Monday, July 04, 2016
Maaaajabu!!!! Akutwa na kichwa cha binadamu
Yaliyojiri kutoka Karimjee Hall: Wakuu wa Wilaya za Dar Es Sallam waapishwa leo.
Wakuu wa Wilaya za Temeke,Ilala,Kinondoni,Ubungo na Kigamboni.Wakuu wa Wilaya wanne ndio wamefika isipokuwa Mkuu wa Wilaya mpya ya Ubungo ndugu Humphrey Polepole ambaye hataapishwa leo,sababu ikiwa ni kufiwa na baba yake.
Shughuli hii inasimamiwa na Clouds Media huku ikionyeshwa moja kwa moja kupitia Clouds Tv na MC wa sherehe hii ni Ephraim Kibonde.Wakuu hao wa Wilaya ni
Felix Jackson
Mgandilwa Hashim
Sophia Mjema
Ally S Happi
Baada ya kuapishwa mkuu wa mkoa atatoa muongozo kwa Wakuu wa Wilaya na baadae waandishi wa Habari watapewa nafasi ya kuwauliza Wakuu wa Wilaya maswali ya moja kwa moja kuhusu Wilaya zao na mipango yao
Mkuu wa Mkoa anasisitiza kuwa Wakuu wa Wilaya wana nafasi ya kuingia katika vikao vya madiwani,na haambiwi cha kufanya na Meya,sababu Meya ni Spika tu wa baraza la madiwani na ndio maana nafasi yake ni kuongoza vikao na huitajika ofisini mara mbili tu kwa week.Shughuli zote zinakuwa chini ya Mkuu wa Wilaya ambaye ndie mwakilishi wa Rais katika Wilaya na si Meya.
Mh Makonda anasema ndio maana Meya analindwa na Mgambo wakati Mkuu wa Wilaya analindwa na Jeshi,Polisi na ana usalama wa Taifa,hivyo Mameya wa Dsm wawaache wakuu wa wilaya kufanya kazi zao sbb wapo kwa mujibu wa Katiba ya Tz.
Mkuu wa Mkoa anawaagiza Wakuu wa Wilaya kupambana na ushoga,na kuwa ana taarifa ya NGO iliyopewa dola milioni 70 katika mkoa wa Dsm ili kuimarisha swala la mashoga,ameipa onyo NGO hiyo na kuahidi kuifutilia mbali sababu inatumika kueneza tabia za kishoga ambazo kwa mujibu wa Katiba ya nchi ni kosa linahitaji hukumu.
Makonda amesisitiza kuwa vita ya shisha ndio imeanza,na kwa mujibu wa TFDA shisha ni madawa ya kulevya na husababisha saratani ya Koo,anasema unaenda Double Tree Hotel unamkuta binti mdogo mzuriii halafu anavuta shisha,anaagiza kuwa shisha ni marufuku na yoyote atakayeuza Segerea inamsubiri.Wavutaji wa sigara wote wanatakiwa kuvuta maeneo ya "private" na kama wanataka kuonyeshwa hizo sehemu za Private basi wavute hadharani ndio wataijuwa hiyo "more private" ipo wapi.
Ombaomba wametangaziwa "kiama",kwamba kwenye mitandao watu wameanza kusema zoezi hilo limeshindwa,lkn anawapa week mbili kuhakikisha wameweka mpango kazi kuondoa hawa ombaomba.Watumie mpango kazi na ilani ya CCM kusaidia watu,na baada ya siku 90 wakuu wote wa mkoa watakuja hadharani mbele za watu pale ukumbi wa Mwalimu Nyerere kusema mambo gani waliyoyafanya na kuyapanga katika wilaya zao
Kitwanga: Sijutii kutumbuliwa na Magufuli
CHARLES Kitwanga, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema kuwa, hajutii ‘kutumbuliwa’ na Rais John Magufuli, anaandika Moses Mseti.Ametoa kauli hiyo wikiendi iliyopita jimboni kwake Misungwi jijini Mwanza ikiwa ni takribani mwezi mmoja baada ya kung’olewa kwenye nafasi hiyo.Kitwanga alifukuzwa kazi kwa madai ya kuingia bungeni na kujibu masali ya wizara yake akiwa amelewa.Amesema kuwa, anamshukuru Mungu kwa kuondolewa katika nafasi hiyo na kwamba, huenda kama angeendelea kuwepo, angepata matatizo makubwa zaidi.Na kwamba, hatua ya Rais Magufuli kumwondoa katika nafasi hiyo kitamsaidia kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kwa ukaribu zaidi tofauti na alivyokuwa kwenye nafasi ya uwaziri.“Namshukuru sana Mungu kuondolewa katika nafasi hii (Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi) labda ameniepusha na mambo mengi ambayo yangeweza kunikumba na hii itanisaidia kuwatumikia wanamisungwi kwa ukaribu,” amesema Kitwanga.Kitwanga baada ya kung’olewa katika nafasi hiyo, siku kadhaa baadaye alitimkia nchini Israel ambako inadaiwa kwenda kupumzika ambapo alirejea nchini hivi karibuni.Baada ya kurejea nchini, Kitwanga moja kwa moja alikabidhiana Ofisi na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa Mwigulu Nchemba aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo. Nchemba alikuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.Kabla ya kutimuliwa Kitwanga alikuwa akiandamwa na kashfa ya Kampuni ya Lugumi iliyopewa zabuni ya kufunga mashine za kutambua alama za vidole katika vituo vyote vya Jeshi la Polisi nchini.Jeshi hilo liliingia mkataba na Kampuni ya Lugumi Enterprises ili kufunga mashine 108 nchi nzima lakini kampuni hiyo ilifunga mashine 14 tu.
