Alikiba ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa radio, na kusema kuwa hivi karibuni kuna timu ya mpira imemfuata kumtaka kujiunga na timu hiyo, lakini atakuwa na masharti ya kujiunga, kwa sababu bado anaupa kipaumbele muziki kuliko mpira.
“Nitakuwa na condition zangu katika mpira kwa sababu muziki kwanza, kuna timu imenifuata hivi karibuni, lakini nahitaji ufree ambao hauwezi kunibana, nikiamua nina nafasi nafanya mpira”, alisema Alikiba.
Alikiba amesema iwapo atajiunga na soka na kulisakata kabumbu, haitakuwa na manufaa kwake tu, bali hata kwa mashabiki kwani watapata fursa ya kutengeneza pesa, pamoja na kuongeza mashabiki kwake na timu hiyo ya mpira.
“Unajua siku hizi promotion ni kitu cha msingi sana, niko na fans wengi sana kwa hivyo kuna watu ambao wananifuatilia wanaangalia either wanaweza wakawa mafans wa timu ambayo nitaenda kuchezea, kwa sababu najua mimi naenda kucheza sio kwa kucheza tu, kutakuwa na vitu vingi kwa hiyo watapata faida ya vitu vingi, watauza jezi na vitu kama hivyo”, alisema Alikiba.