KINGAZI BLOG: 05/14/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, May 14, 2016

Kibao Chamgeukia NAPE Nhauye Bungeni...Awekwa Kikaangoni na Wabunge..Aitwa Waziri Mzigo



Wabunge wamemcharukia Waziri wa Habari, Nape Nnauye kwamba aliwahi kuwaita mawaziri wa Serikali iliyopita mizigo, lakini yeye amezuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, ili wananchi washindwe kumpima kama ni mzigo au lumbesa. 

Hayo yalijitokeza jana wakati wabunge walipochangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari kwa mwaka 2016/2017, iliyowasilishwa bungeni na Waziri Nape. 

Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) alieleza kushangazwa na hatua ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhimiza wananchi kudai risiti wanaponunua bidhaa, lakini haitaki wananchi waone inavyopanga matumizi yake. 

Alisema Nape akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, aliwaita baadhi ya mawaziri ni mizigo, lakini amepewa wizara hiyo amezuia mijadala ya wazi ambayo ingesaidia wananchi kumpima. 

“Nilipoona amepewa wizara ya habari nikajua ataruhusu mijadala ya wazi ili tumuone yeye kuwa hatakuwa mzigo, lakini yeye akawa lumbesa. Hilo amelizuia kwa hiyo tunashindwa kumpima,” alisema. 

Alisema waziri huyo hawezi kukwepa lawama ya hicho kinachoendelea cha kuzuia matangazo ya Bunge, kwa vile wanaopiga picha na kuhariri taarifa zinazorushwa ni watumishi wa TBC. 

Udhibiti wa Bunge 
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (Act-Wazalendo), alisema kuwa wabunge wote waliopinga Bunge kutoonyeshwa ‘live’ na kusababisha mtafaruku bungeni, wameitwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge. 

“Wabunge hapa tulisimama tukapinga na wapo waliounga mkono, lakini kiti chako kimetuita wabunge wote tuliopinga kauli ya Serikali kwenye kamati ya maadili. Jana mimi nimepata barua,” alisema Zitto. 

“Kwamba mnatubana kusema. Mnazuia Bunge lisionekane. Hata kutoa maoni ndani ya Bunge tunakwenda kuhojiwa? TBC ni chombo cha umma, siyo chombo cha Serikali, inaendeshwa kwa kodi za wananchi,” alisisitiza. 

Baada ya mchango huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alisema si kweli wabunge hao wanahojiwa kutokana na michango yao, bali wanahojiwa kutokana na mambo waliyoyafanya kwa kutotii maagizo ya kiti wakati wa mjadala wa ‘Bunge Live’. 

Kwa upande wake, Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), aliunga mkono hoja ya Zitto ya kuifanya TBC iendeshwe kama inavyoendeshwa BBC kwa kupewa  leseni maalumu. 

Pia, aliitaka Serikali kupeleka muswada bungeni utakaowabana wamiliki wa vyombo vya habari kuwa na mikataba na waandishi wanaowaandikia, pia, akadai baadhi ya vyombo haviwalipi waandishi wake.

Hata hivyo Mbunge wa Viti Maalumu, Agness Marwa (CCM) alitetea uamuzi wa Serikali kuondoa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, akisema wabunge wanaodai hilo ni wale waliokuwa wakiuza sura. 

Katika hatua nyingine, Waitara alisema kitendo cha Nape kuwaalika wabunge kwenye muziki, baada ya bajeti yake kupita ilikuwa ni kuwahonga. 

Juzi jioni wakati akitoa matangazo kabla ya kuahirisha Bunge, Naibu Spika alisema baada ya kupitisha bajeti ya Wizara ya Habari, wanamuziki Diamond Plutnum na King Kiki watatumbuiza katika viwanja vya Bunge. 

“Mnaposema mnabana matumizi hao wanamuziki wameletwa kwa gharama za nani,” alihoji mbunge huyo. 

