Hali ya siasa nchini ni ya hamasa, lakini isiyokuwa na misingi endelevu.
Kwa kuwa Rais amekuwa akigawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo ambacho ni bunge.
Pia nasononeshwa ninapoona watu wanaachishwa kazi na mashirika mbalimbali kwasababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo.
Bandari sasa hivi nasikia uingizaji mizigo umeshuka kwa asilimia 50, kampuni nyingi za mizigo zimefunga shughuli zake na pale palikua na vijana wetu wengi wameajiriwa,sasa hivi wako mtaani hakuna mbadala wa ajira, hii inasababisha hali ya maisha ya wananchi yanakua magumu.
Kuhusu swala la MCC ni pigo kwa mustakabali wa uchumi, kutaka nchi ya viwanda kunahitaji uwekezaji mkubwa,katika hili fedha tutatoa wapi kama sio wafadhili wa ndani na nje kufanikisha?
Hawa wafadhili sio watu wa kuwabeza kwakuwa tunafanya nao miradi mingi ya kimaendeleo na wanavyotoka hivi itaturudisha nyuma, Tunahitaji kujitegemea, ndiyo, ila kwa mipango huku tunatafuta mbadala wa kila msaada.
Hapa kinachotakiwa ni kufanya mabadiliko katika mfumo na kuufanya kuwa endelevu.