Mabasi ya haraka kuanza kutumia gesi
MSIMAMIZI wa Usambazaji Gesi katika Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Ismail Naleja, amesema awamu ya pili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam yatatumia nishati ya gesi asilia badala ya mafuta jambo litakalosaidia kupunguza gharama. Katika awamu ya pili, mabasi mapya 200 ya mradi huo yanatarajiwa kuingizwa nchini.
Akizungumza katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, kuhusu usambazwaji wa gesi katika magari, Naleja alisema hatua hiyo itaongeza idadi ya magari yanayotumia gesi nchini ambapo hivi sasa kuna mabasi 60 yanayotumia gesi na kuwashauri wenye magari kutumia mfumo huo ili kupunguza gharama za uendeshaji.
“Uendeshaji wa gesi utakuwa nafuu jambo linaloweza kufanya hata nauli zake kupungua kwani kilo moja ya gesi inatumika katika umbali unaotumiwa na mafuta ya dizeli lita moja na nusu,” alieleza Naleja.
Alisema kilo moja ya gesi ni Sh 1,500 wakati lita moja na nusu ni Sh 3,000, pia gesi haiharibu mazingira kwa sababu haina kaboni ikilinganishwa na petroli.
Aliongeza kuwa, gharama ya ufungaji wa mfumo wa gesi kwenye gari ni Sh milioni mbili, fedha ambayo inarudi baada ya kupunguza gharama katika matumizi kwa miezi mitano tu.
Mtaalamu huyo alisema matumizi ya gesi katika magari si hatari, kwani gesi inayotumika ni nyepesi kuliko inayotumika majumbani, hivyo ikivuja inasambaa hewani na tatizo likitokea mtungi wa gesi unajifunga.
Naye Msemaji wa Kampuni inayoendesha mabasi ya haraka ya UDART, Sabri Mabrouk alisema ni kweli kuwa awamu ya kwanza ya magari yaendayo haraka hayakuweza kutumia gesi kutokana na shirika hilo kuchelewa kupeleka wazo hilo. Hata hivyo sasa wameshafanya mazungumzo ili mradi wa awamu ya pili utumie gesi ili kupunguza gharama.
Alisema wanatarajia awamu ya pili ya mradi utakuwa na mabasi 200.
(CHANZO: HABARI LEO)
WAUMINI WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA WAHOJI KUHUSU AFYA YA ASKOFU GWAJIMA
Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, wamesali Jumapili ya tatu bila kuwapo kwa Askofu wao, Josephat Gwajima,lakini wameshtushwa na taarifa kuwa kiongozi huyo wa kiroho ni mgonjwa na anapata matibabu nje ya nchi.
Waumini hao walisema wamekuwa wakisikia kuwa askofu wao anatafutwa na Jeshi la Polisi na juzi wamesikia kuwa anapata matibabu nje ya nchi wakati wao hawajatangaziwa rasmi kuhusu taarifa hizo.
Juzi, Wakili wa Askofu Gwajima, Peter Kibatala aliileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mteja wake hakufika mahakamani kwa kuwa yuko nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Askofu Gwajima alitakiwa kufika mahakamani hapo anakokabiliwa na kesi ya kumtolea lugha chafu Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi, Cyprian Mkeha.
Mbali na taarifa za kuumwa, pia Gwajima anatafutwa na Polisi baada ya kusambaa kwa sauti inayosikika kama yake ikitaka Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika katika utawala wake.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa atalizungumzia suala hilo leo Jumatatu.
Katika ibada ya jana, kama kawaida, Mchungaji Adriano Edward hakuwaeleza chochote waumini wa kanisa hilo kuhusu alipo Askofu Gwajima wala hali ya afya yake.
Mchungaji Adriano alipotakiwa kuzungumzia suala la afya ya Gwajima, alisema kupitia msaidizi wake kuwa hawezi kuzungumza chochote na vyombo vya habari.