Sunday, October 16, 2016
CHOMBEZO: ILAMBE HUMOHUMO sehemu ya -1
Sh 330 milioni kusaidia upasuaji wa moyo kwa watoto nchini
Dar es Salaam. Jumla ya Sh303 milioni zimekabidhiwa kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili kukamilisha matibabu ya upasuaji kwa watoto 138 wanaosubiri huduma hiyo kwa sasa.
Fedha hizo zimewasilishwa leo na taasisi tatu tofauti ikiwemo ya Baps Charities iliyotoa Sh222 milioni, Youth Welfare Trust Sh48,400,000 milioni na I & M Bank iliyotoa Sh33 milioni.
Akizungumzia mara baada ya kupokea msaada huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohammed Janabi alisema fedha hizo zitawezesha upasuaji kwa watoto 138 ambao walitakiwa kufanyiwa upasuaji mwakani.
"Upasuaji tunafanya kwa foleni, wapo waliopangiwa mwakani lakini baada ya msaada huu tuna imani kwamba ifikapo Desemba mwaka huu tayari watoto 138 watakuwa wamefanyiwa upasuaji," alisema.
Waasi 'waiteka' ngome muhimu ya IS Syria
Waasi wanaoungwa mkono na serikali ya Uturuki nchini Syria wameuteka mji muhimu wa Dabiq kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State,kulingana na makamanda wa waasi hao na wachunguzi.
Waasi hao waliuteka mji wa Dabiq baada ya wanachama wa kundi la Islamic State kuuondoka kulingana na kundi la haki za kibinaadamu lililo na makao yake huko Uingereza.
Mji huo mdogo wa Kaskazini una thamani kubwa kwa IS kwa sababu umekuwa ukitajwa katika ubashiri mwingi wa vita vya kundi hilo pamoja na propaganda zake.
Utekaji wa mji huo ni miongoni mwa vita vikali vilivyoanzishwa na makundi ya waasi nchini Syria dhidi ya kundi hilo.
Diamond, Harmonize na DJ D-Ommy washinda tuzo za Afrimma 2016
Diamond Platnumz, Harmonize na DJ D-Ommy, wameibuka washindi kwenye tuzo za Afrimma 2016, zilizofanyika Dallas, nchini Marekani Jumamosi hii.
Diamond ameibuka tuzo ya Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki, Harmonize Msanii bora chipukizi na D- Ommy, DJ bora wa Afrika.
“Team Tanzania Mungu ni mwema siku zote,” ameandika Harmonize baada ya ushindi huo.
Harmonize akiwa na Akothee aliyeshinda tuzo ya msanii bora wa kike Afrika Mashariki na Willy M Tuva
Diamond na D-Ommy hawakuwepo kwenye tuzo hizo.
Mwana Samatta Atajwa Tuzo ya Mchezaji Bora ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya GENK ya nchini Ubelgiji ametajwa miongoni mwa wachezaji 30 wanaowani Tuzo ya Mchezaji Bora ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).
Wachezaji wengine ni pamoja na Mkenya Victor Wanyama anayecheza ligi kuu ya Uingereza katika klabu ya Tottenham Hotspur, Denis Onyango kutoka Uganda anayekipiga katika klabu ya Mamelodi Sundowns.
Hapa chini ni orodha kamili.
1. Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)
2. El Arabi Hillel Soudani (Algeria & Dinamo Zagreb)
3. Islam Slimani (Algeria & Leicester City)
4. Samuel Eto’o (Cameroon & Antalyaspor)
5. Benjamin Mounkandjo (Cameroon & Lorient)
6. Serge Aurier (Cote d’Ivoire & PSG)
7. Eric Bailly (Cote d’Ivoire & Manchester City)
8. Yao Kouasi Gervais ‘Gervinho’ (Cote d’Ivoire & Hebei Fortune)
9. Mohamed Salah (Egypt & Roma)
10. Mohamed El Neny (Egypt & Arsenal)
11. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Dortmund)
12. Andre Ayew (Ghana & West Ham)
13. Victor Wanyama (Kenya & Tottenham)
14. William Jebor (Liberia & Wydad Athletic Club)
15. Mehdi Benatia (Morocco & Juventus)
16. Hakim Ziyech (Morocco & Ajax)
17. John Mikel Obi (Nigeria & Chelsea)
18. Kelechi Iheanacho (Nigeria & Manchester City)
19. Ahmed Musa (Nigeria & Leicester City)
20. Cedric Bakambu (DR Congo & Villareal)
21. Yannick Bolasie (DR Congo & Everton)
22. Sadio Mane (Senegal & Liverpool)
23. Kalidou Koulibaly (Senegal & Napoli)
24. Keegan Dolly (South Africa & Mamelodi Sundowns)
25. Itumeleng Khune (South Africa & Kaizer Chiefs)
26. Mbwana Samatta (Tanzania & Genk)
27. Aymen Abdennour Tunisia & Valencia)
28. Wahbi Khazri (Tunisia & Sunderland)
29. Dennis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)
30. Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns)
Mamelodi Sundowns yajiweka pazuri kutwaa klabu bingwa Afrika
Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imejiweka kwenye nafasi nzuri kuelekea mchezo mchezo wa marudiano wa fainali ya klabu bingwa Afrika Jumamosi ijayo baada ya kuifunga Zamalek 3-0 kwenye mechi ya kwanza mjini Pretoria.
Licha ya ushindi huo mnono ilioupata Sundowns, tangu mwaka 2010 ambapo TP Mazembe iliifunga Esperance ya Tunisia 5-0, bado hakuna klabu ambayo imeweza kufanya hivyo kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya fainali.
Anthony Laffor na Tebogo Langerman walifunga magoli mawili ya kuongoza kipindi cha kwanza huku bao la tatu likifungwa kipindi cha pili.
Ushindi huo unaifanya Sundowns kupewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa marudiano mjini Alexandria ambako watakuwa wakisaka taji lao la kwanza barani Afrika na kuwa timu ya pili kutoka Afrika Kusini kushinda taji hilo kubwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.
Wakitazamwa na watazamaji 40,000 Sundowns walikuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwa kuichezesha Zamalek katika mchana wa jua kali.
Endapo Sundowns watatwaa taji mwishoni mwa juma lijalo, wataandika historia mpya kwenye ardhi ya Afrika Kusini kwa ngazi ya vilabu. Walitupwa nje mapema wakati wa hatua za kufuzu dhidi ya AS Vita Club lakini walirejeshwa tena mashindanoni baada ya Vita Club kupokwa nafasi hiyo kufatia kumchezesha mchezaji asiye na vigezo.
Mchezo wa marudiano utapigwa Alexandria Jumapili October 23.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza amezindua meli kubwa ya kisasa yenye uwezo wa kubeba abiria 500
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela amezindua rasmi huduma ya usafiri wa meli kati ya Mwanza na mji wa Nansio wilayani Ukerewe katika ziwa Victoria, ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 500 magari madogo 40 na tani 284 za mizigo, hatua itakayosaidia kutatua changamoto ya huduma za usafiri wa abiria kwa wakazi wa kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
Meli hiyo MV. Nyehunge II, imejengwa na kampuni ya Songoro Marine Transport kwa gharama ya shilingi milioni 800 na kufanyiwa ukaguzi na maofisa wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMTRA), makao makuu Dar es Slaam.
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Ukerewe, akiwemo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo George Nyamaha wanaeleza changamoto za usafiri zilizokuwa zinawakabili awali.
Meli zinazotoa huduma ya usafiri ndani ya ziwa Victoria kati ya Mwanza na Ukerewe, ni mv. Butiama inayomilikiwa na kampuni ya huduma za meli Tanzania pamoja na meli ya MV. Nyehunge.
Madereva wa vigogo walia na agizo la Rais Magufuli kurejesha fedha za Mwenge
Madereva na Wasaidizi wa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya mbalimbali nchini ambao walikuwa tayari wamefika Mkoani Simiyu kushiriki sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wameeleza kuumizwa na agizo la kurejesha fedha za kujikimu ambazo kiasi walizitumia kwa shughuli husika.
