KINGAZI BLOG: 05/28/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Saturday, May 28, 2016

Wimbo wa 'Panya' Wakiponza Kitua cha EATV, Chapigwa Faini ya Milioni 3 na TCRA


Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imevitoza faini vituo vya East Africa Television na Entertaiment FM (E- FM) baada ya kukiuka kanuni za utangazaji.

Akisoma nakala ya hukumu hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema baada ya kupitia maelezo ya utetezi kutoka kwa viongozi wa vituo hivyo, kamati hiyo imeamua kuitoza EATV faini ya Sh3 milioni na Sh4 milioni kwa E-Fm.

“Pamoja na adhabu hiyo tumetoa onyo kali kwa kukiuka kanuni ya maudhui, lakini pia endapo kosa hili litajirudia tunaahidi kutoa adhabu kali zaidi,” alisema.

Katika maelezo ya awali ya hukumu hiyo, Mapunda alisema adhabu ya EATV imetolewa baada ya kituo hicho kupitia kipindi chake cha muziki mnene kurusha video ya wimbo wa Panya wa kundi la muziki la Bracket kutoka nchini Nigeria uliomshirikisha msanii Techno.

“Baadhi ya mavazi yaliyotumika katika wimbo huo hayaendani na maadili ya Kitanzania. Na kwa upande wa E-FM wameadhibiwa baada ya kurusha kipindi cha Ubaoni kilichotoa simulizi ya msichana mchawi aliyekiri kuua,”alisema Mapunda.

Baada ya kupokea nakala ya hukumu hiyo, Mkurugenzi wa EATV, Regina Mengi alisema hawana tatizo na adhabu hiyo na kwamba, atalifikisha suala hilo kwa uongozi wa kampuni yao.

“Bado siwezi kujibu lolote, uamuzi wa kuikubali au kukata rufaa itategemea na uamuzi wa bodi,” alisema.

Mkurugenzi wa E-FM, Scolastica Mazula alisema ameridhishwa na hukumu iliyotolewa, hivyo haoni kama kuna sababu ya kukata rufaa.

Mamlaka hiyo imevitaka vyombo vyote vya utangazaji nchini kuzingatia maadili na taratibu za sheria zinapofanya kazi ili kuepuka kuleta athari katika jamii.

Waziri atangaza Kiama wenye elimu feki

Dodoma. Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali itafanya msako katika vyuo vyote nchini ili kubaini wanafunzi waliodailiwa bila kuwa na sifa kama ilivyotokea kwa wanafunzi 480 wa Chuo Kikuu cha St Joseph.

Vilevile, amesema msako kama huo utafanyika katika maeneo ya kazi ili kubaini wafanyakazi walioajiriwa bila kuwa na sifa stahiki.

Profesa Ndalichako alisema hayo jana jioni wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge walizotoa wakati wa mjadala wa bajeti yake ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2016/17.

“Kazi ndiyo imeanza, haitoishia hapo (St Joseph) itakwenda na vyuo vingine. Wanaotumia vyeti wajitokeze wenyewe. Hata huko kwenye ofisi za Serikali tutafika kufanya ukaguzi,” alisema Profesa Ndalichako na kuongeza, “Inawezekana hata hapa bungeni wapo.”

Kauli hiyo ya Waziri ilitokana na michango ya wabunge waliokuwa wanahoji kuhusu hatua ya Serikali kufuta udahili wa wanafunzi wa St Joseph iliyokwenda sambamba na kuvunja Kamisheni ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.

Ada elekezi
Awali, katika mjadala, wabunge kadhaa, wakiwamo waliokuwa naibu mawaziri wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete waliitaka Serikali kuacha kuzibana shule binafsi kwa kuweka ada elekezi badala yake iboreshe mazingira ya shule zake na masilahi ya walimu ili wazazi wasione haja ya kuwapeleka watoto wao huko.

Mawaziri hao ni Philipo Mulugo aliyekuwa naibu waziri wa elimu na Daniel Nsanzungwanko aliyekuwa naibu waziri wa habari, utamaduni na michezo katika baraza la kwanza la Kikwete.

Katika mchango wake, Mulugo ambaye ni Mbunge wa Songwe (CCM), alisema wamiliki wa shule binafsi wanaendesha shule zao kwa kupata mikopo benki na pia wanalipa kodi kubwa serikalini, jambo linalowafanya kuwa katika wakati mgumu.

Aliitaka Serikali iziache shule binafsi zishindane zenyewe kwa viwango vya ada vinavyoendana na ubora wa mazingira na elimu inayotolewa.

Alisema Serikali imeweka mazingira magumu kwa walimu kutoka nje ya nchi kufundisha wakati hakuna hapa nchini walimu wanaoweza kufundisha shule zinazotumia Kiingereza.

