Habari kutoka kwa ndani ya familia zinasema KINYAMBE amefariki Dunia baada ya kuugua kwa siku kadhaa japo taarifa zaidi zitaendelea kutolewa juu ya undani wa kifo cha staa huyo wa vichekesho nchini.
Kinyambe ataendelea kukumbukwa kutokana na jitihada mbalimbali alizozifanya katika tasnia ya filamu za vichekesho hasa kwa staili na sauti yake ya uchekeshaji wa aina yake.MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMINA.
(R.I.P.KINYAMBE)