Simba yaahidi kichapo Tanga | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Friday, March 18, 2016

Simba yaahidi kichapo Tanga



KOCHA Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja amesema wanakwenda Tanga kushinda katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union utakaochezwa mwishoni mwa wiki.

Kuelekea kwenye mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, klabu hiyo imeandaa mabasi maalumu kwa ajili ya mashabiki kujitokeza kwa wingi kushangilia pointi tatu ambazo wana uhakika wa kuzipata.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mayanja alisema mechi hiyo ina umuhimu mkubwa kushinda na wamejipanga kushambulia na kushinda na si kwenda kuzuia. “Tunakwenda kucheza mpira wa kisasa, kama mnavyojua mpira wa sasa si kuzuia bali kushambulia na kushinda.
Hatutaki kuwa na sifa ya kushinda nyumbani tu, awamu hii ni kipigo cha nje na ndani,” alisema. Alisema wachezaji wake wote wanaendelea vizuri tayari kwa mchezo huo, ambapo hata kwa waliokuwa majeruhi kama Haji Ugando, Raphael Kiongera, Mohamed Fakii na Peter Manyika Jr, wanaendelea na mazoezi mepesi.
Wakati Simba akiwahakikishia mashabiki wa timu yao ushindi, jana kulikuwa na kikao cha wenyeviti wa matawi Dar es Salaam kujipanga namna ya kushinda mchezo huo, lakini pia kwenda kwa wingi kushuhudia ushindi huo.
Mwenyekiti wa matawi ya wanachama ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Idd Kajuna alisema timu yao imedhamiria kuchukua ubingwa, hivyo inatambua umuhimu wa mechi hiyo.
Alisema mashabiki wa Dar es Salaam wanaotaka kwenda kuishangilia timu yao Tanga, wajiorodheshe kwenye matawi yao kwa ajili ya kuondoka pamoja katika mabasi yatakayoandaliwa na klabu hiyo kwa gharama ya Sh 25,000 kwenda na kurudi.
“Tunakwenda kuchukua ushindi ili kuwafunga midomo wa matopeni ndo maana tunahimiza mashabiki wengi popote walipo waje kwa wingi kuishangilia timu ikishinda na tena tuvae jezi zetu mpya,” alisema. Timu hiyo imedhamiria kuchukua ubingwa msimu huu na imejipanga kushinda mechi za ugenini na nyumbani. Inaongoza kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 54

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us