 “Wabunge wote ambao wataenda katika hiyo miziki ili kuunga mkono habari ya Nape mtakuwa mmekula rushwa,” alisisitiza Waitara, kauli ambayo ilimfanya Naibu Spika, Dk Tulia kufafanua, akisema suala hilo lilitangazwa bungeni kama mengine, lisiingizwe kosa la jina la rushwa. 

Upinzani na udikteta 
Msemaji mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Joseph Mbilinyi, alisema kitendo cha Serikali kuminya uhuru wa habari ni kuelekea kwenye udikteta. 

 “Kana kwamba haitoshi, Serikali sasa imezuia Televisheni ya Umma, inayoendeshwa na kodi ya wananchi (TBC1) kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mijadala inayofanyika bungeni. Dalili hizi siyo njema kwa ukuaji wa demokrasia na uhuru wa habari hapa nchini na zinatoa taswira ya utawala wa ki-dikteta,” alisisitiza. 

“Tunaitaka Serikali kuliomba radhi Bunge hili, kwa kosa la kuminya uhuru wa habari kinyume na Katiba na kuviacha vyombo vya habari hususan vya umma kufanya kazi zao za kuhabarisha umma kwa uhuru,” alisema.

( DOWNLOAD) Madee - Migulu Pande( Official Video )


(download)LINAH SANGA - IMANI( NEW AUDIO)


(DOWNLOAD) Ben Pol - MOYO MASHINE (Official Video)


(AUDIO) SHILOLE FT BARNABA - SAY MY NAME(AUDIO)

Jela miaka 30 kwa kuoa na kuzaa ni binti yake wa kumzaa.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, jana ilimhukumu kifungo cha miaka 30, Godfrey Mjelwa (48), baada ya kupatikana na hatia ya kuishi kinyumba na binti yake wa kumzaa. 

Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo, Mwajuma Lukindo alisema ushahidi wa pande zote ulithibitisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kuishi chumba kimoja na binti yake, kama mke na mume. 

Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa, Mjelwa aliamua binti yake mwenye umri wa miaka 15 (jina limehifadhiwa) kuwa mke na kuishi naye katika Mtaa wa Kizota Manispaa ya Dodoma. 

Hakimu Lukindo alisema kosa alilokutwa nalo mtuhumiwa ni ‘maharimu’ (kufanya mapenzi na ndugu za damu), licha ya kuwa mtoto huyo bado alikuwa mdogo, lakini ni mtoto wake wa kumzaa. 

Mwendesha mashtaka Janeth Mgome, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa, ili liwe fundisho kwa wengine ambao wana tabia ya aina hiyo. 

Utetezi wa mtuhumiwa huyo uliwavunja mbavu watu waliokuwapo mahakamani hapo, kwani alitaka kupunguziwa adhabu kwa kuwa mtoto wake ana miaka 14 na miezi tisa na siku tisa, siyo miaka 15 kama ilivyodaiwa mahakamani hapo

Mtoto wa Michael Jackson aanza kufuata nyayo za baba yake.

Mtoto wa nyoka ni nyoka tu.

Hatimaye mtoto wa Michael Jackson, Pris Jackson (18) ameanza kufuata nyayo za baba yake kwa kuanza kutoboa ulimi. Paris amepost picha inayomuonyesha akiwa ametoboa ulimi na kuweka kipini na kuandika: “almost like ring-toss. but with noodles and needles.”

Miaka kadhaa nyuma kabla ya kufariki, Michael Jackson aliwahi kujibadili muonekano wake wa ngozi na kuzua maswali mengi kwa mashabiki duniani.

