SIMULIZI FUPI: NILIKUWA NA MPENZI
MTUNZI: George Iron Mosenya SIMU: 0655
 727325;
 Mwanzoni sikumpenda kutoka moyoni, nilimpenda kwa kuwa tu 
alikuwa mrembo haswa.
.kwa kifupi nilimtamani tu….yaani nilitegemea 
akinivulia nguo zake tukashiriki tendo hamu yangu itaisha na nitaachana 
naye. Ndio ningeachana naye kwa sababusikuona umuhimu wa kudumu na 
msichana ambaye sijui hata kama nitamuoa.
Nilipomwambia tutaoana hakika 
nilidanganya Alinipenda sana, kadri siku zilivyokwenda alizidisha upendo
 wake kwangu. Hakuna nilichohitaji kwake akaninyima, aliwahi kumdanganya
 baba yake kuwa anaumwa akatumiwa pesa ilimradi anipatie mimi 
nilipomwambia kuwa kuna mtu ananidai na abananisumbua kwelikweli.
 Alisikitika kusikia vile, akaahidi kunipigania. Haikuwa kweli 
nilichomwambia juu ya kudaiwa, pesa ile aliyonipa niliitumia kulipia 
chumba nikafanya uzinzi na Fatuma. Alihadithiwa habari hiyo na marafiki 
walioniona nikiingia kule, akalia kwa uchungu mbele yangu, lakini neno 
lake la mwisho likabaki kuwa ‘NAKUPENDA SANA…..WEWE NI MWANAUME WA 
MAISHA YANGU’……..Nilij isikia vibaya lakini nafsi nyingine ikanikumbusha
 kuwa nilikuwa katika mahusiano na msichana yule kwa sababu moja 
tu…NGONO… na katu hakutaka kushiriki ngono na mimi. Alinikwepa sana hadi
 nikajisikia vibaya.
 Nikahisi huenda ana mtu mwingine. Hakika nilidhani 
kuwa anajihusisha na mtu mwingine ambaye hushiriki naye tendo hilo la 
ngono ambalo kwangu mimi kilikuwa kitu pekee ambacho kingeweza 
kuniaminisha kuwa ananipenda kweli.
 Msichana mrembo kama huyo kamwe 
asingeweza kuishi bila kufanya mapenzi. Hakika haikuniingia akilini. 
Wangapi wenye ,ali zao wanamtongoza, yeye ni nani hadi asiingie 
majaribuni?? Hapana ni uongo mtupu ananiongopea mimi. Nikaendelea na 
vimbwanga vya hapa na pale. Hakuchoka kunibembeleza, hakuchoka kunipenda
 na hakuchoka kunikumbusha kuwa ni mimi pekee nilikuwa katika moyo wake 
wa nyama. “Nikipotea jumla nd’o utajua kuwa nilikuwa nakupenda..” 
aliwahi kunambia neno hilo. Japo lilinigusa lakini sikulitilia maanani. 
Hatimaye tukamaliza shule, 
nikategemea kuwa ule muda wa kumfaidi 
msichana yule kingono ulikuwa umewadia. Lakini haikuwa hivyo, akaendelea
 kuwa mgumu huku akijitetea kwa sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu.
Mwanzoni nilidhani kuwa aliogopa kufanya mapenzi kabla hajamaliza shule,
 lakini ajabu hadi tulipomaliza bado alisimamia msimamo. Sasa nikajikuta
 katika pepo mbaya, nikaanza kumwonyesha hadharani kuwa nina wanawake 
wengine. Japo chozi lake liliniumiza sana lakini sikujali. Kwa nini 
ananinyima penzi binti huyu? Nilijiuliza. Hatimaye nikafikia uamuzi wa 
kuachana naye. Lakini siwezi kuachana naye bila kumjua ladha yake.
 Nilijiapia kuwa jambo hilo haliwezekani hata kidogo, mimi kama mwanaume 
kamili atanitangazaje kwa marafiki zke, kuwa sijawahi kulala naye 
tukafanya tendo??? Aibu kubwa!!! Nikampangia shambulizi moja la mwisho 
na kama ni ubaya uwe ubaya tu. Ilimradi nilishapanga kuachana 
naye….haitanidh uru lakini lazima nifanye naye tendo Nilimuita nyumbani 
kwangu, ilikuwa mida ya jioni. Alipofika nilimlaghai hapa na pale 
nikamgusa matiti yake madogo yaliyosimama wima yakijitahidi kunidhihaki.
 Na yalifanikiwa hasa hasa kunikebehi. Nikamgusa huku na kule..nilipotak
 a kumvua nguo akanizuia. Nilikuwa nimekunywa pombe kiasi hivyo sikuwa 
na aibu, nikaamua kutumia nguvu, niliamua KUMBAKA…..nikai chana sidiria 
yake, kisha nikaiondoa chupi yake sasa akabaki yu uchi wa mnyama. 
