Wednesday, March 16, 2016
Tatizo la nguvu za kiume, maana yake na tiba – 4
Published Under
HEALTH
ulevi kupita kiasi wa pombe, madawa ya kulevya husababisha mwanaume kupoteza nguvu za kiume. Msomaji ningependa kukujulisha kuwa tafiti zinaonesha unywaji pombe unaathari nyingi
katika afya ya binadamu, husababisha tatizo la kuharibika kwa ini (Liver damage), uharibifu wa mfumo wa fahamu (Nervous system) na kuvuruga mpangilio wa uzalishaji wa tezi za uzazi wa kiume na hatimaye kusababisha upungufu wa nguvu za kiume. Endelea…
Msongo wa mawazo au uchovu kupita kiasi
Hii husababisha mwanaume kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa hata anapokuwa katika sita kwa sita na mke wake. Msongo wa mawazo unaufanya mwili kushindwa kuzalisha kiwango cha kutosha cha vichocheo vya kufanya tendo la ndoa.
Ili mwanaume aweze kuwa na hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa lazima tezi dume lake liwe na afya bora. Madini ya zinki ambayo hupatikana kwa urahisi katika maharage, vitunguu, matango, karoti, spinachi, kabichi na matunda mbalimbali husaidia kufanya tezi dume kuwa imara.
Kuna mambo mengi yanayosababisha tatizo hili kama vile ugonjwa wa ngiri na kupooza kwa mwili. Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vema ukafuatilia makala haya.
About Author
BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi