Baadhi ya wanawake wamekuwa wakiona ujauzito kama mzigo,walioubeba na baadhi wakiona kama zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenye miili yao.
Kubeba ujauzito sio jambo dogo,kukibeba kiumbe tumboni kwa miezi tisa kunaweza kuleta msongo wa mawazo.Zipo njia mbalimbali zinazoweza kumpunguzia mwanamke mjamzito msongo wa mawazo.S.ex katika kipindi cha ujauzito ni best S.ex ambayo huwezi kuipata katika kipindi kingine cha maisha na inasiadia kuimarisha misuli katika njia za uzazi hata baada ya kujifungua.
1.Husaidia presha kushuka.
S.ex katika kipindi cha ujauzito inasidia kushusha presha ya damu.Oxytocin, love homoni inayozalishwa kwa wingi mtu akifanya mapenzi inasaidia kupunguza kama sio kuondoa kabisa msongo wa mawazo na kuhakikisha presha iko katika hali ya kawaida ya mwili.
2.Husaidia mjamzito kupata usingizi mnono.
Mjamzito anakumbwa na mambo mbalimbali yanayoweza kumnyima usingizi kama maumivu kwa mbali kwenye uti wa mgongo,kukojoa mara kwa mara,masaa ya kulala kupungua/kuonekana mafupi fetus anavyozidi kukua katika mfuko wa uzazi.S.ex katika kipindi cha ujauzito kunamsaidia mwanamke kufika kileleni na hivyo kupata usingizi mnono kwani huisi kupungukiwa na mzigo(anarelax).
3.Inasaidia mwanamke kuwa karibu zaidi na mumewe kwenye kipindi hiki.
Bond kati ya mume na mke inaendela kuwepo kwani wanaweza kuendelea kufanya mapenzi kwenye kipindi hiki cha ujauzito.Wanawake katika hiki kipindi wanakuwa na hali isiyo ya kawaida na mara nyingi huwa na hasira wanatakiwa kuangaliwa kwa umakini.Oxytocin inamfanya mwanamke awe anajali,na kuamini kuwa mpenzi wake anamjali.
4.Kupunguza maumivu
Homoni kama oestrogen,prolactin na progesterone zinasaidia damu kupita kwa wingi katika maeneo ya nyonga,na hata kwenye uke uongeza hisia na utelezi.