BASATA WATOA TAMKO KALI KWA MASTAA WALIOTOA BEI ZA KUJIUZA   | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, July 17, 2016

BASATA WATOA TAMKO KALI KWA MASTAA WALIOTOA BEI ZA KUJIUZA  


DAR ES SALAAM: Wakati serikali ikitangaza vita dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara ya ngono, ripoti mpya iliyokusanywa inaonesha viwango vya fedha vinavyolipwa na wahitaji ili kuweza kupata huduma hiyo kutoka kwa mastaa wa fani mbalimbali nchini.

Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba mastaa hao wa Bongo Fleva na filamu ambao wamekuwa wakijiuza kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, Instagram na mingine, ambako huweka picha zao zinazoonesha pozi mbalimbali, wanaweka bayana jinsi walivyo tayari kushiriki tendo na mwanaume wasiyemfahamu, ilimradi mifuko yao imetuna.

“Unajua kutokana na maisha magumu, mastaa wetu wanajilipua kabisa, wanataja waziwazi kiasi wanachotaka wapewe, sema ndiyo wengine wanachukua mkwanja mrefu na wengine hela mbuzi tu, sanaa hailipi ndiyo maana wapo tayari kujiachia,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilidokeza majina kadhaa ya mastaa hao walio tayari kujitoa kwa yeyote mwenye fedha za kutosha ambazo zitamhakikishia maisha bora, ingawa baadhi ya mastaa waliotajwa, waliruka kimanga kujihusisha na mchezo huo unaokiuka maadili ya Kitanzania.

GIFT STANFORD ‘GIGY MONEY’

Video Queen huyu aliyeuza sura kwenye video mbalimbali za wanamuziki wa Bongo Fleva, alisema hali ya maisha inamlazimu kuwa tayari kukabiliana na mazingira yoyote ili mradi mambo yake yanaenda ‘supa’ hivyo hana kinyongo kama mwanaume yeyote,  awe ni wa kwenye mitandao au barabarani, atakayempatia kiasi cha shilingi milioni tatu.

GLASNOST KALINGA ‘GILLA’

Chipukizi huyo anayefanya vizuri kwa sasa katika filamu, naye alijianika wazi kuwa yupo tayari kuangukia mikononi mwa mtu kwa kiasi cha shilingi milioni mbili unusu hadi tano, kwani kama suala ni kupatwa na magonjwa, binadamu wote ni lazima watakufa.



ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’

Staa huyu wa filamu Bongo alisema hawezi kujiuza kwa njia yoyote ile kwani kitendo chake cha kuweka picha zake za aina mbalimbali katika mitandao ni kwa ajili ya kujifurahisha na pia mashabiki wake.

“Huwa napigiwa simu sana, unakuta nyingine napokea nikisikia mtu anachoongea ni ujinga namkatia na sipokei tena hata akiendelea kupiga.”

 ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’

FATUMA AYUBU ‘BOZI’

Bozi naye alisema; “Kama jamaa akija na shilingi milioni kumi niko tayari lakini hata hivyo itategemea na afya ya huyo mtu maana siko tayari kufa kwa milioni kumi.”

TIKO HASSAN

“Sijawahi kufikiria kujiuza wala kujaribu, lakini kama kuna wanaojiuza na kuona ina masilahi, basi waendelee ila ina madhara makubwa sana katika maisha yao, kwani kama wamekutana kwenye mitandao ya kijamii wanaenda kuwa na mtu wasiyemfahamu vizuri au hata kama ni barabarani mmekutana bado ni hatari pia.”

ESTER KIAMA

“Kiukweli sijawahi kujiuza na sina mpango kwa sababu nina mwanaume wangu anayeniridhisha kwa kila kitu, mimi sitaki fedha, ila nataka mapenzi na tayari mlango huo nishaufunga hata aje nani na fedha zake siwezi kujiuza.”

Ester Kiama akiwa katika pozi.

ISABELA MPANDA

“Sijawahi kujiuza na nimekuwa nikiweka picha za kuacha mwili wangu wazi kwenye mitandao kwa sababu kazi yangu inaruhusu, wapo wanaume wanaingia kingi na kunitafuta, lakini nimekuwa nikiwachuna tu, hawajawahi kufanikiwa kuwa nami kimapenzi.

“Kwa siku huwa nawachuna hata watu sita, wakishatuma fedha zao nawa-block na wale ninaowabakiza wananimwagia mitusi tu, lakini ndiyo hivyo nakuwa nimeshakula fedha zao tayari.”

MWAKIFWAMBA ANASEMAJE?

Paparazi wetu alimtafuta Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba na kumwelezea hali hiyo ambapo alisema hakuwahi kujua kama wapo baadhi ya wasanii wanaojiuza na kuanika wazi kiasi cha malipo wanayotoza.

Kutokana na sababu hiyo, alisema shirikisho lake litayafanyia kazi maelezo hayo na litakapojiridhisha, hatua muafaka zitachululiwa.

“Ngoja nitalifanyia kazi, maana siwezi kutoa maamuzi peke yangu, nitakaa na bodi na kujiridhisha kwamba ni kweli hapo ndipo tutajua la kufanya.”

SERIKALI YAJIPANGA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa ‘Basata’, Godfrey Mngereza alipotafutwa ili kuzungumzia suala hilo, alisema aachiwe muda ili akishajiridhisha ndipo atakapolifanyia kazi.

“Siwezi kuzungumza kitu ambacho sijakiona au ambacho sina ushahidi nacho, naomba muda nikishajiridhisha ndipo nitakapotoa ufafanuzi,” alisema Mngereza.

KUTOKA MEZANI KWA MHARIRI

Ni kweli kwamba hali ya maisha ni ngumu, lakini ni jambo la hatari kwa mtu kuishi kwa kutegemea kuuza mwili wake, kwani licha ya hatari ya kiafya, pia jambo hilo ni kinyume na maadili ya Kitanzania.

Maisha mazuri yanaweza kupatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na ubunifu. Tunaishauri serikali kupitia vyombo vyake, kutoa adhabu kali kwa yeyote atakayepatikana akiufanya biashara mwili wake.

IMEANDIKWA NA: Gabriel Ng’osha, Mayasa Mariwata na Gladness Mallya - GPL

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us