Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli, amesema uteuzi wake wa wakurugenzi hakubahatisha kwa kuwa sekta hiyo ni muhimu katika maendeleo ya nchi kwa kukuza uchumi na kuondoa kero za wananchi.
Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati Wakurugenzi hao wakila kiapo cha maadili, ambapo amesema ametumia muda mwingi ikiwa ni pamoja na kukesha usiku kuwafuatilia mmoja baada ya mwingine ili asifanye makosa katika uteuzi wake.
Rais Magufuli ameongeza kuwa amezingiatia vigezo vya kila mmoja katika utendaji kazi wake huku akitolea ufafanuzi suala la mkurugenzi mmoja kuwa na cheti cha Hotel Menejiment, na kusema kuwa majina kufanana sio kosa hivyo anaezungumzia kwenye mitandao sio aliemteua yeye.
Amesema kuwa ametumia zaidi ya miezi minne kwa kuvihusisha vyombo mbalimbali ili kuwa fahamu vizuri watu atakaowateua ambao wataweza kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya tano ikiwa ni pamoja na kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi.
Ameongeza kuwa hapo awali ilikua kupata Ukurugenzi kuwa baadhi ya wau walikuwa wanahonga pesa kwa ajili ya kupata nafasi hiyo ambapo amesema kutokana na kulisimamia suala hilo kwa umakini katika kipindi chake hakijatokea kitu kama hicho.
Mhe Magufuli amesema ,Magufuli amesema kuwalikua na mtandao ambao umeundwa kwa ajili ya kupenyeza wakurugenzi wanaowataka hasa katika ofisi za TAMISEMI na tayari ameshaungudua na ameanza kuwaondoa baadhi ya watu waliokuwa wahahusika kufanya udanganyifu huo.