Staa wa Bongo fleva Rajab Abdulhan ‘Harmonize’.
Siri nje! Staa kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) anayejipenyeza kwa kasi kwenye Bongo Fleva, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ amekiri kuwa shemeji yake kwa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz;, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’,ndiye aliyemuunganisha na demu mkali kutoka Nairobi nchini Kenya, Huddah Monroe ‘The Boss Chick’.
“Katika maisha yangu nilikuwa namuona tu Huddah na kumtamani ila namshukuru shemeji yangu Zari aliyenikutanisha na Huddah na kutuunganisha kuwa marafiki ambao tumekuwa tukiwasiliana utadhani tulifahamiana zaidi ya miaka hata mitano huko nyuma,” alisema Harmonize akihojiwa nablog hii.