Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana July 30 2016 ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Tabora akitokea Mkoa wa Singida.
Mkoani Tabora, Rais Magufuli alizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Nanga na Ziba na alifanya mikutano ya hadhara Igunga na Nzega ambako amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza kutumika kuanzia Jumatatu ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016.
Kuhusu kero ya maji, Dkt. Magufuli alisema Tanzania imepata mkopo wa dola za kimarekani Milioni 268.35 kutoka nchini India ambazo zitatumika kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria katika Miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Sikonge
Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga Masesa Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini kuelekea Nzega Mkoani Tabora.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na wabunge wa Singida
Rais Magufuli katika Kijiji cha Nanga Wilayani Igunga mkoani Tabora.