Upungufu wa usalama wa herufi za siri za takriban simu milioni 900 umewapa wadukuzi fursa ya kudhibiti simu za android kote duniani.
Upungufu huo unaowapa wadukuzi mlango wa nyuma wa kuiga herufi za siri uligunduliwa baada ya watafiti wa hali ya ubora wa programu Checkpoint walipojaribu kusuluhisha hitilafu iliyowezesha kirusi kuambukiza makumi ya mamilioni ya simu zilizokuwa na programu zilizoundwa na kampuni moja ya Marekani Qualcomm.
Kampuni hiyo inayounda programu za simu imeuza programu hiyo kwa watengenezaji wa simu milioni 900.
Hilo linamaanisha kuwa simu milioni 900 zipokatika hatari kubwa ya kudhibitiwa na wadukuzi.
Aina ya simu zilizoathirika
BlackBerry Priv na Dtek50Blackphone 1 na Blackphone 2Google Nexus 5X, Nexus 6 na Nexus 6PHTC One, HTC M9 na HTC 10LG G4, LG G5, na LG V10New Moto X ya MotorolaOnePlus One, OnePlus 2 na OnePlus 3Samsung Galaxy S7 na Samsung S7 EdgeSony Xperia Z Ultra
Mkuu wa kampuni hiyo ya kutathmini ubora wa programu katika kampuni ya Checkpoint Michael Shaulov, anasema kuwa
”hakuna ushahidi kuwa tayari simu hizo zimeathirika ila kwa mtizamo wetu ni kuwa mlango uko wazi kabisa mtu yeyote mwenye ufundi na ubora kama wangu hivi anafahamu waziwazi kuwa hakuna hata kizingiti cha kumuibia mtu herufi za siri katika simu hizo tulizotaja hapo juu”
”upungufu unamwezesha mtu wa tatu kumpokonya mmiliki wa simu udhibiti kwani anaweza hata akabadilisha herufi za siri bila yako wewe kujua”
”Ni hatari sana , ni kama mtu amejenga nyumba akaweka mle ndani mali ya thamani ya juu kisha akaondoka akiwa ameacha mlango wake wazi”alisema Shaulov.
Checkpoint tayari imeanza kutoa programu zenye uwezo wa kudhibiti simu hizo na tayari wameipa kampuni ya Qualcomm mbinu za kudhibiti simu hizo.
Njia moja ya kuimarisha usalama wa simu wanasema ni kununua programu kutoka kwa soko maalum la Google Play.
Qualcomm imenyamaza kimya kuhusu ripoti hii iliyotolewa na Checkpoint.