Baadhi ya wabunge wa chama tawala wamepongeza uamuzi wa bunge wa kuwasimamisha wabunge 7 wa upinzani kwa kutofuata sheria za bunge kwa kutaka kushinikiza kujadiliwa kwa hoja ambayo ilikuwa imeshatolewa maamuzi kuhusu bunge kurushwa live.
Baadhi ya wabunge hao ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambaye ameupongeza uamuzi wa Bunge na kusema kwamba ni lazima ifike sehemu adhabu itawale bungeni. Wabunge 7 waliosimamishwa wamepewa kitu wanachostahili kwa kuvunja kanuni.
Mbunge wa Geita vijijini Joseph Kasheku Msukuma amesema kwamba adhabu hiyo ni sawa kwa wabunge hao ili iwe fundisho kwa wabunge wapya.
Kwa upande wake Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga amesema kwamba kusimamishwa huko kutajenga heshima ya Bunge na kuwa fundisho kwa wengine.
Aidha Wabunge waliosimamishwa ni Tundu Lissu na Ester Bulaya vikao vya mkutano wa tatu na wanne, Godbless Lema, Zitto Kabwe, Paulin Gekul, na Halima Mdee vikao vyote vya mkutano wa tatu na John Heche vikao 10 vya mkutano unaoendelea sasa.
Udaku specialblog