Wenyewe wanasema ‘sasa imetosha.’ Hii ni taarifa kutoka kwa Tanzania Bloggers Network:
Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini ‘Tanzania 
Bloggers Network’ – TBN inawaomba wanachama wake wote kutotumia taarifa 
ama habari au picha yoyote kutoka katika mkutano wa maadhimisho ya Uhuru
 wa Vyombo vya Habari (WPFD) unaofanyika kitaifa mkoani Mwanza. 
Kamati Kuu ya Uongozi TBN imefikia hatua hiyo leo baada ya 
kujadiliana na kujiridhisha kuwa kumekuwepo na taasisi za tasnia ya 
habari ambazo zimekuwa zikiwatenga wanahabari wa mitandao ya kijamii 
(bloggers) na kutotambua umuhimu wao wakati sehemu kubwa ya taarifa 
mbalimbali nchini husambazwa na mitandao hiyo.
TBN iliyosajiliwa rasmi serikalini Aprili 2015 na kupewa namba ya 
usajili; S. A 20008 inawataka wanachama wake kutotoa ushirikiano wa sina
 yoyote kwa taasisi ambazo zinawatenga bloggers. 
Tunasikitika kufikia hatua hii ila hamna jinsi. TBN itasikitika na 
kumshangaa mwanachama wake au blogger asiye mwanachama kutounga mkono 
agizo hili, na kwenda kinyume na agizo hili. Muda umefika ‘Bloggers’ 
kudai heshima, kutambulika na kuthaminika kama tasnia ya habari ingine 
yoyote.
SOURCE; BONGO 5
Tuesday, May 03, 2016
Mabloga Tanzania waungana kupinga taasisi za habari ‘zinazowachukulia poa’
Published Under
IMPORTANT NEWS
About Author
BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi