KINGAZI BLOG: 05/08/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, May 08, 2016

Abiria 73 Wametekea Hadi Kufa Katika Ajali ya basi kugongana na Lori la mafuta



Abiria 73 wametekea hadi kufa katika ajali mbaya iliyohusisha mabasi mawili ya uchukuzi wa umma na lori la kubeba mafuta nchini Afghanistan. Msemaji wa wizara ya afya alieleza kuwa watu kama 70 walikufa...na kwamba wengi waliteketea na hawatoweza kutambulika.
Wakuu wa Afghanistan wanasema kuwa idadi inazidi kuongezeka ya watu waliokufa katika ajali hilo lililotokea katika barabara ya mji mkuu wa Kabul kuelekea mji ulioko kusini wa Kandahar. Abiri wengine walipelekwa hospitalini katika jimbo la Ghazni.
Ajali za barabarani ni kawaida nchini Afghanistan ambapo madereva wanamazowea ya kukaidi kanuni za barabarani na pia maafisa wa kuelekeza magari ni mwachache mno. Mwandishi wa BBC aliyeko huko Mahfouz Zubaide anasema kuwa magari hayo matatu yalikuwa yanaendeshwa kwa kasi mno.
Mohammadullah Ahmadi, mkurugenzi wa trafiki wa mkoa huo analaumu utundu wa madereva kwa ajali hiyo. Anasema kuwa kwa jumla kulikuwa na abiria 125 katika mabasi hayo mawili.
Msemaji wa idara ya afya Ismail Kawasi anasema kuwa itakuwa vigumu kuwatambua kwani walioteketea ,waliteketea kabisa.

6

Floyd Mayweather Kurudi Tena Ulingoni, Kuzichapa na Staa wa UFC, Conor McGregor


FLOYD MAYWEATHER na staa wa UFC, Conor McGregor wapo mbioni kuingia ulingoni kuzichapa kwenye pambano kubwa na aghali zaidi la masumbwi katika historia.

Gazeti la The Sun limedai kuwa Mayweather, anatarajia kuzichapa na staa huyo jijini Las Vegas mwaka huu.

Mayweather alitangaza kustaafu ndondi akiwa ameshinda mapambano yote 49 aliyowahi kupigana. Kwenye pambano hilo Mayweather atachukua paundi milioni 100 huku McGregor atachukua paundi milioni 7.

Tangazo rasmi litatolewa wiki chache zijazo.

Chanzo kililiambia gazeti la The Sun kuwa Floyd alichukia baada ya Conor kudai anaweza kumtwanga KO ndani ya sekunde 30 tu na sasa anataka kumuonesha kazi.

Kwa Hali Hii ni ‘Ni Ndoto Tanzania Kuwa na Uchumi wa Viwanda


Wabunge wamesema ni vigumu Tanzania kufikia lengo la kuwa na uchumi wa viwanda iwapo Serikali itaendelea kusuasua kutekeleza miradi yenye mchango mkubwa katika sekta hiyo.

Akisoma maoni ya Kamati ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka 2016/17, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Vicky Kamata alisema hawaridhishwi na namna Serikali inavyotoa fedha za bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

“Kwa kuzingatia takwimu hizi ni dhahiri miradi mingi ya maendeleo iliyopangwa kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha haitatekelezwa,” alisema Kamata.

Alisema kamati hiyo inaunga mkono dhamira ya Serikali ya kuifanya nchi kuwa ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025 lakini hairidhishwi na kasi ya utekelezaji wa azma hiyo.

“Hali hii ikiendelea itakuwa vigumu Tanzania kuwa nchi ya viwanda iwapo Serikali itaendelea kuchelewesha utekelezaji wa miradi yenye mchango mkubwa katika sekta hii,” alisema.

Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu alisema: “Kamwe tusijiaminishe kuwa tunaweza kufikia Taifa la viwanda kwa Sh42.159 bilioni kwenye bajeti ya mwaka kama fedha za maendeleo kwa ajili ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,” alisema.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti bungeni jana Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema kati ya viwanda 106 vilivyofanyiwa tathmini, viwanda 45 vinafanya kazi, 24 vinasuasua na 37 vimefungwa.

“Mpango wetu ni kuhakikisha kuwa viwanda 35 vilivyobaki vinafanyiwa tathmini haraka na kabla ya nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha unaoanza Julai Mosi mwaka huu, hatima ya viwanda visivyofanya kazi itajulikana,” alisema.

Alisema hatima ya wenye viwanda visivyofanya kazi ni kwa wamiliki kutekeleza mkataba ya mauzo au kupewa wawekezaji wapya ili waviendeleze,” alisema.

Wizara hiyo imeomba kutengewa Sh 81.87 bilioni katika mwaka wa fedha 2016/17 kati ya hiyo, Sh41.87 bilioni sawa na asilimia 51 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh40 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

UNYAMA WA KUTISHA! MUME AMKATA NYETI MKEWE ILI AKAZIUZE MIL. 5



Unyama wa kutisha kisa utajiri! Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 (pichani jina linahifadhiwa), anadai kukatwa sehemu zake za siri (nyeti) na mumewe aliyemtaja kwa jina moja la Mashaka ili akauze Sh. milioni tano za Kitanzania akauze kwa mganga wa kienyeji ili apate mtaji.Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 aliyekatwa sehemu zake za siri (nyeti) na mumewe anayefahamika kwa jina moja la Mashaka. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo baya, 

Mwanamke huyo anadai kujeruhiwa na mumewe usiku wakati wakiwa wamelala nyumbani kwao 

Akizungumza na mwanahabari wetu kwa tabu akiwa wodini kwenye hospitali hiyo akiwa na maumivu makali, mama huyo alikuwa na haya ya kusema:

“Siku ya tukio, nakumbuka mume wangu alikwenda kutembea, aliporejea nyumbani alifuatana na mtu mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji.“Walipofika nyumbani aliniambia yupo na mganga wa kienyeji ambaye alikuwa akitafuta viungo vya sehemu za siri za mwanamke akiwa na fedha milioni tano.

Magazeti ya tanzania yalichoandika leo jumapili ya Mei 8 kwenye habari za udaku kitaifa kimataifa. Michezo na stori nyingine kali



MAAJABU YA DUNIA..:, ANGALIA WATOTO WALA MAYAI YA CHURA NA KUZUNGUMZA LUGHA YA AJABU.


Watoto wamekaa na mamayao wakila chakula.nchini Uganda watoto watatu waliofungiwa na baba yao kwa miaka saba wameanza kuzungumza lugha isiyofahamika.

Watoto watatu kutoka kijiji cha Barca katika kaunti ndogo ya Aber Wilayani Oyam nchini Uganda wameanza kuzungumza lugha tofauti isiojulikana baada ya kufungiwa katika nyumba kwa miaka saba.Lugha hiyo mpya imetajwa kuwa Leb -adam ikimaanisha lugha ya ubongo na jamii ya eneo hilo.Inadaiwa kuwa baba ya watoto hao aliwafungia ili kuwalinda kutokana na hatari yoyote.

Kulingana ma gazeti la the monitor nchini Uganda,watoto hao hawajaathirika kiakili lakini hawawezi kuzungumza na watu wengine.Wanaamini tu kile baba yao anachowaambia.

Kulingana na mama yao watoto hao waliweza kuishi kwa kula mayai ya chura yaliochemshwa na majani,ambayo hula kila asubuhi na jioni na hutumia maji kutoka shimo lililochimbwa na baba yao.

Mama yao anasema kuwa baba ya watoto hao alimzuia kutozungumza nao hatua iliowafanya kutojifunza lugha ya kiluo wakati walipokuwa wadogo.

Mwanamke huyo amesema kuwa alionywa na baba huyo kutosema chochote kuhusu watoto hao.via>>BBC

 

Gallery

Popular Posts

About Us