Katika uhakiki wa awali Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo haikuwahakiki watumishi 159 kutokana na kuwa masomoni. Halmashauri hiyo imekamilisha uhakiki huo ambapo imebainika watumishi wawili (2) ni watumishi hewa.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Ili kuhakikisha Mkoa unaondokana kabisa na tatizo la watumishi hewa, niliwaelekeza Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri kufanya zoezi hilo awamu ya pili.
Nimepokea taarifa kutoka kwa Wakuu wa Wilaya inayoonesha kuwapo kwa watumishi hewa kumi na mbili (12) hadi kufikia tarehe 18/04/2016. Watumishi hao wameisababishia Serikali hasara ya shilingi 155,205,681/=
Watumishi hao wapo katika mchanganuo ufuatao:
Uhakiki uliofanywa na Mkuu wa Wilaya katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa umebainisha kuwapo kwa watumishi tisa (9) ambao ni watoro na mtumishi mmoja ambaye aliomba likizo bila malipo na kwenda kufundisha mahala pengine lakini akaendelea kulipwa mpaka kufikisha kiasi cha Tsh. 25, 831,000/= lakini baada ya kufanya ufuatiliaji amerejesha kiasi cha Tsh. 18,604,679/= Mtumishu huyu ni mwalimu anaitwa Dinner J. Kissamo alikuwa mwalimu Manispaa ya Iringa.
Aidha, Uhakiki pia ulibaini mwalimu mmoja (Ifunda) alikuwa na Check 2 na zote alikuwa analipwa na halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika.
Mtumishi Mwingine ni Khalid M. Meza Afisa kilimo Kilolo ni mtoro wa muda mrefu mkurugenzi tayari ameshamfungulia mashtaka. Hii ni mifano tu ya watumishi hewa.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Ili kuendelea kujiridhisha na kuondolewa kabisa watumishi hewa katika Mkoa wa Iringa, nimechukua hatua zifuatazo;
1. Nimewaagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha kuwa, zoezi la uhakiki watumishi linakuwa endelevu na hatua zinachukuliwa ili kuwaondoa watumishi hewa wote