
Tamko
 hilo limetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. 
Servacius Likwelile kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari 
iliyotolewa hivi karibuni Jijini Dar es salaam.
Taarifa
 hiyo imefafanua kuwa Washirika wa Maendeleo bado wanaendelea kuisadia 
Serikali katika bajeti yake na kwamba tuhuma za kujitoa kwa makundi 14 
ya kuisaidia bajeti ya Tanzania sio za kweli.
Taarifa
 hiyo imesisitiza kuwa bado makundi hayo yanaendelea kuisaidia bajeti ya
 Tanzania ambapo kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Washirika wa Maendeleo 
nane waliahidi kuendelea kusaidia Bajeti Kuu wakiwemo Benki ya Maendeleo
 ya Afrika, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ireland, Sweden, 
na Benki ya Dunia.
Kwa
 mwaka wa fedha 2016/2017 baadhi ya Washirika wa Maendeleo 
wameshathibitisha kusaidia bajeti kuu ya Serikali, Washirika hao ni 
pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika, Denmark, Umoja wa Ulaya pamoja 
na  Benki ya Dunia.
Washirika wengine wa Maendeleo wataendelea kuisaidia Serikali kupitia wa Mfuko wa Pamoja wa Maendeleo na Miradi.
Washirika
 hao ni pamoja na Ubelgiji, Canada, China, Denmark, Finland, Ufaransa, 
Ujerumani, Hispania, India, Italia, Japan, Korea ya Kusini, Norway, 
Sweden, Uholanzi, Uingereza,  Marekani na Uswisi.
Washirika
 wengine wa maendeleo ambao wanaisaidia bajeti ya Serikali ni Benki ya 
Maendeleo ya Afrika, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, BADEA, Mfuko wa OPEC
 pamoja na Saudia Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia.
Taarifa
 hiyo ya Dkt. Likwelile imeongeza kuwa, Serikali ya pamoja na washirika 
wa maendeleo wanaoisaidia Tanzania wako katika mazungumzo juu ya namna 
ya kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na nchi hizo.
Serikali
 imewashukuru Washirika wa Maendeleo kwa kuendelea kuisaidia Tanzania 
katika kupelekea juhudi za kimaendeleo zenye tija kwa wananchi.