TAJIRI ANUNUA NDEGE YA ZAMANI NA KUISAFIRISHA KWA KUTUMIA USAFIRI WA MAJINI



Ndege aina ya Boeing 767 imeanza safari kwa kubebwa na chombo cha baharini kinachovutwa na boti kuelekea eneo ambalo itabadilishwa matumizi yake na kutumika kama kivutio nchini Ireland.
Mfanyabishara David McGowan ameinunua ndege hiyo ya zamani ya abiria kwa paundi 16,000 za Uingereza, ambayo inaumri wa mika 30, kutoka uwanja wa ndege wa Shannon.
Awali ndege hiyo yenye uzito wa tani 50, ilikuwa isafirishwe kwa njia ya barabarani, lakini maafisa usafirishaji walimueleza tajiri huyo italeta usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara.

Crane yenye uzito wa tani 150, ilitumika kuibeba ndege hiyo na kuiweka kwenye chombo cha majini

Safari ya kuelekea Ireland ikiendelea kama inavyoonekana hapa

GIGY MONEY AFUNGUKA MAZITO KUHUSU GADNER



MUUZA nyago kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Giggy Money’ amefunguka kuwa mtangazaji maarufu Bongo anayeuza maneno katika Kituo cha Redio cha Clouds FM, Gardner 
G. Habash hachomoki kwake na hadi sasa wako kwenye uhusiano wa mapenzi kwa muda wa miezi sita, Risasi Jumamosi  linakumwagia ubuyu wote. Akichonga na gazeti hili baada ya picha zinazomuonesha akiwa kwenye mapozi ya kimahaba na Gardner kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Giggy alisema mtangazaji huyo amekuwa mtu wa muhimu kwake kwa sasa. “Kwani kuna tatizo nikiwa na Gardner? Yule ni mtu muelewa na sahihi kwangu, ninafikiri kupitia yeye nitajifunza mambo mengi na kuzidi kufanikiwa kwa sababu yeye ni moja kati ya watu ambao wako kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu,” alisema Giggy Money.

Gazeti hili lilimtafuta pia Gardner ili aweze kufungukia ubuyu huo, alipopatikana alisema; “Nipo karibu na Giggy lakini hatuna uhusiano wa kimapenzi, kwa hiyo kama anasema hivyo si kweli lakini yeye ni shabiki wangu na mimi ni mshabiki wake, ninapenda pia kazi anazozifanya,” alisema Gardner

Rais Magufuli ataja mali zake zote anazomiliki.

RAIS John Magufuli amewasilisha orodha ya utajiri wake kwa Sekretarieti ya Madili ya Viongozi wa Umma, kama Sheria inavyomtaka.
 

 RAIS John Magufuli

Magufuli aliyeingia Ikulu Novemba 5, mwaka jana, alikuwa Mbunge ama waziri kwa miaka 20 mfululizo, akitumika kama Naibu Waziri wa Ujenzi na baadaye Waziri kamili kwenye Wizara mbalimbali.
Kamishna wa Tume ya Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda alilieleza Nipashe katika mahojiano maalum hivi karibuni kuwa Rais Magufuli alishawasilisha kwenye tume hiyo orodha ya mali alizonazo.
Jaji Kaganda alisema Rais Magufuli aliwasilisha fomu inayoonyesha mali alizozipata kwa muda wote alipotumikia nyadhifa mbalimbali serikalini, kabla ya kuingia Ikulu.

Nipashe lilizungumza na Jaji Kaganda kujua kama Rais Magufuli alishatoa tamko kama Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 na kanuni zake zinazoeleza, lakini pia kufahamu idadi ya mali anazomiliki Rais huyo na thamani yake.
Kaganda alisema ni kweli Rais Magufuli aliorodhesha mali zake zote katika tume lakini alikataa katakata kumtajia mwandishi mali zlizomo kwenye tamko hilo.

Kaganda alisema Sheria inazuia kumwonyesha mtu mwingine mali za mtumishi wa umma hadi kuwe na sababu ya maana ya anayehitaji, na pia kuwe na ulazima wa kufanya hivyo.

