Chama
 cha mapinduzi CCM kimemteua Mbunge wa Zamani wa SIMANJIRO mkoani 
Manyara, CHRISTOPHER OLE SENDEKA kuwa msemaji wa chama hicho
Katibu
 Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtangaza Mjumbe wa Halmashauri Kuu 
ya Taifa ya CCM, Christopher Ole Sendeka kuwa Msemaji Rasmi wa CCM leo, 
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam 
Akitangaza hatua hiyo katika mkutano na waandishi wa habari 
jijini DSM katibu mkuu wa CCM ABDULRAHMAN KINANA amesema uteuzi wa OLE 
SENDEKA kwa msemaji wa chama hicho, ni hatua ya kupunguza majukumu ya 
kiutendaji kwa aliyekuwa msemaji wa chama hicho NAPE NNAUYE aliyeteuliwa
 kuwa waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo.Kanana amesema hatua hiyo itatoa fursa kwa watendaji hao kutimiza majukumu yao kwa ufanisi zaidi katika kuwatumikia wananchi.
Akizungumza mara baada ya uteuzi huo,msemaji huyo wa CCM CHRISTOPHER OLE SENDEKA ametoa wito kwa wanasiasa nchini kuacha siasa za kuponda jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kutimiza majukumu yake, ambapo amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi.