KINGAZI BLOG: 05/20/16

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Friday, May 20, 2016

Sakata la Escrow na IPTL Laibuka Upya Bungeni


Kambi ya upinzani imeliibua upya  bungeni sakata la Escrow, Richmond na umiliki wa kampuni ya IPTL, huku ikihoji sababu za Rais John Magufuli kutoheshimu maazimio ya Bunge ya kumwajibisha Sospeter Muhongo, badala yake kumteua tena kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Hoja hizo ziliibuliwa na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika wakati akiwasilisha maoni ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2015/16 na makadirio ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2016/17.

Muhongo alikuwa akiiongoza wizara hiyo wakati kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kuhifadhi fedha za malipo umeme kusubiri kumalizika kwa mzozo wa kimkataba baina ya kampuni ya IPTL, inayozalisha umeme  na Shirika la Umeme (Tanesco).

Bunge lilimuona Profesa Muhongo kuwa alishindwa kuwajibika na kusababisha Serikali kupoteza mapato.

Profesa Muhongo alilazimika kujiuzulu wadhifa huo saa chache kabla ya Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kutangaza baraza jipya.

Hata hivyo, Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma lilimsafisha na kashfa hiyo iliyohusisha malipo yaliyofanywa kwa mawaziri, majaji, wabunge na watumishi waandamizi wa umma.

Jana, Mnyika, ambaye ni mbunge wa Kibamba (Chadema), alirejea maazimio ya Bunge la Kumi akisema lilishafanya maamuzi kuhusiana na mikataba ambayo Serikali inaingia na kampuni mbalimbali, hasa kwenye sekta ya nishati na madini.

“Katika maazimio ya Bunge kuhusiana na fedha, ufisadi uliofanyika katika akaunti ya Tegeta Escrow na umiliki wa IPTL yanayohusu sekta ya nishati na madini, bado hayajatekelezwa kwa ukamilifu wake,” alisema Mnyika.

 Akinukuu Azimio Namba 2, Mnyika alisema liliagiza kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kununua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa Tanesco kwa lengo la kuokoa fedha inazolipa kwa kampuni hiyo binafsi.

Alisema kambi hiyo inasikitika kuona kwamba mbali ya Serikali kushindwa kununua, bado inaendelea kulipia gharama za uwekezaji na hivyo kuendelea kukiukwa kwa azimio hilo.

Akizungumzia azimio la saba linalohusu kuwajibishwa kwa mawaziri na watendaji wakuu wa wizara na bodi ya Tanesco, Mnyika alisema Profesa Muhongo naye aliwajibishwa kwa uteuzi wake kutenguliwa, lakini Rais Magufuli amemteua tena kuongoza wizara hiyo.

“Rais bila ya kujali nini Bunge lilishaazimia katika kikao ambacho na yeye alikuwa sehemu ya azimio hilo, akamteua Muhongo kuendelea kuiongoza wizara hii. Kambi ya upinzani inaliona jambo hili kama ni dharau sana kwa Bunge na ni fedheha binafsi kwake,” alisema.

Alisema kambi ya upinzani imelazimika kunukuu maazimio hayo kutokana na ukweli kwamba Serikali imeshindwa kabisa kutekeleza maazimio ya Bunge na badala yake mikataba hiyo inaendelea kutekelezwa kama ilivyoingiwa.

“Mfano mzuri ni Tanesco kuendelea kuilipa IPTL fedha za capacity charge mpaka sasa. Jambo hili linazidi kuliondolea shirika hilo la umeme uwezo wa kuwahudumia wateja wake kwa kuwa haliwezi kuwekeza zaidi katika miundombinu ya kusambaza umeme kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha,” alisema.

Diamond Platnumz Atajwa Kuwania Tuzo za BET


Mwananmuziki Diamond Platnumz ametajwa kwa mara ya pili kuwania tuzo za BET katika kipengele cha Best International Act: Africa.

Wakali wengine wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na Wizkid, Yemi, AKA na wengineo.

Tuzo hizo zitatolewa mwishoni mwa mwezi Juni nchini Marekani.

Gardner Amjibu Lady Jay Dee, Agoma kuomba Radhi


Hatimaye mtangazaji wa Clouds Fm, Gardner G. Habash amemjibu aliyekuwa mkewe, Lady Jay Dee, aliyemtaka aombe radhi ndani ya siku saba kwa kauli aliyoitoa iliyodaiwa kuwa imelenga kumdhalilisha. Katika majibu yake amekana madai hayo.

Siku chache zilizopita, Gardner alionekana katika kipande cha Video akisherehesha tukio la kumsaka mrimbwende wa chuo cha Tanzania Institute of Accountancy (TIA) jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa “yule binti sina tatizo naye, nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi…”, kisha wimbo wa ‘Ndindindi’ wa Jay Dee ukachezwa na DJ.

Kama ilivyokuwa kwa Lady Jay Dee aliyetoa siku saba za kuombwa radhi kupitia kwa mwanasheria wake Amani Tenga, Gardner amejibu kupitia mwanasheria wake Stephen Axwesso.

Katika barua yake kwa mwanasheria wa Lady Jay Dee, mwanasheria huyo wa Gardner amekiri kuwa ni kweli mteja wake alizungumza maneno hayo alipokuwa katika shughuli iliyotajwa, lakini alidai kuwa hakuna sehemu aliyomtaja mkewe huyo wa zamani.

Alisema kuwa madai ya upande wa Lady Jay Dee hayana mashiko na alimshauri mwanasheria huyo kupitia upya sheria inayozungumzia wanandoa waliotalakiana ili aweze kumshauri vizuri mteja wake kuhusu suala hilo.

Nakala ya barua hiyo pia imetumwa Clouds Media Group na kwa Rais wa Wanafunzi wa Chuo cha TIA.




magazeti ya Tanzania leo Ijumaa tar 20 Mei

Naanza kwa kukuletea Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya May 20.usiache kukaa karibu nasi kwenye mitandao ya kijamii yaani facebook na twitter@Tanzaniampyasasa




Jide kumuanika mrithi wa Gardner Leo!



Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee au Jide’

Exclusive! Lejendari wa Bongo Fleva kwa zaidi ya miaka kumi na tano, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee au Jide’, anatarajia kumuanika mrithi wa aliyekuwa mumewe, Mtangazaji wa Kituo cha Radio CloudsFM, Gardner G. Habash ndani ya saa 24, Ijumaa lina data kamili.

HABARI ZA KUAMINIKA

Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizothibitishwa na uongozi wa staa huyo, Jide atamtambulisha mchumba wake huyo kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa Mlimani City leo, Dar ambapo pia atafanya shoo ya saa tatu mfululizo, inayokwenda kwa jina la Naamka Tena.

“Itakuwa ‘sapraizi’ kwa mashabiki wote wa Jide ambapo sapraizi hii itaendana na shoo ya kihistoria ya Naamka Tena atakayoipiga kwa saa tatu akiwa na bendi yake (Lady Jaydee and The Band),” alisema mmoja wa viongozi wanaomsimamia ambaye hakutaka kutajwa gazetini.


Jide na Gardner

JIDE ALIPOTOKEA

Jide alifunga ndoa na Gardner Mei 14, 2005 ambapo waliishi na kufanikiwa kuwa na mali mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba, Ukumbi wa Nyumbani Lounge na Bendi ya Machozi.

FIGISUGISU NA GARDNER

Mvutano wa wawili hao ulidaiwa kuanzia kwa Jide aliyeamua kuomba talaka kwa kile kilichosemekana kuwa Gardner alipata kazi ya kutangaza redio moja nchini Kenya hivyo kama angeenda huko wakati ni meneja wake, angeshindwa kuwa naye huku pia figisufigisu nyingine nyingi zikijitokeza kama kubadilisha jina la Ukumbi wa Nyumbani Lounge na kuwa M.O.G na mambo mengine ikiwepo kusalitiana na kupigana.

WAFIKISHANA MAHAKAMANI

Baada ya mvutano wa muda mrefu, wawili hao walifikia hatua ya kufikishana katika Mahakama ya Mwanzo ya Manzese jijini Dar, miezi michache iliyopita na mahakama kuamua kuvunja rasmi ndoa yao ya Kikristo na kila mmoja kupewa hati yake ya talaka.

Source. global publishers

 

Gallery

Popular Posts

About Us