Maafisa wanne wa polisi mjini Dallas nchini Marekani wamepigwa risasi na kuuawa huku wengine saba wakijeruhiwa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi.
Maafisa wa polisi katika mji ulio katika Jimbo la Texas, wanasema mauaji hayo yametekelezwa na washambuliaji wawili wa kulenga shabaha (snipers).
Msako mkali unaendelea kuwasaka washambuliaji hao, mkuu wa polisi wa Dallas David Brown amesema.
Maafisa wengine saba wa polisi wamejeruhiwa, Bw Brown amesema.
Kati ya hao majeruhi,wawili wamefanyiwa upasuaji wa dharura na mmoja yumo mahututi.
Ufyatuaji risasi ulianza waandamanaji walipokuwa wakipitia barabara za mji na kuwafanya waandamanaji kukimbilia usalama wao.
Maandamano hayo yametokana na kuuawa kwa wanaume wawili weusi, Philando Castile Jimbo la Minnesota na Alton Sterling eneo la Baton Rouge Jimbo la Louisiana.