Alisafirishwa hadi mjini Landon wiki moja iliopita kwa matibabu.
Akithibitisha kifo chake rais wa Kenya 
Uhuru Kenyatta amesema kuwa kenya imesikitishwa na kifo cha mama Lucy 
mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki.
Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari Uhuru amesema bi Lucy amekuwa mgonjwa kwa kipindi cha mwezi mmoja .
Amesema kuwa Kenya imempoteza mwanamke 
aliyechangia mengi katika maendeleo ya taifa la Kenya hususan katika 
vita dhidi ya ugonjwa wa ukimwi.
Rais ametuma risala za rambi rambi kwa mtangulizi wake Mwai Kibaki pamoja na familia yake.
Via>>BBC