitiza hapana,” alieleza Kinana.

Ashitakiwa kwa JK

“Baadaye Rais mstaafu Kikwete alikuwa Msoga, viongozi wa Mkoa wa Pwani wakaenda kumwambia tumezungumza na Katibu Mkuu wako naona hasikii tumemuandikia barua ya kumuomba asisafiri na boti hasikii, Rais akaandika meseji ndefu sana…nikamjibu rais nakuheshimu mamlaka yako ni makubwa si vizuri nikakukatalia, lakini niruhusu nikukatalie kwa sababu hata wananchi wanaosafiri kwenye boti hii wanahatarisha maisha yao, ni vizuri na mimi nikahatarisha maisha yangu hata kidogo… akaniambia nimekuelewa endelea,” alibainisha.

Alisema zipo changamoto nyingi sana nyingine, kwa mfano Mbambabay kwenda Kyela, mkuu wa mkoa akamuambia boti haifai kusafiri akasema mara haiwezi kusafiri imeharibika.

“Nikazungumza na Mwakyembe akapeleka mafundi wakatengeneza, safari haikuwa rahisi, lakini changamoto zilikuwa nyingi sana, kwingine Lupingu kule ni gari moja tu ndio inayoshuka chini hakuna kupishana magari nikaambiwa nisiende nikasema nina kwenda,” alisema na kuongeza kuwa kulikuwa na ubishi mwingi wakati mwingine alionekana mtu mmoja kidogo ambaye hasikilizi ushauri sana.

Pia nyingine zinazotokana na changamoto za wananchi kutolipwa mazao yao kwa wakati, mbolea kutofika kwa wakati, halmashauri kutopata fedha za maendeleo kwa wakati, watumishi wa umma wanaohamishwa kwenda vijijini hawaendi vijijini kwenda kuwahudumia wananchi, tatizo kubwa la migogoro kati ya wakulima na wafugaji kati ya wananchi na hifadhi za taifa.

“Ndio maana mnaniona siku hizi nimenyamaza kwa sababu yale yote niliyokuwa nikiyaombea yanafanyika, umangimeza haupo watu wachape kazi wawahudumie wananchi, uadilifu unapigwa vita, rushwa inapigwa vita, uwajibikaji na uadilifu unahimizwa, utendaji kazi unatakiwa na hayo yasipofanyika mtu anaondolewa mara moja,” alifafanua Kinana ambaye kuanzia mwaka 2014 hadi mwanzoni mwa mwaka jana alitembea kote nchini akikisafisha chama chake na kuibana serikali.

Kurejea kwake CCM

“Yalitokea mazingira ambayo niliombwa na viongozi wastaafu na viongozi wa chama kuniomba niwe mtendaji mkuu wa chama chetu. Si nafasi ambayo niliipenda, bali niliitwa na nikakalishwa wakanisihi na mimi nikakubali sababu ni wito na kwa kuwa ni watu ninaowaheshimu na wana dhamana kubwa kwenye nchi yetu, nikakubali kufanya kazi hiyo,”alisema Kinana akizungumzia jinsi alivyoteuliwa kushika nafasi hiyo.

Alisema amekuwepo katika uongozi ndani ya chama kwa muda mrefu (miaka 25) ndani ya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa, na alihisi ni wakati muafaka wa kung’atuka.

“Mwanasiasa mzuri ni yule anayejua wakati wa kuingia na wakati wa kutoka. Ni wakati mzuri wa kung’atuka kuachia waingie wenye umri wa kati na umri wa vijana kuachia waongoze chama na kuwaamini,” alieleza.

Alisema moja ya mambo ambayo walikubaliana wakati ule akajitahidi kukiimarisha chama, kusimamia na kumsaidia mwenyekiti kusimamia mchakato wa kuwapata wagombea kwenye nafasi zote za Urais, Ubunge na Udiwani. Pia alijitahidi kuendesha shughuli za kampeni na uchaguzi na utakamalizika.

“Uchaguzi umekwisha niruhusiwe kupumzika, na wote waliafiki na kukubali sasa muda umefika kwa hiyo nimewakumbusha yale tuliyokubaliana muda wake umefika sasa wengine wakaniuliza hivi ndivyo tulivyokubaliana nikawaambia wazee hamjawa wazee kiasi cha kusahau ndio haya tuliyokubaliana,” alieleza.

Akiombwa na JPM

Alipoulizwa kama akiombwa na Rais Magufuli aendelee kwa Katibu Mkuu, Kinana alisema, “Niseme hajasema, hatujazungumza hilo, likitokea tutaangalia, tutakaa naye kikao kama akiniomba, tutakuwa na kikao na mazungumzo muda utakapofika kama nilivyokuwa na mazungumzo na kikao kama kwa wale walioniomba mwaka 2012.”

Waliokisaliti chama

Akizungumzia walioisaliti CCM katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana, mtendaji huyo wa CCM alisema msaliti yeyote adhabu yake ni mbaya sana, hata kwenye chama cha siasa.

“Kwenye CCM wapo watu walioyumba, kulikuwa na wimbi kubwa mwaka jana, watu waliyumba hivi kidogo wakakaa mguu upande huku hawapo na kule hawapo, wako ambao sio tu waliyumba, bali walikiuka maadili na hawakushiriki kwenye shughuli za kampeni,”alisema.

Pia alisema wapo ambao hawakushiriki, hawakusaidia na wakasaidia upinzani na kila mtu atakuwa na adhabu yake kulingana na makosa yake.

“Kama mmekuwa mkifuatilia kuna waliochukuliwa hatua ngazi za wilaya na mikoa. Kwa mfano, Shinyanga 123 walichukuliwa hatua. Wapo wanaotakiwa kuchukuliwa hatua kwenye ngazi za juu, sasa jambo moja mtu yeyote kabla ya kuchukuliwa hatua lazima aelezwe mashtaka yake, apewe fursa ya kusikilizwa, kwa hiyo hawa wote watasomewa mashtaka, watasikiliza na kupewa adhabu kwa kadri itakavyostahili, lakini hatua zitachukuliwa mara baada ya Mkutano Mkuu kumalizika,” alieleza.

Magazeti ya Leo alhamisi Julai 21 kwenye habari za udaku, kitaifa kimataifa, michezo n. K















 

Gallery

Popular Posts

About Us