
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amefika nyumbani kwake katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani
Geita kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais, ambapo akizungumza
na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa
shule ya sekondari Chato, ametoa wito kwa kila mtanzania kuchapa kazi
kwa juhudi ili nchi iondokane na utegemezi...