“Mwananchi anaweza kupata taarifa za mali za viongozi kwa kufuata utaratibu uliopo, lakini baada ya kupata taarifa hizo, haruhusiwi kuzitangaza au kuzichapisha kwenye vyombo vya habari,” alisema Jaji Kaganda.
Rais Magufuli amekuwa tofauti na marais waliopita baada ya kuonyesha msisitizo kwa viongozi wa umma kujaza fomu hizo na kuzirudisha kwa wakati.

Katika kuonyesha msisitizo katika jambo hilo, Rais Magufuli kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Februari 26, mwaka huu aliwatangaza mawaziri ambao hawakujaza fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni, na kuwapa saa nane hadi saa 12:00 jioni wawe wamejaza na kurudisha fomu hizo.

Viongozi hao walitajwa kuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, January Makamba, ambao wote hawakuwa wamerudisha fomu za rasilimali na madeni na fomu za ahadi ya uadilifu, kwa wakati huo.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga hakuwa amerudisha fomu ya Ahadi ya Uadilifu. Mwingine alikuwa ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ambaye hakuwa amerudisha fomu ya tamko la rasilimali na madeni, na Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina ambaye hakuwa amerudisha fomu zote mbili.

SHERIA INASEMAJE?
Kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 kifunga 9(1), “Kila kiongozi wa umma atatakiwa katika kipindi cha miezi mitatu au katika kipindi cha siku thelathini baada ya kupewa wadhifa, mwisho wa mwaka au mwisho wa kutumikia wadhifa wake:
kumpelekea kamishna tamko la maandishi katika hati rasmi linaloorodhesha mali au rasilimali zake.” Aidha, kifungu namba 9(6) kinaeleza kuwa “Wakati wa kutoa tamko la rasilimali zake kwa mujibu wa fungu hili, kiongozi wa umma atatakiwa:
(a)kutaja thamani ya mali aliyotamka na chanzo au namna alivyopata mali hiyo. Kifungu namba 11 (2) cha sheria hiyo, kinaeleza kuwa rasilimali zinazotakiwa kutajwa ni pamoja na:

Nyumba, mali ya starehe na mashamba yanayotumiwa au yanayotarajiwa kutumiwa na viongozi wa umma au familia zao. Rasilimali nyingine ni kwa mujibu wa kifungu 2(b) ni kazi za sanaa, mambo ya kale na vitu alivyonunua kidogokidogo, (c) magari na aina nyingine binafsi za usafiri kwa matumizi binafsi, (d) fedha taslimu na amana zilizowekwa benki au taasisi nyingine za fedha, (e) hawala za hazina na uwekezaji mwingine katika dhamana zenye thamani maalumu, zinazotolewa au kudhaminiwa na serikali au wakala wa serikali.
Mwezi uliopita Jaji Kaganda aliiambia Nipashe kuwa naye Rais mstaafu Jakaya Kikwete alitangaza utajiri wake kwa sekretarieti hiyo ya maadili punde baada ya kung’atuka, lakini sekretarieti hiyo ilikataa kutaja mali hizo.

MAGUFULI AKASIRIKA KUDANGANYWA MASHINE JNA MBOVU
RAIS John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza na kubaini ‘madudu’ katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Jiulius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Alibaini madudu hayo jana alipofanya ziara hiyo ya ghafla katika uwanja huo, akiwa ametua akitokea jijini Kampala, Uganda alikokwenda kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni.

Rais Magufuli alibaini kuwa mashine za ukaguzi za sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi kazi kwa muda mrefu na ofisa mmoja wa uwanja huo alijaribu kumdanganya kuwa ni nzima. Maofisa wa uwanja huo waliokuwa wakitoa taarifa kwa kutofautiana katika maelezo yao ndio waliomkera Rais Magufuli na kuanza kuwahoji maswali ambayo walishindwa kujibu.
Ofisa mmoja alimweleza Rais Magufuli kuwa mashine hizo zinafanya kazi na mwingine alisema kuwa hazifanyi kazi kwa muda mrefu.

