Mnamo msimu wa mwaka 1992-1993 ligi kuu ya nchini England ilianza kutambulika kama ‘ENGLISH PREMIER LEAGUE (EPL) ‘ Ni ligi inayohusisha Club 20, Manchester ikiwa ni moja ya timu ya mpira inayoshiriki katika ligi hiyo.Ni klabu kubwa nchini England na barani Ulaya kwa ujumla, ndiyo club inayoongoza kwa kutwaa kombe hilo ikiwa imechukua mara 13 tangu ligi hiyo iaanze kutambulika kama EPL. Ni klabu ambayo Wanasoka Bora wengi duniani walishawahi kuchezea.
Na namba ya jezi mgongoni imekuwa moja ya alama kwa wachezaji. Leo tutajikita katika kuangalia historia ya jezi namba 6 na tutapata kuona wanasoka mashuhuli ambao walishaivaa jezi hiyo ndani ya Manchester United.
1995-1998 GARY PALLISTER
Mwaka 1989 alisajiliwa kutoka katika klabu ya Middlesbrough na ndio ulikuwa usajili ghali zaidi kwa mchezaji nafasi ya beki, ni beki wa kati aliyeweza kuisaidia timu yake ya Middlesbrough kupanda daraja kutoka ligi daraja la pili hadi ligi daraja la kwanza msimu wa mwaka 1988-1989 kabla ya Manchester United na kukabidhiwa jezi namba 6 mnamo mwaka 1993.
Mlinzi huyo wa kati mwenye asili ya Uingereza atakumbukwa pia kwa kuweza kuipeleka Manchester United fainal katika kombe la FA baada ya kuweza kuisawizishia bao katika dakika za nyongeza za mchezo wa kwanza wa nusu fainal dhidi ya Crystal Palace na kufanya mchezo huo kumalizika kwa kufungana 2-2 na hivyo mchezo kurudiwa na aliweza kuipatia tena goli Manchester United katika ushindi wa 2-0 katika mchezo wa marudiano na kufanikiwa kuipeleka katika fainal ya kombe la FA mwaka 1995.
1998-2001 JAAP STAM
Alisajiliwa kutoka klabu ya nchini kwao Uholanzi klabu ya PSV Eindhoven kwenda kuziba pengo la Gary Pallister ambaye alirejea katika klabu yake ya zamani ya Middlesbrough kwa kiasi cha pauni million 2.5 ikiwa kiasi kikubwa zaidi ya alichosainiwa nacho mara ya kwanza na klabu ya Manchester United. Stam alikabidhiwa jezi namba 6 iliyovaliwa awali na mlinzi wa kati Gary Pallister.
Jaap Stam alisifika kuwa beki mwenye kasi, nguvu na mwenye uwezo wa kuuchezea mpira, aliweza kudumu Manchester United kwa muda wa misimu mitatu na kuweza kushinda mataji matatu ya ligi kuu, taji moja la kombe la FA, kombe la mabara la vilabu pamoja na kombe la mabingwa barani Ulaya.
2001-2002 LAURANT BLANC
Alikuwa ni moja ya walinzi ambao walikuwa wakimvutia sana Sir Alex Ferguson. Sir Alex Ferguson alishajaribu mara kadhaa kutaka kumsajili mfaransa huyu tangu mwaka 1996 lakini juhudi zake ziligonga mwamba, kupelekea kuondoka kwa Jaap Stam na kuelekea katika klabu ya Lazio, Sir Alex Ferguson alijaribu tena bahati yake kumsajili mlinzi huyo na kuweza kuipata saini yake kutoka klabu ya Internazionale ya nchini Italia mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 35.
Laurant Blanc alirithi Jezi namba 6 kutoka kwa Jaap Stam na katika miezi mitano ya kwanza alionekana kutovaa viatu vya Mholanzi huyo kwani alionekana akiboronga katika nafasi yake ya ulinzi wa kati na kupelekea klabu ya Manchester United kupoteza mechi tano mfululizo dhidi ya Bolton Wandereres, Liverpool, Arsenal, Newcastle United na Chelsea (B.L.A.N.C) huku ukizuka utani wa kuwa timu zote hizo zilizoifunga Manchester United zinaunda Jina la B.L.A.N.C
2002-2003 RIO FERDINAND
Alisajiliwa na klub ya Manchester United kutoka klabu ya Leeds United kwa ada ya pauni million 30 ikivunja rekodi ya kuwa beki aliyesajiliwa kwa kiasi kikubwa cha pesa kuliko wote na huku akikabidhiwa jezi namba 6. Ila Jezi hiyo ikionekana kama ilimpa gundu baada kufungiwa kutojihusisha na mpira kwa muda wa miezi 8 ikiwa ni mwaka mmoja na miezi miwili mara baada tu ya kukabidhiwa jezi namba 6 na kujiunga na klabu ya Manchester United. Rio Ferdinand aliukosa mchezo wa fainali wa kombe la FA, na vilevile alishindwa kuiwakilisha timu yake ya taifa ya England katika michuano ya kimataifa ya barani Ulaya.
2003-2011 WES BROWN
Ndiye mchezaji pekee mpaka sasa aliyeweza kukaa na Jezi no 6 mgongoni katika Klabu ya Manchester United katika EPL kwani ameweza kudumu nayo kwa muda wa miaka 8. Aliweza kukabidhiwa jezi namba 6 miaka 7 baadae baada ya kupandishwa katika kikosi cha kwanza akitokea katika akademia ya Manchester United ambayo alijiunga nayo akiwa na umri wa miaka 12 mwaka 1992 na hadi kufikia kupandishwa katika timu ya wakubwa ya Manchester United mwaka 1996.
Wes Brown alikuwa ni mmoja ya wachezaji walioweza kushinda mataji matatu (treble) mwaka 1999 chini ya uongozi wa Sir Alex Ferguson. Wes Brown alikuwa ni mmoja ya wachezaji waliopendwa sana na Sir Alex Ferguson aliwahi kunukuliwa akisema kuwa Wes Brown ni mmoja ya walinzi wenye asili ya Uingereza wenye vipaji vikubwa.
Kuwasili kwa Nemanja Vidic Mwaka 2006 na kuwa na kombinesheni nzuri na Rio Ferdinand katika ulinzi wa kati kukamfanya Sir Alex Ferguson kumuhamisha nafasi Wes Brown kutoka katika nafasi ya ulinzi wa kati na kwenda kucheza nafasi ya ulinzi wa pembeni huku akiwa na namba yake hiyohiyo 6 mgongoni na atakumbukwa katika kusababisha goli kwa kumpa assist Christiano Ronaldo katika mchezo wa fainal ya ligi ya Mabingwa Ulaya na kuisaidia Manchester United kushinda taji hilo mwaka 2008.
2011-2015 JONNY EVANS
Kabla ya kuanza kwa msimu wa mwaka 2011-2012 John Evans alipewa jezi namba 6 baada ya Wes Brown kuhamia klabu ya Sunderland Aug 2011 John Evans alivaa jezi yake mpya hiyo ya nambari 6 kwa mara ya kwanza katika mchezo wa kwanza wa ligi baina ya Manchester United dhidi ya West Browmich Albion ambapo aliingia dakika ya 52 kuziba pengo la mlinzi wa kati Nemanja Vidic baada ya kuumia na Mchezo huo ulimalizika Kwa Manchester United kushinda 2-1.
Baada ya miezi saba na siku 4 baada ya John Evans kupewa jezi namba 6 aliweza kufunga bao lake la kwanza katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers. Katika msimu huohuo 2011-2012 aliokabidhiwa jezi namba 6 alishindwa kuitumikia jezi namba 6 hiyo katika michezo mitatu ya mwisho wa msimu baada ya kupata majeraha ya mguu iliyompelekea kufanyiwa operation na kushindwa kufanya mazoezi ya kabla ya kuanza kwa msimu mpya (pre season) wa mwaka 2012-2013 huku kukiwa na makadirio kuwa angeweza kurejea katika mchezo wa pili dhidi ya Fulham. John Evans akiwa na jezi namba 6 aliweza kufunga bao lake la pili akiwa na jezi namba 6 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Newcastle October 7 2012 na nyota yake ya kufunga iliendelea baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Robin Van Persie na kuweza kufunga bao lake la kwanza katika UEFA Champions League katika uwanja wa Old Trafford dhidi ya Braga.
Akiwa na jezi namba 6 mgongoni aligombana na mshambuliaji wa Newcastle Papis Cisse na kupelekea kufungiwa kwa mechi sita March 7 2015. John Evans aliiacha jezi namba 6 ya klabu ya Manchester United mnamo tarehe 29 Uugust 2015 baada ya kujiunga na West Browmich Albion.
2016-2017 PAUL POGBA
Awali jezi namba 6 katika klabu ya Manchester United ilionekana kuvaliwa na Walinzi hasa walinzi wa kati. Sasa jezi hiyo itavaliwa na kiungo ghali kwa sasa Paul Pogba baada ya kusajiliwa kwa kiasi cha £89 million kutoka Juventus.
Kiungo huyo amerejea tena na ‘Mashetani Wekundu’ baada ya kuondoka klabuni hapo mwaka 2012 kuelekea Juventus. Paul Pogba alisajiliwa kwa mara ya kwanza na Manchester United kutoka Le Havre ya nchini Ufaransa akiwa na miaka 16 na kuweza kupenya moja kwa moja katika kikosi cha vijana cha Manchester United na kuweza kufunga mabao 7 katika michezo 21 katika msimu wake wa kwanza 2009-2010.
Msimu uliofuata 2010-2011 aliweza kuendelea katika akademia ya manchester united hadi November 2010 alipoitwa katika kikosi cha akiba, aliingia katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Bolton Wanderers katika ushindi wa 3-1 Feb 2011 Paul Pobga alikuwa miongoni mwa wachezaji waliopandishwa kwenda katika kikosi cha timu ya wakubwa cha Manchester United na Sir Alex Ferguson na alikabidhiwa jezi namba 42 na aliweza kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Arsenal katika mchezo wa ufunguzi na alioonyesha kiwango bora.
August 25 alifunga bao dhidi ya Swansea katika ushindi 6-0 3 July 2012 alijiunga na Juventus baada ya Sir Alex Ferguson kuthibitisha hilo na kuongezea kuwa Paul Pogba alionyesha utovu wa nidhamu kwa klabu hiyo ya jijini Manchester.
Baada ya miaka minne sasa amerejea Manchester United na kupewa jezi namba 6 yenye heshima klabuni hapo kwa sasa klabu hiyo ipo chini ya kocha Mreno Jose Mourinho na akitarajiwa Paul Pogba kufanya makubwa klabuni hapo baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano.