Mch. Msigwa asems lazima atalipa kisasi | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Tuesday, August 02, 2016

Mch. Msigwa asems lazima atalipa kisasi


KEJELI za Rais John Magufuli dhidi ya vyama vya upinzani lazima zijibiwe, tena bila hofu

Ni kauli ya Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini leo alipozungumza na mtandao huu kuhusu mashari aliyopewa kuhusu kufanya mkutano wake wa hadhara kwenye jimbo hilo.

“Magufuli (Rais Magufuli) amekuwa akitukashfu kuwa vyama vya upinzani ni vya hovyo hovyo na ameua nyoka imebaki mikia inachezacheza. Mimi sitoogopa, nitaongea kama ambavyo rais amekuwa akitukashfu,” amesema Mchungaji Msigwa.

Katika taarifa ya jeshi hilo yanye kumbukumbu Na. IRI/A.24/9/VOLXIII/273 iliyojibu barua ya Msigwa yenye kumbukumbu Na. MB/IR/M/O5 ya tarehe 1 iliyokuwa ikitoa taarifa ya kufanya mikutano ya hadhara mjini humo kuanzia tarehe 3- 22 mwezi huu, imempa masharti ya kuendesha mikutano hiyo.

Sehemu ya barua hiyo inasomeka “mikutano yote hiyo kibali kimetolewa kwako kama Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, sitarajii mtu mwingine kutoka nje ya Mkoa wa Iringa kuja kusemea kuhusu maendeleo ya jimbo lako ama kuja kupokea kero za wananchi wako na kuzijibia wakati hiyo ni kazi ya mwenye himaya ambaye ni wewe.

“Kashfa, kejeli, matusi na maneno ya uchochezi kwa viongozi wa serikali vitahesabika ni uvunjifu wa amani na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yako na zitapelekea kuzuiliwa kufanya mikutano yako inayoendelea.”

Mchungaji Msigwa amesema, kauli iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Iringa, SP Mjengi katika barua yake iliyohusu kufanya mikutano ya hadhara Iringa Mjini ni ya kipuuzi.

“Hii ni kauli ya kipuuzi. Jeshi la Polisi linatoa matamko bila kufuata sheria badala yake linamuogopa Rais Magufuli,” amesema Mchungaji Msigwa.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us