“Mpaka sasa Tanzania haina chuo kinachofundisha walimu kwenda kufundisha kwa kutumia lugha ya Kiingereza. Serikali imeweka wigo kwa shule binafsi bila kuangalia umuhimu wa shule hizi,” alisema Mulugo ambaye pia ni mmiliki wa shule.

Mulugo aliishauri Serikali kuanzisha mamlaka huru ya udhibiti wa elimu ili kusimamia viwango na ubora wa shule zote nchini za umma na zile binafsi.

Alisema shule za umma zinaanzishwa wakati hazina viwango vya ubora vinavyotumika wakati wa kuanzisha shule binafsi. Alisema kukiwa na mamlaka huru, shule yoyote haiwezi kuanzishwa kama haijakidhi viwango vya ubora hata kama ni ya umma.

“Anayewalipa walimu ni Wizara ya Fedha; anayesimamia ubora wa elimu ni Tamisemi; anayepandisha vyeo walimu ni Utumishi; anayesimamia sera ya elimu ni Wizara ya Elimu. Kuna haja ya kuwa na chombo kimoja kitakachosimamia mambo yote haya,” alisema.

Nsanzugwanko ambaye ni Mbunge wa Kasulu (CCM), alisema kuweka ada elekezi ni kuwaonea wamiliki wa shule binafsi ambao alisema wana mchango mkubwa katika sekta ya elimu nchini.

“Serikali ikae na wamiliki wa shule binafsi ili wakubaliane namna ya kuendesha elimu. Zamani ilikuwa fahari kwa mwanafunzi kusoma shule za umma na aliyekwenda kusoma shule za binafsi alionekana amefeli. Serikali ikae na kujiuliza maswali ilikosea wapi?” alisema.

Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola alisema ada elekezi hazina maana kwa sababu ya soko huria, hivyo badala ya kuishusha Serikali inatakiwa kuboresha shule zake ili ziingie kwenye ushindani na shule za binafsi.

Aliitaka Serikali kuwa na utaratibu wa kuwajengea uwezo walimu ili Taifa liwe na walimu wazuri.

Alisema bila kujenga msingi bora wa walimu, elimu bora haitapatikana hata kukiwa na mazingira bora ya kufundishia.

“Zamani wazazi walipeleka watoto wao kusoma Kenya na Uganda, hali ilikuwa mbaya hapa nchini. Leo shule hizi (binafsi) zimeanza kufanya vizuri, mnataka kuzivuruga tena? Serikali iachane na mpango huo,” alisema Lugola.

Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Jesca Kishoa alisema viongozi wa Serikali hawaoni uchungu wa elimu nchini kwa sababu watoto wao hawasomi shule za umma, bali kwenye shule binafsi na wengine nje ya nchi.

“Ninamuomba Rais atangaze kwamba watoto wote wa mawaziri wasome shule za Serikali. Ni aibu kuona tunajadili namna ya kuinua shule zetu wakati watoto wa viongozi wetu hawasomi katika shule hizo,” alisema.

Watumishi Wavaa Vimini, vipedo, t-shirt, Jeans Kufyekwa Mshahara

HALMASHAURI ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, imepiga marufuku watumishi wote wa halmashauri hiyo kuvaa mavazi ambayo hayana maadili katika sehemu za kazi na kwamba atakayebainika atarudishwa nyumbani na kukatwa mshahara wa siku husika.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Adriano Jungu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Bomani wilayani Muheza juzi.
  
Alisema lazima mtumishi ahakikishe staha ya mavazi aliyovaa kabla hajaingia kazini katika ofisi yake na kwamba mtumishi atakayekiuka kuvaa mavazi ambayo hayaendani na maadili sehemu ya kazi atachukuliwa hatua za kinidhamu.
  
Akieleza zaidi, Jungu alisema kuwa mavazi ambayo hayaruhusiwi kwa watumishi ndani ya halmashauri yake ni pamoja na fulana, suruali za jeans, vimini, vitop, Pedo, yeboyebo, kaptula (pensi) na kandambili kwa sababu kuvaa vyote hivyo ni kinyume cha maadili ya utumishi.
  
Alisema kuwa mtumishi yeyote katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kabla ya kuingia kazini lazima aangalie mavazi aliyovaa na kwamba sheria iko katika waraka wa utumishi wa umma namba 3 wa mwaka 2007 na lazima watumishi waheshimu waraka huo.
  
Jungu alisema mtumishi yeyote katika halmashauri ya Wilaya ya Muheza ambaye atakiuka sheria hiyo kwa kuvaa nguo za kihuni wakati wa kuingia kazini basi atarudishwa nyumbani na atakatwa mshahara wake wa siku hiyo.
  
Alisema kuwa lazima watumishi waheshimu sehemu ya kazi kwa kuvaa nguo za heshima ikiwamo wanawake na wanaume kwa kuwa ofisi hizo wanaingia watu wenye heshima ikiwamo wazee sasa haiwezekani mtumishi mwanamke anaingia ofisini na kimini kinachofika katika magoti na hivyo mapaja yake yanaonekana sasa anamtamanisha nani.
  
Jungu alisema kuwa kwa wanaume nao lazima wawe na nidhamu ya kuvaa mavazi ya heshima na siyo kuvaa mavazi ya jeanz mlegezo na flana zinazowabana ni marufuku kabisa katika halmashauri ya Muheza.
  
Alisema ataanza kupita kila ofisi Jumatatu Mei 30 asubuhi kwa ajili ya kuwakagua mavazi yao watumishi hao wakiwamo wanawake na wanaume ili kukomesha tabia kama hiyo ambayo ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma hapa Tanzania.
  
Jungu alitoa onyo kwa kupiga marufuku watumishi kufika kazini wakiwa wamelewa na mtumishi akibanika amefanya hivyo na ushaidi upo atampeleka hospitali kupimwa na akibainika atamtumbua jipu hadharani kwani serikali ya awamu ya tano ni ya hapa kazi tu.

Ali Kiba Apata Mpenzi Mwingine, Asema: Nikimrudia Jokate nisutwe

King-KibaStaa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’
 Siku chache baada ya kusaini mkataba wa kimataifa na Kampuni ya Sony, Staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amedaiwa kufunguka kuwa, kamwe hawezi kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake na akifanya hivyo asutwe mchana kweupe.
kiba na jokateeKiba na Jokate.

Chanzo makini ambacho kipo karibu na msanii huyo kimeeleza kuwa, staa huyo amegundua alipotea njia kwenye penzi la Jokate hivyo hana sababu ya kurudi nyuma kwani huu ndiyo wakati wake wa kufanya mambo makubwa.
“Jamaa tangu asaini mkataba mpya na Sony, hataki kuutia doa. Amesema anataka kutusua kimataifa zaidi hivyo anaona akirudi kwa Jokate ni kama atakuwa amerudi alikotoka kisanii.
“Unajua amejifunza mambo mengi kipindi yupo na Jokate, hataki tena kurudi kule kwani kusaini kwake mkataba mkubwa anataka kuendane na maisha yake binafsi,” kilisema chanzo chetu.
jokate12Jokate Kidoti ‘Jojo’

Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, mbali na kula mkataba mnono, Kiba tayari amempata mpenzi mpya ambaye wanaendana kwa kila kitu hivyo anaona ni wakati mzuri wa kufaidi maisha ya uhusiano sambamba na maisha yake kimuziki.
“Ni mtoto f’lani mwenye maadili. Kama unavyojua Kiba ni mtoto wa Kiislamu, safari hii ameona achukue binti mwenye imani kama yake ili aweze kufika mbali maana japo hana mpango wa ndoa kwa sasa lakini anataka mtu ambaye ataishi naye kwa muda mrefu,” kilisema chanzo hicho.
KUFANYA MAMBO MAKUBWA
Chanzo hicho kilizidi kuweka bayana kuwa, Kiba ameapa kufanya mambo makubwa kwani amepata uongozi mzuri ambao unajua kuongoza wasanii na kuwaunganisha na televisheni za kimataifa.
“Kiba kwa sasa ngoma yake inachezwa kimataifa, juzikati kupitia televisheni ya Sound City Africa ambayo makao makuu yapo Nigeria, walitoa saa 12 kwa ajili ya Kiba, wakaiita Ali KibaDay, hapo zilichezwa nyimbo zake tu, ni nafasi kubwa sana ya kujitangaza, imempa connection nyingi za kimataifa,” kilisema chanzo hicho.
DIAMOND ATASUBIRI SANA
Chanzo hicho kilizidi kummwagia sifa Kiba kuwa kutokana na uwezo, uongozi na mkatapa huo mpya, sasa hivi  Diamond atasubiri sana kwani levo zake zitakuwa za mbali.
“Aaah! Diamond atasubiri sana. Kiba anabebwa na vingi kwa sasa, uongozi mzuri na anajua kuimba kuliko huyo Diamond. Ataisoma namba kama unavyosikia wimbo wa Aje ndani ya muda mfupi tu, tayari umekamata,” kilisema chanzo hicho.
MENEJA AFUNGUKA
Baada ya kushibishwa ubuyu huo, mwanahabari wetu alimvutia waya mmoja wa mameneja wa msanii huyo ambaye hapendi jina lake lichorwe gazetini kwa kile alichodai si mambo ya muziki aliyoulizwa, lakini akaweka bayana kuwa kweli Kiba hayupo tayari kurudiana na Jokate kwani ana mtu wake mpya.
“Hawezi kumrudia, sijui hata amemchukia nini yule mrembo (Jokate). Jamaa kwa sasa ana kifaa kipya lakini hapendi kukiweka wazi. Si unajua naye alivyo mtu wa sirisiri,” alisema meneja huyo.
KIBA ANASEMA
chanzo hiki lilimtafuta Kiba ili kuweza kumsikia anazungumziaje juu ya mrembo huyo na kama kweli hana mpango wa kurudi nyuma hadi kufikia hatua ya kutamka kuwa asutwe kuliko kurudina na mrembo huyo, Kiba alijibu kwa kifupi:
“Haya ni mambo yangu binafsi. Sipendi sana kuyazungumzia. Kifupi wewe elewa kwa sasa siwezi kurudi nyuma, nipo kwenye hatua nyingine za kimaendeleo na namshukuru Mungu nakubalika.”
YA AWALI
Miaka miwili iliyopita, Kiba na Jokate wamekuwa habari kwenye vyombo vya habari wakidaiwa kuwa wapenzi licha ya kwamba, mara nyingie alikuwa akikanusha huku mwenzake akiwema wazi.
Hata hivyo, maisha yao ya kimapenzi yamekuwa yakitawaliwa na mlolongo wa kumwagana na kurudiana.
Kuna wakati ilidaiwa Jokate alinasa mimba ya Kiba lakini baadaye ikasemekana kuchoropoka.
Maneno mengi yalisemwa kuwa,  hakuna tumaini la mbele katika uhusiano wao kwa vile, Jokate ni Mkristo, Kiba Muislam huku familia ya mrembo huyo ikitajwa kutokuwa tayari binti yao kuingia kwenye ndoa na mwanaume wa imani tofauti.
Kumwagana kwa safari hii na Kiba kupata kifaa kingine kunahitimisha ‘kapo’ yao iliyodumu kwa miaka mitatu sasa.

VIDEO:Mkuu wa Mkoa Afumaniwa Akifanya Mapenzi na Mwanae


Mkuu wa zamani wa Mkoa wa Kaskazini Pemba na mshauri wa Rais wa Zanzibar kisiwani humo, Dadi Faki Dadi amekamatwa akituhumiwa kufanya mapenzi na mtoto wake wa kambo.

Dadi alikamatwa juzi akidaiwa kukutwa na mtoto huyo wa mkewe wa ndoa mwenye umri wa miaka 21 katika nyumba ya kulala wageni inayoitwa Executive, jirani na makao makuu ya Uhamiaji Zanzibar katika eneo la Kilimani chini na Maisara, mjini Unguja.

Mwanasiasa huyo alijikuta akipigwa pingu na polisi akiwa kifua wazi mbele ya mkewe na wanafamilia na kisha kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Mwembemadema.

Picha za video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zilimwonyesha Dadi akikabiliwa na mashambulizi makali ya maneno kutoka kwa watu waliomkamata, akiwamo mkewe.

“Mwacheni avae nguo kwanza, mpeleke bwana, twende bwana..." ni baadhi ya maneno yanayosikika katika video iliyorekodiwa wakati wa kumtia mbaroni.

Taarifa zilizopatikana miongoni mwa wanafamilia ya kiongozi huyo, zilidai kwamba alikamatwa baada ya kumtilia shaka binti huyo kutokana na mienendo yake ya hivi karibuni na kuamua kumfuatilia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha kumshikilia Dadi kwa muda kabla ya kumwachia kwa dhamana.

“Kijamii alitenda kosa, lakini sisi tunaendelea kufanya uchunguzi, iwapo tutabaini ametenda kosa la kisheria na anaweza kuwa mashtaka tutamkamata ili kumpeleka katika vyombo vya sheria,” alisema Mkadam.

Mmoja wa wanafamilia ambaye aliomba jina lake lisitajwe alisema: “Mwizi siku zake ni arobaini, tulimtega na hatimaye tumemnasa sasa tuone mwisho wake utakuwa nini na kipi kitajiri baadaye.” Tazama Video:

Gigy Money sikio la kufa

KUONESHA kwamba haoni wala hasikii, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amezidi kutia fora kwa kunaswa na wanaume tofauti safari hii, ametupia picha kimahaba akiwa na msanii wa Singeli, Amani Fongo.

Gigy ambaye amekuwa akitupia picha za nusu utupu katika Mtandao wa Instagram pamoja na kuwa kimahaba na wanaume tofauti kama staa wa Bongo Fleva, Seif Shaban ‘Matonya’, mtangazaji Gardner G. Habash na Idris Sultan, amepondwa vibaya baada ya kutupia picha mpya ya Fongo.

“Huyu kama vile hana wazazi sasa tumueleweje, mara Gardner mara Matonya yaani sijui ndiyo kiki au vipi,” aliandika mdau mtandaoni huku Gigy mwenyewe akidai aachwe kwani ndiyo maisha yake.
GPL
 

Gallery

Popular Posts

About Us