Watu watatu wameuawa kwa nyakati tofauti mkoani Tabora akiwemo Askali wa Jeshi la wananchi wa Tanzania,(JWTZ)aliyepigwa fimbo na wafugaji akiwa katika ujenzi wa nyumba yake,baada ya kuwalalamikia kuwa, ng’ombe wamevamia katika kiwanja chake na na kuharibu vitu mbalimbali vya ujenzi.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Tabora Kamanda wa polisi mkoani humo ACP Hamis Issa Suleiman,amemtaja marehemu kwa jina la Carritus Mkunozi (35) wa kikosi cha 212KJ,ambapo ugomvi ulitokea baada ya kupishana kauli na wafugaji,na ugomvi kuanza,ambapo alifariki akiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete muda mfupi,akipata matibabu.
Aidha amesema kuwa katika tukio hilo kundi kubwa la ng’ombe zaidi ya mia mbili,waliokutwa katika kiwanja cha marehemu huyo wanashikiliwa, na muuaji mmoja,huku akiwataja marehemu wengine,waliouawa kuwa ni mama mmoja,mganga wa kienyeji aliyepigwa fimbo kichwani baada ya kuwapa kisogo wauaji waliokuwa wamemwomba maji ya kunywa.
Katika hatua nyingine Kamanda Hamisi Issa Suleiman amesema huko kata ya kijiji cha Motomoto Vumilia wilayani Urambo kijana mmoja kibarua ambaye hakufahamika alipigwa ngumi kifuani na kufariki papo hapo, wakati wakigombea mgao wa posho ya kazi yao.