vitatu wilayani Babati mkoani Manyara wakiwa na silaha za jadi mishale na mikuki wanalazimika kulala nje ya maboma yao wakipinga uamuzi wa serikali wa kutaka kubomoa maboma 11 kati ya 25 yaliyopo katika eneo la Maramboi linalopakana na mwekezaji raia wa Ufaransa kwa madai kwamba kumekuwepo na ongezeko la wafugaji ambao si wakazi wa kijiji hicho na wamekuwa wakiingiza mifugo yao katika eneo la mwekezaji huyo.
Kauli hiyo ya kupinga agizo la kutakiwa kuondoka ama kubomoa maboma yao wameitoa baada ya watendaji wa kijiji,kata na tarafa wakiwa na timu maalum iliyoandaliwa chini ya usimamizi wa polisi kufika katika eneo hilo la kijiji ili kuwashawishi kuondoka kabla ya kubomoa kwa nguvu na kwenda eneo walilopangiwa huku wakidai hawawezi kuondoka katika eneo hilo kwa kuwa agizo hilo linapingana na amri ya Mahakama ya Rufaa ya 2013 iliyowataka kuendelea kubaki hapo aidha pia wakipinga kuwepo kwa ongezeko la wageni.
Nae Katibu wa chama cha wafugaji nchini kata ya Nkaiti Bw Juma Kwanjay amesema chama hicho kinapingana na operesheni hiyo yenye muonekano wa ushawishi ngazi ya kata kwa mujibu wa barua kwenda kwa mkuu wa wilaya hiyo badala ya kijiji,huku akidai kama lengo ni kubomoa maboma 11 na kuacha maboma 17 yaliyoamriwa na mahakama yatabaki maboma 14 kinyume na amri ya mahakama na kuchochea mgogoro huo uliokuwa umetulia.
Hata hivyo kiongozi wa oparesheni hiyo na Afisa Tarafa ya Mbugwe bw faustine Sedoyeka amesema operesheni hiyo ni utekelezaji wa agizo la mkuu wa wilaya la kuwasimamia kubomoa maboma yao na kuwapeleka eneo maalum lililotengwa lakini wamelazimika kusitisha operesheni hiyo kutokana na mazingira hayo kutokuwa rafiki kwao hasa kutokana na wafugaji hao kujificha vichakani kama mtego dhidi yao.