Kutofautiana kwa maelezo hayo kulimfanya Rais Magufuli kuwa mkali na kuanza kumfokea ofisa aliyemdanganywa kwamba mashine hizo zinafanya kazi.
“Unajua mimi sipendi kudanganywa, ni vizuri uzungumze ukweli tu, kwanini nimeanzia hapa huwezi kujiuliza?” Alihoji Rais Magufuli.
“Sasa nakwambia sipendi kudanganywa, ukinidanganya nitachukia sasa hivi, wewe umenidanganya kwamba hiyo hiyo ndiyo mbovu na hii ni nzima nikawaambia muiwashe hiyo nzima, amekuja huyu mwenzako amezungumza ukweli kabisa, akasema hii ni mbovu kwa miezi miwili.
“Kwa hali hii mizigo inayopitia hapa huwa hamuikagui kwa namna yeyote ile, kwa hiyo mimi nikiamua kuja na dawa za kulevya, nikaja na dhahabu zangu na almasi zangu na pembe za ndovu napita tu?” aliendelea kuwabana maofisa hao ambao walikosa cha kujitetea.
Rais Magufuli aliagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja dhidi ya dosari hizo alizoziona.

(CHANZO: NIPASHE)

Undani kifo cha Kinyambe huu hapa

WAKATI mwili wa msanii wa vichekesho James Peter Nsemwa maarufu kama Kinyambe ulitarajiwa kuzikwa jana katika Makaburi ya Uyole mkoani 

Kwa mujibu wa baba wa marehemu, mzee Lugendelo Nsemwa, mwanaye aliyejipatia umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa uchekeshaji, alianza kuumwa tangu Juni mwaka jana, ambapo tumbo na miguu ilikuwa ikijaa maji. Alisema tatizo hilo lilisababisha mapafu yake kushindwa kufanya kazi sawasawa.


Jeneza lenye mwili wa marehemu Kinyambe.

“Kwa kipindi kirefu alikuwa amelazwa katika hospitali binafsi ya Abaja iliyopo Uyole, lakini Mei 9, mwaka huu hali yake ilibadilika, alizidiwa na kupoteza fahamu, kitu kilichotufanya tumkimbize katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya iliyopo maeneo ya Forest ya zamani, ambako alilazwa katika wodi ya ‘private’ chumba cha peke yake na bahati mbaya Jumatano saa 3.5 akafariki dunia,” alisema mzazi huyo.

Katika hali ya kushangaza, mzazi huyo alisema jina la Mohamed Abdalah, ambalo linafahamika kwa wengi kama ndilo halisi la msanii huyo, yeye halitambui, kwani tangu amezaliwa alipewa jina hilo na hakuwahi kusikia kama alilibadili.

Aidha, aliwalaumu wasanii wenzake kwa kutotoa msaada wowote wakati wa ugonjwa, kwani kwa kipindi chote hakuwahi kuwaona wasanii wa Dar es Salaam wala kupata salamu zao, zaidi ya kuwaona wale wa Mbeya ambao nao walikuwa wakienda mara mojamoja.

Daktari mmoja wa hospitali hiyo aliyemhudumia marehemu tangu alipolazwa, ambaye jina lake linahifadhiwa kwa kuwa siyo msemaji wa hospitali hiyo, alisema marehemu alipopokelewa na kupimwa, aligundulika kiwango cha sukari kuwa chini huku pia akiwa na homa ya mapafu.

Wakati wa uhai wake, Kinyambe aliwahi kuishi na wanawake watatu, ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja, lakini imefahamika kuwa wa kwanza alizaa naye mtoto mmoja, wa pili alizaa naye mtoto mmoja pia, lakini alifariki mwezi uliopita akiwa na miaka minne. Mwanamke wake wa mwisho ni mjamzito ambaye endapo Mungu atamjaalia, atajifungua mwezi ujao.
Marehemu alijipatia umaarufu kwa vichekesho vyake kupitia vipindi mbalimbali vya televisheni, kikiwemo cha Vituko Show katika Channel Ten na pia aliwahi kufanya kazi na Sharo Milionea.
Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi!  SOURCE.GLOBAL PUBLISHERS

Lady Jaydee kumshtaki Gadner Mahakamani..Amtaka Gadner Kuomba Msamaha Mbele ya Umma


Lady Jay Dee sasa ameamua kumshtaki aliyekuwa mumewe ambaye ni mtangazaji wa kiruo cha redio cha Clouds Garner  G Habash baada ya hivi karibuni Gardner kutoa kauli zilizodaiwa kumdhalilisha jide.soma waraka huu hapa chini kutoka mahakamani.


Serikali yasitisha ajira kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa muda.


WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesitisha kwa muda ajira zote kwenye vyombo vya ulinzi na usalama vilivyomo ndani ya wizara hiyo, ikiwemo Jeshi la Polisi ili kupitia upya utaratibu wa kutoa ajira na kuondoa uwezekano wa watu wasio na sifa kujipenyeza.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alisema hayo jana bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (Chadema), aliyetaka kufahamu ni kwa nini Serikali inasitisha ajira katika Jeshi la Polisi, wakati bado nchi inakabiliwa na uhaba wa askari ndani ya jeshi hilo wakiwemo askari wa kike.

“Tumesitisha kutoa ajira ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ili kuondoa uwezekano wa watu wasio na sifa kujipenyeza na kupata ajira ndani ya vyombo vilivyo chini ya wizara hiyo,” alisisitiza.

Miongoni mwa vyombo hivyo vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mbali na Jeshi la Polisi ni Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uhamiaji. Mbali na Komu, Mbunge mwingine ambaye ni wa Viti Maalumu, Hawa Mwaifunga (Chadema), alitaka kufahamu Serikali inachukua hatua gani kuhakikisha askari wasio na sifa wanachukuliwa hatua, ambapo pia alitaka kufahamu utaratibu wa uhakiki vyeti vya askari wasio na sifa ndani ya Jeshi la Polisi umefikia wapi.

Akizungumzia Jeshi la Polisi, Masauni alisema Jeshi la Polisi limo kwenye utaratibu wa kuwachukulia hatua za kisheria askari wachache, wanaochafua taswira na kazi nzuri inayofanywa na Polisi kwa kukiuka sheria, kanuni na taratibu kwa kujihusisha na vitendo vinavyokinzana na maadili.

Kuhusu uhakiki wa vyeti, waziri huyo alielezea kuwa, uhakiki huo unahusu askari wasio na sifa ndani ya Jeshi la Polisi unaendelea na mpaka sasa, askari 19 wamechukuliwa hatua za kisheria baada ya kugundulika kuwa walipata ajira kwa njia zisizokubalika.

Kuhusu uhaba wa askari wa kike, Waziri huyo alikiri kuwa kuna uhaba wa askari wa kike katika Jeshi la Polisi na kutoa mwito kwa wanawake wahamasike zaidi kujiunga na vyombo vya usalama.

Mwaka jana Idara ya Uhamiaji iliyokuwa chini ya Wizara hiyo, ililazimika kufuta ajira mpya 200 za makonstebo na makoplo, baada ya kubaini upatikanaji wa ajira hizo, ulifanyika kwa upendeleo.

Magazeti ya tanzania yalichoandika leo tar 14.5.2016 kwenye habari za kitaifa,kimataifa,udaku na michezo.

Jumamosi ya Mei 14 naanza kwa kukuletea habari zilipewa kipaumbele kwenye magazeti ya Leo.usiache kukaa karibu nasi kwenye mitandao ya kijamii yaani facebook /Tanzaniampyasasa blog na twitter@tanzaniampyasasa.


 

Gallery

Popular Posts

About Us