Hapa mkuu wa Wilaya ya Kigamboni akikabidhiwa Ilani ya CCM na kuapa kwenda kuitekeleza kwa vitendo Leo ndio mkuu wa Mkoa wa Dsm anawaapisha Wakuu wa Wilaya wapya wa Dsm.Tukio hili linafanyika katika ukumbi wa Karimjee.
Wakuu wa Wilaya za Temeke,Ilala,Kinondoni,Ubungo na Kigamboni.Wakuu wa Wilaya wanne ndio wamefika isipokuwa Mkuu wa Wilaya mpya ya Ubungo ndugu Humphrey Polepole ambaye hataapishwa leo,sababu ikiwa ni kufiwa na baba yake.
Shughuli hii inasimamiwa na Clouds Media huku ikionyeshwa moja kwa moja kupitia Clouds Tv na MC wa sherehe hii ni Ephraim Kibonde.Wakuu hao wa Wilaya ni
Felix Jackson
Mgandilwa Hashim
Sophia Mjema
Ally S Happi
Baada ya kuapishwa mkuu wa mkoa atatoa muongozo kwa Wakuu wa Wilaya na baadae waandishi wa Habari watapewa nafasi ya kuwauliza Wakuu wa Wilaya maswali ya moja kwa moja kuhusu Wilaya zao na mipango yao
Mkuu wa Mkoa anasisitiza kuwa Wakuu wa Wilaya wana nafasi ya kuingia katika vikao vya madiwani,na haambiwi cha kufanya na Meya,sababu Meya ni Spika tu wa baraza la madiwani na ndio maana nafasi yake ni kuongoza vikao na huitajika ofisini mara mbili tu kwa week.Shughuli zote zinakuwa chini ya Mkuu wa Wilaya ambaye ndie mwakilishi wa Rais katika Wilaya na si Meya.
Mh Makonda anasema ndio maana Meya analindwa na Mgambo wakati Mkuu wa Wilaya analindwa na Jeshi,Polisi na ana usalama wa Taifa,hivyo Mameya wa Dsm wawaache wakuu wa wilaya kufanya kazi zao sbb wapo kwa mujibu wa Katiba ya Tz.
Mkuu wa Mkoa anawaagiza Wakuu wa Wilaya kupambana na ushoga,na kuwa ana taarifa ya NGO iliyopewa dola milioni 70 katika mkoa wa Dsm ili kuimarisha swala la mashoga,ameipa onyo NGO hiyo na kuahidi kuifutilia mbali sababu inatumika kueneza tabia za kishoga ambazo kwa mujibu wa Katiba ya nchi ni kosa linahitaji hukumu.
Makonda amesisitiza kuwa vita ya shisha ndio imeanza,na kwa mujibu wa TFDA shisha ni madawa ya kulevya na husababisha saratani ya Koo,anasema unaenda Double Tree Hotel unamkuta binti mdogo mzuriii halafu anavuta shisha,anaagiza kuwa shisha ni marufuku na yoyote atakayeuza Segerea inamsubiri.Wavutaji wa sigara wote wanatakiwa kuvuta maeneo ya "private" na kama wanataka kuonyeshwa hizo sehemu za Private basi wavute hadharani ndio wataijuwa hiyo "more private" ipo wapi.
Ombaomba wametangaziwa "kiama",kwamba kwenye mitandao watu wameanza kusema zoezi hilo limeshindwa,lkn anawapa week mbili kuhakikisha wameweka mpango kazi kuondoa hawa ombaomba.Watumie mpango kazi na ilani ya CCM kusaidia watu,na baada ya siku 90 wakuu wote wa mkoa watakuja hadharani mbele za watu pale ukumbi wa Mwalimu Nyerere kusema mambo gani waliyoyafanya na kuyapanga katika wilaya zao
Monday, July 04, 2016
Yaliyojiri kutoka Karimjee Hall: Wakuu wa Wilaya za Dar Es Sallam waapishwa leo.
Published Under
KITAIFA
About Author
BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi