KINGAZI BLOG: 05/26/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Thursday, May 26, 2016

Trump apata wajumbe wa kutosha kupata uteuzi


Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Donald Trump amefikisha idadi ya wajumbe ya kupata uteuzi wa chama hicho kulingana na chombo cha habari cha AFP.

Bw Trump ambaye aliwashinda wagombea wengine 16 wa chama hicho ameripotiwa kupata wajumbe 1,238 mmoja zaidi ya inavyohotajika.

Chama cha Republican kinataraijiwa kukamilisha uteuzi wao katika mkutano wa chama hicho utakaofanyika huko Cleveland mnamo mwezi Julai.

Iwapo atathibitishwa ,bw Trump atakabiliana na aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Hillary Clinton au seneta wa Vermont Bernie Sanders ambao wanashindania uteuzi wa chama cha Demokrat.

Siku ya Jumatano,bilionea huyo wa New York alipanga kufanya mjadala na Bernie Sanders katika runinga mjini California kabla ya uchaguzi wa mchujo wa tarehe 7 mwezi Juni.

Bw Sanders alikubali kushiriki katika mjadala huo katika ujumbe wake wa Twitter uliosema: ''Game on''.

Mrema Alaani Hatua ya Katibu Mkuu CUF Maalim Seif Kutangaza Kumwondoa Rais wa Zanzibar, Dr Shein Madarakani kabla ya 2020

Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Tanzania Labour Party  ( TLP), Augustino Mrema amelaani hatua ya Katibu Mkuu wa  CUF Maalim Seif kutangaza kumwondoa Rais wa  Zanzibar, Dr Shein  madarakani kabla ya 2020 huku akiwataka wazanzibar kutoyumbishwa na kauli za mwanasiasa huyo.

Mrema amezungumza hayo leo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari na kusema kwamba amani ya Zanzibar ni muhimu kuliko maslahi binafsi hivyo ni vyema kuzitafakari kauli ambazo zinaweza kuleta machafuko.

Amesema hakuna mtu aliye  juu  ya sheria hivyo kuwepo kwa watu wanaochochea  vurugu  ni kama waahini pia ni  vyema  hatua zichukuliwe dhidi yao katika kuhakikisha  wananchi wanakuwa salama

Aidha Mrema amesema kwamba amani ya Zanzibar ikiharibika hata bara haiwezi kuwa salama hivyo ni vyema kauli za kuvuruga amani zizingatiwe ili kulinda maslahi ya wananchi wa pande zote mbili.

Amesema Zanzibar ina historia ya kuuawa watu mwaka 2001 kutokana na vurugu za kisiasa hivyo lazma  kwa  sasa suala la ki uchochezi liangaliwe kwa macho mawili dhidi ya watu wanaotaka kuvuruga amani katika mazingira hayo.

Mrema amesisitiza hakuna chama cha siasa ambacho  kinajengwa kwa kususia uchaguzi bali kwa kufanya hivyo ni  kuwanyima wapiga kura haki pia ni hatari na  kunaweza kusababisha chama kusambaratika kama kulivyotokea kwa baadhi ya vyama mfano, UPC cha Uganda na vinginevyo.

Pamoja na hayo mrema amefafanua kwamba mahakama ya ICC haingalii tu viongozi wa serikali bali hata viongozi wa kisiasa ambao wamesababisha mauaji kutokana na kauli wanazozitoa.

Pia mwenyekiti huyo wa TLP amewataka wahisani kutoingilia mambo ya ndani ya nchi kwani kusitisha misaada kwa hoja ya kufutwa uchaguzi wa Zanzibar na sheria ya mitandao ni kuingilia uhuru wa watanzania.

Makandarasi 4572 Wafutiwa Leseni Nchini



Bodi ya Usajili wa Makandarasi imefuta usajili wa jumla ya makandarasi 4572 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Sheria ya Usajili wa Makandarasi ya mwaka 1997.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Bw. Rhoben Nkhori wakati wa Mkutano wa Mashauriano wa CRB uliofanyika jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Nkhori amesema kuwa katika jukumu la kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi, Bodi ilikagua miradi 2735. Katika miradi hiyo iliyokaguliwa, miradi 1873 sawa na asilimia 68.5 haikuwa na kasoro.

Ameongeza kuwa miradi mingine ilikuwa na kasoro za kutofanywa na makandarasi waliosajiliwa, kutozingatia usalama wa wafanyakazi, kutokuwa na bango wala uzio na miradi kutosajiliwa. Kwa mujibu wa Bw. Nkhori miradi yote iliyopatikana na upungufu wahusika walichukuliwa hatua mbali mbali kwa mujibu wa sheria.

Aidha, Bwana Nkhori amesema kuwa kwa mwaka jana, Bodi ilisajili miradi 3,172 yenye thamani ya shilingi trilioni4.23. Katika miradi hii asilimia 44.4 ilifanywa na Makandarasi wazawa na asilimia 55.6 ilifanywa na makandarasi wa kigeni.

Licha ya mafanikio hayo CRD ilikumbana changamoto kadhaa ikiwemo kuwasilisha nyaraka za kugushi wakati wa usajili hususani kadi za magari na mitambo, vyeti vya wataalam, kutumia majina ya makandarasi kwa udanganyifu kwa kuuza vibao, waendelezaji kutotoa taarifa sahihi za umiliki kwa Bodi na baadhi ya makandarasi kushindwa kuwalipa wafanyakazi na vifaa vya ujenzi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi, Bi Consolata Ngimbwa amemwomba Mhe. Rais John Pombe Magufuli kuwapa kipaumbele Makandarasi wa humu nchini ili kuwawezesha kiuchumi. “Mhe. Rais tunaomba utupe kipaumbele kwani sisi tukipata hiyo miradi tutawekeza hapa nchi na kuongeza soko la ajira,”alisema Bi Ngimbwa.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema serikali yake itawapa kipaumbele makandarasi wazawa lakini akawataka wajipange na kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ikiwemo kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Mkutano huu pamoja na mamabo mengine utajadili jinsi ya kuwajengea uwezo makandarasi nchini. Kauli mbiu ya Mkutano huo ni “Juhudi za Makusudi za kukuza uwezo wa makandarasi wazawa, changamoto na mustakhabali.”

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo 26 May 2016

MOURINHO KOCHA MPYA MANCHESTER UNITED


Kwa mujibu wa matandao wa Sky Sports, Jose Mourinho ametangazwa kuwa kocha mpya wa Manchester United.

Tayari ameshasaini mkataba na tayari umeshatumwa kwenda Manchester na vuguvugu la tetesi za kocha huyo kujiunga na United zimekwisha.

Kabla ya mashabiki hawanjaanza kusherekea ujio wa Maurinho kwenye klabu yao, Manchester United walikuwa wanachelewesha kutangaza kama dili tayari limefikiwa.          
Source shaffii dauda.

Majipu yatumbuliwa Bodi ya TCU,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako amevunja Bodi ya Tume ya Vyuo Vikuu nchini Tanzania(TCU ) kufuatia Tume hiyo kupitisha majina ya wanafunzi 486 wasio na sifa kusomea Shahada ya Elimu.

Pia,Waziri Ndalichako amewasimamisha kazi Maafisa kadhaa waandamizi wa TCU kwa kushindwa kusimamia na kutekeleza vyema wajibu wa TCU. Waziri Ndalichako amewateua Makaimu wa nafasi za waliosimamishwa.

Rais Magufuli na Mkewe Waguswa na Stori ya Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Aliyepofuka Macho..Waamua Kumchangia Mil 10 Akatibiwe

Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DktJohn Pombe Magufuli, Mkewe Mama Janeth Magufuli na familia yake kuahidi kuchangia Milioni 10 kwaajili ya matibabu ya #Kipepeo Bernadeta Msigwa mwakilishi kutoka ofisi ya Rais Bw. Ngusa Samike amefika katika ofisi za CloudsMediaGroup na kukabidhi fedha hizo. Vilevile Mheshimiwa Rais ametoa ujumbe kwa Kipepeo Bernadeta kuwa amtumainie Mungu kwani ndiye muweza wa kila kitu. Katika upande mwingine Naibu wa Waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde amechangia Shilingi Milioni 1. 
Kama umeguswa na unahitaji kuchangia au unataka maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kumsaidia piga namba 0742848729. Pia unaweza kuangalia story yake kamili kwenye account hii ya Instagram@BernadetaMsigwa. 
Asante sana Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli

 

Gallery

Popular Posts

About Us