kuisha, utafanyika msako mkali katika wilaya zote za mkoa huo na watakaokamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mkuu huyo wa mkoa Mara aliyasema hayo juzi kwenye kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa huo pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda.
Kikao hicho pia kiliwashirikisha wakuu wa wilaya zote sita za mkoa huo na wakurugenzi wote wa halmashauri.
Mulongo alisema watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria wanatakiwa wazisalimishe mara moja katika vituo vya polisi au kwenye ofisi yoyote ya serikali na kwamba watakaozisalimisha ndani ya muda huo hawatachukuliwa hatua yoyote ile.
Aliwataka wanaomiliki silaha kihalali ndani ya muda huo wazipeleke polisi ili zifanyiwe uhakiki na kuwaagiza wakuu wa polisi, wilaya kuwanyang’anya wote wanaotumia silaha visivyo hata kama wanazimiliki kihalali.
Alisema baada ya muda huo wa wiki tatu kuisha atatoa amri halali kwa kushirikisha mahakama na kuwakamata wale wote wanaomiliki silaha hizo kinyume cha sheria.
Katika hatua nyingine, Mulongo alisema uhakiki wa watumishi mkoani humo kwa kipindi cha mwezi mmoja tu, umebaini kuwa kuna watumishi hewa 84 ambao kwa kipindi hicho zimekwishatumika Sh milioni 105 kuwalipa mishahara.
Alisema halmashauri inayoongoza kwa kuwa na watumishi wengi hewa ni ya Bunda yenye watumishi hewa 35 na kuongeza kuwa halmashauri ambazo hazina watumishi hewa ni Butiama.
Alisema pia wamebaini kuwa watumishi hewa wengine sita ni wa wizarani hasa wanaofanya kazi katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda (DDH) na watumishi hewa hao wamo ambao tayari wameshafariki dunia na wastaafu.