Walisema kuwa agizo hilo la Rais John Magufuli kwao limewatengenezea tatizo lingine la kiuchumi kwani liliwafikia kwa kuchelewa.
Baadhi yao wamesema kuwa wao hawana uwezo wa kurejesha fedha hizo kwani hawakuomba kufanya safari hizo bali ilikuwa sehemu ya kazi zao na kiasi cha fedha hizo walizitumia kama walivyokubaliwa na ofisi kuwawezesha kufika na kuishi katika eneo hilo.
”Sisi hatukuomba kuja Bariadi kwenye sherehe za Mbio za Mwenge wa Uhuru. Tuliambiwa kuja na tukapewa fedha ambazo tumezitumia kwa mujibu wa mahesabu ya matumizi tuliyoandikiwa kwa sababu ilibidi tule na kulala kwenye nyumba za wageni. Hapo sisi kosa letu liko wapi?” Alihoji mmoja kati ya madereva aliozungumza na gazeti la The Citizen.
Alisema kuwa anadhani uamuzi wa wao kurejesha fedha zote ambazo tayari wamezitumia hautawatendea haki kutokana na matumizi husika waliyofanya.
Naye msaidizi wa Mkuu wa Mkoa mmoja ambaye hakutaka kutajwa, alisema kuwa yeye hataweza kurejesha fedha hizo kwa sababu baada ya kufika Bariadi alilazimika kulipia chumba siku 7 alizopaswa kukaa hapo kutokana na upungufu wa vyumba.
”Ilinibidi nimlipe mwenye chumba gharama zote za siku 7 ambazo nilitarajiwa kuishi hapa kama nilivyotumwa kwa sababu ya uhaba wa vyumba hapa. Sasa naanzaje kumwambia mwenye anirudishie pesa yangu yote ili nirejeshe ofisini?” Alihoji.
Hata hivyo, wakati wasaidizi wa vigogo hao wakionesha kuchanganyikiwa na agizo hilo ambalo wanaamini sasa linaweza kuwaingiza hasara ambayo imetokana na kutumwa wafanye wajibu wao, baadhi ya wakuu wa mikoa tayari wameshaanza kurejesha fedha hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ni mmoja kati ya wakuu hao wa mikoa walioweka wazi mbele ya waandishi wa habari kusitisha safari hiyo na kurejesha kiasi cha fedha walizopangiwa kwa shughuli hiyo.
Rais John Magufuli aliagiza viongozi wote pamoja na wasaidizi wao waliokuwa wamepanga kuhudhuria sherehe za kuzimwa kwa mbio za Mwenge mkoani Simiyu wasitishe safari zao na waliokwishachukua posho wazirejeshe.
Unene husababisha muda mfupi wa kuishi
Uzito ni sawa na uvutaji wa sigara ambao huleta matatizo makubwa kwa watu ambao wamo katika kilinge hicho.
Wataalam wa afya na urembo wanasema wazi kuwa mnene kunapunguza sit u namna ya kujiweka sawa katika masuala mbalimbali ya kijamii lakini pia unakuwa na muda mfupi sana wa kuishi duniani.
Wataalam wanasema kwamba kuwa mzito kunapunguza maisha yakokwa miaka mitatu anasema mtafiti Gary Whitlock kutoka Clinical Trial Service Unit ya Chuo Kikuu cha Oxford kilichopo
Uzito huo ni ule unaokuwa mara tatu ya uzito ambao mtu anatakiwa awe nao kutokana na urefu wake, umri na afya yake.
Ndio kusema kama mtu anakuwa na uzito mathalani paundi 150 mtu huyo anapunguza umri wake wa kuishi duniani kwa miaka 10.
Pia uzito wa kuchusha umekuwa ukileta tatizo la figo, ini na aina kadhaa za kansa na pia huleta matatizo ya magonjwa ya moyo na kiharusi.
Unene huleta mchosho mkubwa kwa moyo na huleta mizania dhaifu ya rehemu na kusababisha shida katika mwenendo wa damu.
Wakati wanaume wenye kiuno kikubwa huongeza hatihati ya kifo wakati wanawake wenye mzunguko mkubwa huongeza hatihati ya kifo kwa asilimia 78