Dar es Salaam. Jumla ya Sh303 milioni zimekabidhiwa kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili kukamilisha matibabu ya upasuaji kwa watoto 138 wanaosubiri huduma hiyo kwa sasa.
Fedha hizo zimewasilishwa leo na taasisi tatu tofauti ikiwemo ya Baps Charities iliyotoa Sh222 milioni, Youth Welfare Trust Sh48,400,000 milioni na I & M Bank iliyotoa Sh33 milioni.
Akizungumzia mara baada ya kupokea msaada huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohammed Janabi alisema fedha hizo zitawezesha upasuaji kwa watoto 138 ambao walitakiwa kufanyiwa upasuaji mwakani.
"Upasuaji tunafanya kwa foleni, wapo waliopangiwa mwakani lakini baada ya msaada huu tuna imani kwamba ifikapo Desemba mwaka huu tayari watoto 138 watakuwa wamefanyiwa upasuaji," alisema.