Dar
es Salaam. Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limesema
Uganda itachagua kupitishia mradi wake wa bomba la mafuta Tanzania kwa
sababu ni nafuu kwa Dola 500 milioni za Marekani (zaidi ya Sh1
trilioni), ikilinganishwa na ujenzi huo ukifanywa Kenya.
TPDC
imetoa kauli hiyo huku kukiwa na maono tofauti juu ya ujenzi wa mradi
huo, ambao unagombewa kati ya Tanzania na Kenya ambazo zina bandari
zinakazofanikisha usafirishaji mafuta kutoka Uganda kwenda soko la
dunia.
Akihojiwa
katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Kituo cha Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC1), Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk James Mataragio
alisema anashukuru hivi sasa Watanzania wengi wanauona mradi huo kuwa
ni suala la kitaifa, hivyo kuupa msukumo unaostahili.
Akionyesha
sababu za Tanzania kupewa nafasi kubwa kushinda mradi huo dhidi ya
Kenya, ambayo ilikuwa na nafasi hiyo tangu mwanzo wa upembuzi wa mradi
huo, Dk Mataragio alibainisha miradi ya Tazama (Bomba la mafuta kati ya
Tanzania na Zambia), Songosongo, Mnazi Bay na bomba la gesi kutoka
Mtwara mpaka Dar es Salaam.
Alisema
miradi hiyo imetoa uzoefu wa kampeni za uelewa juu ya miradi, kutwaa
ardhi kutoka kwa wananchi kwa utaratibu mzuri na kulipa fidia ya
mashamba na mali zilizomo kwenye maeneo yanayopitiwa na mradi husika.
“Kwenye
miradi tuliyoitekeleza hakuna malalamiko kutoka kwa wananchi. Hakuna
aliyepunjwa, hivi sasa asilimia 70 ya umeme unaozalishwa nchini
unatokana na gesi. Haya ni mafanikio ya miradi iliyotekelezwa,
kukamilika kwa bomba hili pia kutakuwa na faida kubwa hasa ajira kwa
wananchi,” alisema.
Aliwataka
Watanzania, kila mmoja kwa nafasi yake kushawishi na kuuvutia mradi huu
na kubainisha faida nyingine zitakazofuata baada ya ujenzi wa mradi
kuwa, ni ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano na gesi na kuongezeka kwa
wawekezaji.
Kutokana
na ushawishi unaoendelea kati ya Tanzania na Kenya, Rais Uhuru Kenyatta
anatarajiwa kufanya ziara nchini Ufaransa kuanzia Jumatato wiki ijayo.
Rais
Kenyatta anatazamiwa kutumia ziara hiyo kushawishi Kampuni ya Total
ambayo inahusika kwenye ujenzi wa mradi huo kulegeza msimamo wake, ili
itumie Bandari ya Lamu kusafirisha mafuta hayo. Kenya inaituhumu
Tanzania kwamba tangu awali ilishindwa kushiriki upembuzi yakinifu
uliofanywa Bandari ya Mombasa.
Mradi
huo ambao utaanza kutekelezwa mwakani na kuchukua miezi 36 kabla
haujakamilika unaweza kujengwa njia tatu zilizopo. Kwanza ni kutoka
Hoima mpaka Bandari ya Mombasa, au ile ya Hoima mpaka Bandari ya Lamu,
zote za nchini Kenya. Ya tatu ni Hoima mpaka Bandari ya Tanga