Washtakiwa, Mohamed Yusufali “Choma” na Samwel Lema wakizungumza na wakili wao mara baada ya kesi hiyo kuhiishwa.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeahirisha kesi inayomkabili mfanyabiashaa Mohamed Mustapha na mwenzake wanaodaiwa kuiibia serikali shilingi milioni saba kwa kila dakika, kesi hiyo imetajwa kusikilizwa tena Agosti 18, 2016 huku watuhumiwa wakirudishwa rumande.
Hakimu aliyekuwa akisoma shauri la kesi hiyo, Wilbard Mashauri amesema watuhumiwa hawawezi kupewa dhamana na mahakama hiyo kwa kuwa haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa watuhumiwa wa kesi hiyo.
Wafanyabiashara Mohamed Yusufali “Choma”, na mwenzake Samwel Lema ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Northern Engineering Works Limited wakikabiliwa na mashitaka 222 ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 14.
Baadhi ya ndugu, jamaa, marafiki na wanahabari waliofika kuhudhuria kesi hiyo.
Washtakiwa wanadaiwa kujipatia pesa hizo kwa njia ya udanganyifu katika mapato ya serikali, , Samwel Lema, ambao wanadaiwa kusababisha hasara kwa kughushi na kukwepa kulipa kodi.
Watuhumiwa wakitoka kotini.