Alihaha huku na kule asiamini kile kinachotokea mbele yake. Nikamrukia 
ili niweze kutimiza lengo… Kamwe sikuwahi kumwona binti huyu akiwa 
katika uoga namna ile…alikuwa amekodoa macho yake….na alikuwa 
anatetemeka… Akataka kukimbia uchi, nikamdaka mkono nikamvutia pale 
nilipokuwa. Sikuwa nahuruma hata kidogo, nilichotaka ni itu kimoja 
tu..NGONO KISHA AKINICHUKIA NA ACHUKIE. Mara akatokwa na kelele kubwa 
sana zilizonishtua sana. Amakweli sikuzitegemea. Sikudhani kama amnaweza
 kufanya tendo lile “ANANIBAKAAAAA, NISAIDIEENI ANANIBAAAKA…..” ilikuwa 
kelele kubwa haswa, na alifanya kwa kurudia rudia Kelele zikawafikia 
wasamalia wema, binti akaendelea kupiga kelele. Hatimaye mlango 
ukavunjwa, wasamaria wakanivagaa na kuanza kunipiga……nilip igwa hadi 
nikapoteza fahamu.
 Nilipozinduka nilijikuta na pingu mkononi, pingu 
iliyounganishwa na kitanda. Nilikuwa na maumivu makali mwili mzima. 
Nikakumbuka kuwa nilifumaniwa nikitaka kufanya ubakaji. Pombe zilikuwa 
zimenitoka na niliona aibu wa kitendo cha kinyama nilichotaka kumfanyia 
Maria. Baada ya kujitambua vyema na nguvu kunrejea mwilini nilirejeshwa 
mahabusu. Nikaingia mahabusu nikikabiliwa na kesi mbaya ya ubakaji. SIKU
 NNE baadaye nilikuja kutolewa……hapak uwa na dhamana lakini ilikuwa 
barua tu ya kustaajabisha niliyokutana nayo.
 “Mpenzi Christopher 
mwanaume wa maisha yangu…..haikuwa nia yangu kukusababishia kipigo 
kikali na kuitwa mbakaji… nimefan ya haya kwa sababu nakupenda kutoka 
moyoni…napenda uishi miaka mingi..Chriss ni wewe mwanaume pekee 
niliyetokea kuvutiwa naye kihisia ukauteka moyo wangu na kujikuta nikiwa
 mtumwa wa mahaba yako… lakini nina mapungufu makubwa…nina kasoro kubwa 
ambayo hainipi hadhi ya kulala kitanda kimoja na wewe…..Chriss mimi 
ningekuwa muuaji iwapo ningekuruhusu unibake….hivi chriss unadhani 
mpapaso wako haukunisisimua?
Nilisisimka haswa na nilitamani nikutimizie
 kwa hiari kile ulichotaka, labda mimi nilikuwa muhitaji kuliko wewe 
mpenzi lakini…..lakini nisingeweza kukuua, ….Chriss ninayo furaha na 
wala usisikitike kusikia hili, mimi nimefurahi sana kufa nikiupigania 
uhai wa mwanaume niliyempenda, ninayempenda na ninayekufa kwa ajili 
yake.
 Kitanzi hiki kiwe kumbukumbu yako milele kuwa NILIKUPENDA…….C 
hriss mimi ni muathirika wa gonjwa la UKIMWI niliambukizwa na wazzi 
wangu …nilizaliwa nikiwa na Ukimwi Chriss, mama kabla ya kufa alinikanya
 kuwa nisiwe na tabia kama ya marehemu baba ambaye alimuambukiza maksudi
 kutokana na taba yake ya kutotulia nyumbani, mama akanikanya kuwa ni 
heri nife peke yangu kuliko kuua yeyote asiyekuwa na hatia.
 Na huyo mtu 
ni wewe Chriss haukuwa na hatia na haukustahili kufa..…..laiti kama 
ungenibaka basi leo hii ningekufa nikiwa MUUAJI… ninafura hi kuwa nakufa
 kama SHUJAA. Nimeyaadika haya huku kitanzi kikiwa shingoni mwangu, 
nakufa leo lakini wakuache wewe huru. Huru kabisa, naenda kuungana na 
mama yangu nimweleze kuwa sikuwahi kuua duniani na nimeamua kuondoka ili
 siku moja nisije kuua yeyote. Ubaki salama Chris wangu” Nilijikuta 
napoteza fahamu tena baada ya kuhakikishiwa kuwa Maria alizikwa baada ya
 kujinyonga katika chumba chake nyumbani kwao nabaruaile ilikutwa chini 
ya miguu yake iliyokuwa unaning’inia……. nilipozinduka nilikuwa nyumbani 
kwetu…kila jicho lilinitazama kwa namna yake……wengine kwa hasira wengine
 dharau na baadhi kwa huzuni.
AMA KWA HAKIKA nilikuwa na mpenzi 
aliyenipenda kwa dhati……. UPUMZIKE PEMA PEPONI Maria…..kamwe sitakusahau
 mpenzi……. UJUMBE; Usilipize baya kwa baya kwa kizazi kisichokuwa na 
hatia…..JIFUNZE kupenda kwa dhati lakini HISIA ZAKO ZISIKUFANYE 
MTUMWA!!!! SHARE KWA WENGINE MWISHO!!!...
Wednesday, March 16, 2016
SIMULIZI FUPI: NILIKUWA NA MPENZI
Published Under
HADITHI
About Author
BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi