Hatimaye
 Wananchi wa Zanzibar hii leo wamejitokeza kwa wingi  kupiga kura katika
 uchaguzi wa marudio uliofanyika Kisiwani Unguja na Pemba
Rais
 wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  ambae ni mgombea wa 
Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein
 akipiga kura katika uchaguzi wa marudio  kituo namba 1 cha kupiga kura 
Skuli ya msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo
Hatimaye Wananchi wa Zanzibar hii leo wamejitokeza kwa 
wingi  kupiga kura katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Kisiwani 
Unguja na Pemba kutokana na agizo la tume ya Uchaguzi Zanzibar.Akipiga kura yake katika kituo namba moja katika shule ya msingi ya Bungi mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM DKT ALI MOHAMMED SHEIN amesema, hatua hii ni muhimu katika kukuza demokrasia ambapo kila mwananchi wa Zanzibar anapaswa kupiga kura kuchagua kiongozi anayemtaka.
Huko pemba wananchi wamejitokeza kupiga kura kwa wingi ambapo mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC HAMAD RASHID MOHAMED amepiga kura huko Wawi PEMBA.